Mimi ni binadamu kwa sababu hili umbile ni kibinadamu na linamilikiwa na binadamu
Habari ndugu yangu, sijakuelewa vyema hapo. Umesema umbile lako ni la kibinadamu na linamilikiwa na binadamu, lakini kama umesoma vyema mada ilikuwa inasema kuwa:
Umbile hilo linamwisho wake, kila kitu hapa ulimwenguni kina cause na effect, mwisho wa jambo fulani ni chanzo cha jambo fulani na chanzo cha jambo fulani ni mwisho wa jambo fulani. Hivyo mwili huo ni wa muda, ni kama barafu, huyeyuka na kuisha na maji hubakia, sisi tunapenda kuuliza je maji hayo au chanzo chako kikuu cha asili ambacho hivi sasa hata ukikitaja unaweza kukihisi au kukitambua ni chanzo gani?
Pili umesema kuwa mwili wako unamilikiwa na binadamu, mwili wako haumilikiwi na binadamu bali mwili wako unamilikiwa na ufahamu. Kama mwili wako hauna ufahamu tutasema umekuwa kicha, umekufa, au umelala. Mwili wako pia hauwezi kumilikiwa na mwanadamu kwani mwili wako ndio unaokufanya wewe ujulikane ni mwanadamu.