Pendaelli
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 13,075
- 38,625
Kukata tamaa ni moja wapo wa mfumo wa hisia kwa binadamu kutaka kurudi kawaida au kujipa tumaini lingine.
Nadhani haiwezekani kujipa moyo kabla kujiwa na hisia za kukata tamaa.
Mbaya ninile kukata tamaa moja kwa moja, hii ni kiwango kikubwa cha maumivu ya ndani yalio kosa kupoozwa .
Binafsi nikiangalia mtindo wa maisha yangu, mwenendo wangu, makuzi yangu , na mfumo wa maisha kwa sasa nakata tamaa kabisa ,ila kila ninapo kata tamaa na kumbuka kuna watu wao tumaini lao ni kwangu kama baba, wao wakiniangalia wanaona kesho yao bora kupitia kwangu halafu mimi nimekata tamaa! Aisee nalengwa kidogo na machozi lakini naamka na kujipa moyo na matumaini makuu, kuna pambazuka kuna kuchwa siku zinaenda , ila yote ya yote siachi kushukuru kwa kila yote.