Umeshawahi kukata tamaa ya maisha? Ipi ilikuwa sababu

Kukata tamaa ni moja wapo wa mfumo wa hisia kwa binadamu kutaka kurudi kawaida au kujipa tumaini lingine.

Nadhani haiwezekani kujipa moyo kabla kujiwa na hisia za kukata tamaa.

Mbaya ninile kukata tamaa moja kwa moja, hii ni kiwango kikubwa cha maumivu ya ndani yalio kosa kupoozwa .

Binafsi nikiangalia mtindo wa maisha yangu, mwenendo wangu, makuzi yangu , na mfumo wa maisha kwa sasa nakata tamaa kabisa ,ila kila ninapo kata tamaa na kumbuka kuna watu wao tumaini lao ni kwangu kama baba, wao wakiniangalia wanaona kesho yao bora kupitia kwangu halafu mimi nimekata tamaa! Aisee nalengwa kidogo na machozi lakini naamka na kujipa moyo na matumaini makuu, kuna pambazuka kuna kuchwa siku zinaenda , ila yote ya yote siachi kushukuru kwa kila yote.
 
Dah kumove on Kwangu labla nipate sehemu kama hiyo tena aisee ila bila hvy najiona nikizidi kuumia, sio kwa kupenda bali n sehemu ambayo automatically utakuta najua mambo yanayoendelea hapo na ndo naumia tena.

Baba labla kuna vitu kwenye maisha sio lazima viende vile unataka ili kupata furaha na faraja ya kuishi,

Life has soo much to offer! Hiyo dream job yako isiwe chanzo cha maumivu while unaweza kuishi na kufanya vitu vingine vizuri zaidi

Ni kampuni ipi kwani?
 
Pole sana sana Joanah kwa yote uliyopitia. Kupoteza kazi ya ndoto yako kwa figisu na uongo ni jambo gumu sana, linavunja moyo na kukuacha na maswali mengi. Na pia kupoteza mama ni maumivu makali mno, na kupitia machungu ya mahusiano pia kunaacha kovu. Ni kweli, inachukua muda mrefu sana kupona kutoka kwenye majeraha kama haya, hasa pale akili inapokumbuka.

Mbaga Jr, nakuelewa kabisa unavyosema ni ngumu kupona wakati unazungukwa na mazingira yanayokukumbusha maumivu. Hiyo inafanya safari ya uponyaji iwe ndefu na yenye changamoto zaidi.

Lakini ninyi wote wawili, na wengine wote tunaopitia nyakati ngumu, msikate tamaa. Maisha yanaweza kuwa magumu sana wakati mwingine, lakini ndani yetu tuna nguvu kubwa ya kusimama tena. Chukua muda wako kupona, jipe nafasi ya kuhisi maumivu, lakini usikubali yakutawale kabisa. Hatua ndogo ndogo za kujiweka sawa zinahesabika. Na kumbuka, haupo peke yako kwenye hili, wengi wetu tumepitia au tunapitia changamoto kama hizi.

Tukumbushane tu, baada ya mvua, jua huchomoza tena. Msiache kutafuta mambo yanayowapa furaha na amani, hata kama ni madogo kiasi gani.
 

cocochanel huu sio mwandiko wako bhana
 
Nimesoma hii nimeishia kuumia mno, ndiyo kipindi ninachopitia hivi sasa, nahisi moyo wangu unavuja damu, Mungu anisaidie tu nivuke salama huu msimu bila kuchukua maamuzi yoyote magumu..!

Ngoja kwanza nikalie tena..!πŸ™ŒπŸΎ

Pole sana sis
This too shall pass! Jipe muda,take it easy β€πŸ«‚
 
Asante sana aisee πŸ™
 
Yah nakuelewa mamaa, na nazidi kusonga mbele hata kama bado nna machozi


Dah hapa hata cjui nikujibu nn aisee,
Anyway, n TV station, Hua wanaonyesha content fulani hv ambayo Wabongo wengi wanapenda sana

Yeap! Muhimu songa mbele braza labla,with time hayo machozi yataisha itaendelea kubaki history

Ooh ni TV station wabongo wengi wanaipenda ama ni tbc2 uloniambia ile siku?
Nwei,kwenye TV huko sina ninalolijua kwasababu siangalii TV kabisaaa
 
Nimesoma hii nimeishia kuumia mno, ndiyo kipindi ninachopitia hivi sasa, nahisi moyo wangu unavuja damu, Mungu anisaidie tu nivuke salama huu msimu bila kuchukua maamuzi yoyote magumu..!

Ngoja kwanza nikalie tena..!πŸ™ŒπŸΎ
Mkuu, mm mwnyw ilifikia hatua nawaza kujiua aisee, nashukuru Mungu kuna watu walikuwa nami japokuwa walishindwa kunisaidia Ila nikajikaza nikavuka Huko.

Mm nasonga mbele huku nalia, cha msingi n kusonga mbele hata kama n kwa 1 cm

Nawe jitahidi ukaze Aisee, mana utajiumiza na maisha yataendelea kusonga mbele bila kujua lolote khs ww.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…