Umeshawahi kupiga One katika levo yoyote ya elimu? Tukutane hapa

Umeshawahi kupiga One katika levo yoyote ya elimu? Tukutane hapa

Mm nimekutana na dogo ana 23 yrs ana 1b! Ana elimu ya std 4!
Ana utitiri wa mitumbwi ya kuvulia acha kbs .yaan kijiji kizima wanamtegemea yeye! Narudia ana 1b...alinionesha akaunt nikarudi gheto kulala!
Kuna jamaa amesomeaga dit ni kichwa balaa... alikua kampuni fulan.maarufu...nimewah kaa naye kama 8mths migodini akisoma mchezo ajabu yulr jamaa ana maisha ya kimaskini kbs...mm nilikua nikifeli mishe zangu ile nna stress yy ndo alikua ananisovia fasta mambi yananyooka[emoji38][emoji38]!
Anakupa idea anakuchorea kila.kitu kwa kitabu anakuambia hebu ifanye utatoka..ila yy kila kitu walaaa...nikaja gundua ni mwathirika wa forex...yaan anahitaji sana maombi...anachoma hela balaa forex...! Haya maisha mm siyaelewagi pia[emoji1787]!
Kifupi ushukuru tu kwa kidogo unachopata
Kitu usichojua biashara sio kwaajili ya kila mtu, kuna watu wana idea ila hawajui kuzifanyia kazi, kuna watu wana pesa ila idea ya kuzizalisha zaidi hawana. Na kuna watu wana vyote sasa akizichanganya ndio hao kina bill gates.
 
Kitu usichojua biashara sio kwaajili ya kila mtu, kuna watu wana idea ila hawajui kuzifanyia kazi, kuna watu wana pesa ila idea ya kuzizalisha zaidi hawana. Na kuna watu wana vyote sasa akizichanganya ndio hao kina bill gates.
Hakika...naielewa hii
 
Mkuu physics ni noumer,pamoja na ufaulu wote huo,sasa naishi maisha kama shetani japo nina master's ila dah!!!!! Mpaka hua najuta sana kusoma
Hahahhaaa, unaishi kama mashetani,, hapo unalinda legacy ya mwendazake kabisa.

Mimi nimeishia kwenye kadigrii tu, nimeapa siendelei tena, ngoja niisake A ya kitaa tu.
 
Form 4 nlipiga division 3 ya kuchechemea

Form six nikapiga 2 ya kuchechemea.


Kiukweli bila ajira ningeviuza hivi vyeti hata kwa laki moja nikatafute karai, mkaa na mahindi mabichi ya kuchoma maisha yaende.

Cha. muhimu hichi cheti kikusaidie kuingiza pesa tu aidha kwa kuajirika ama kujiajiri, zaidi ya hapo itabaki stori tu "yule jamaa alipata matokeo mazuri zamani"
 
Std 7, nilipata A masomo yote, na wastani A, nikachaguliwa kujiunga ktk shule 1 kongwe ni ya bweni na ni jinsia 1,

O level, nilipata div 1 ya 11, nikachaguliwa shule ya vipaji maalumu mchepuo wa sayansi,

A level, nilipata 1 ya 6,..

Naendelea kupambana na maisha.
 
Naielewa sana Advance hasa kwa PCM, PCB, PGM.

Akikaa kimya hilo ni jibu tosha.

Nilibahatika kuangukia miongoni mwa kombi hizo hapo juu, cha mtema kuni nilikiona, ila namshukuru Mungu, Physics ilinipa sana heshima
Kwani phys ya mchezo bas? Inanyoosha watu hatari. [emoji23][emoji23]
 
Wiki ya kwanza baada ya kuripoti na kuanza kusoma mchezo.
Ticha wa Phyz aliingia akapiga Projectile, Error and Dimension na Simple Harmonic Motion ndani ya kipindi kimoja cha dk 40, darasa zima tulipigwa na butwaa. Mimi binafsi nilipaniki, hadi nikaugua na kurudi home(kwa mlezi) kwanza.

Nilipoulizwa maendeleo ya shule, nilisema mambo ni hatari(uzuri huyu mlezi aligonga PCM anajua mziki wa Phyz).

Baada ya kupona nikatangaza vita moyoni mwangu, now the rest is history.

Sasa huku kitaa ndio kimbembe, Hamna kudrive formula kwanza kama nilivyokuwa nafanya kwenye physics, hahahahaa
Phys km hukusoma tuit, afu uende special lol, wallah nilijuta yaan
 
Std 7, nilipata A masomo yote, na wastani A, nikachaguliwa kujiunga ktk shule 1 kongwe ni ya bweni na ni jinsia 1,

O level, nilipata div 1 ya 11, nikachaguliwa shule ya vipaji maalumu mchepuo wa sayansi,

A level, nilipata 1 ya 6,..

Naendelea kupambana na maisha.
Hongera sana, shule zilizokuwa zinaitwa za vipaji maalumu niliishia kuzisikia kwenye soga
 
Sitasahau mabao niliyokuwa nayapiga kwenye chumba cha mtihani wa Physics, hahahahaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] phys bhana, inakuumbua kwenye paper, unabaki kushangaa tyuuh. Sina hamu kabisa.
 
Phys km hukusoma tuit, afu uende special lol, wallah nilijuta yaan
Wote wanaopata B na C za Advance Phyz nawaheshimu sana.

Phyz unaweza kuisoma kwa nguvu zote na ukaishia kuambulia mswaki kabisa
 
Back
Top Bottom