Ilishawahi nitokea , kuna wadada wawili walikua barabarani mmoja ni mkali kinyama ndie nilie mpenda wa pili ni mmasai mmoja mwenye sura yake personal.
Lengo langu niwafuate niombe no ya yule pisi ,ili kutomfanya yule mwingne asijiskie vibaya nikajifanya kuomba no zao wote, mbaya zaidi asiye kwenye lengo ndio akajitia kiherehere cha kunipa no ,yule pisi yeye kimya tu , nikaichukua kishingo upande ,,nikajua kwa sababu ni marafiki naweza pata ukaribu na huyo, ila lengo nisijempoteza yule pisi kupitia mwenzake.
Kufupisha tu ni kwamba yule dada wa kimasai aliniganda hatari zaidi ya mwaka , ili kutomfanya asijisikiie vibaya sikudhubutu kumwambia ukweli , nikawa nawasiliana nae kishingo upande ,alipo kuja kuharibu zaidi alinitambulisha kwa yule pisi kama mimi ni mtu wake, na ile pisi ikawa inaniita shem.
Hali ilizidi kuwa mbaya zaid pale nilipotambulishwa umasaini ikafika hatua mpka kaka wa binti walipo diriki kutamka watanipa n'gombe 100 .
Kilichonifanya nikaingia mitini kabisa ni pale binti alipo fikia hatua ya kutaka kunitunuku zawadi ya bikra yake na akaniambia hiyo kwao ni zawadi kubwa kabisa ya kimila .
MpKa Leo sikuwahi kukutana na pisi kali kama yule rafiki wabinti wa kimasai , nilikuja kupata fununu karudi kwao Rwanda baada ya kumaliza masomo yao pale KCMC .