Umeshawahi kupotea Kariakoo? Juzi ilibaki nukta nipige mayowe

Kwa staili hii lazima upotee
 
Nini Kariakoo, mi jana usiku nimepotea Tandika sokoni kuitafuta stendi ya magari ya kwenda Gerezani
Kwa asiyefika Tandika anaweza kushindwa kukuelewa lakini aliyewahi kufika, wala hashangai kusikia ulipotea!!
 
Kwa staili liyofanya, ya kununua nguo halafu anaacha hapo hapo kisha anaenda sehemu nyingine na nyingine ili apitie baadae; my braza, hata kama unaifahamu vizuri mitaa lazima utachanganya madesa tu kwa sababu hapo issue ni zaidi ya kujua mitaa bali kujua nini ulinuua wapi!!!
 
watu bwana mnapoteaje kkoo yaani ww unakodi bajaji toka mnazi mmoja mpka gerezani kwa 4000 wa mikoani mnachekesha
Huyo mimi ndo nimemshangaa kwa sababu kwa mjanja, hata kama alishapoteza network, baada ya kuambiwa angeendelea tu na safari hadi Mnazi Mmoja, na baada ya kufika pale, network zingesoma mnara za kujua anatakiwa kuelekea wapi!
 
Aiseee watu wa mikoani bhana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]


Unapoteaje kariakoo
Kuna mtu ni yupo Dar kuanzia mwaka 98. Aliniomba nimsindikize kariakoo nikajua labda anataka kampani yangu tu. Kufika kariakoo ndio nikashtuka anapajua mtaa wa msimbazi na uhuru tu.
 
Mkuu wewe kiboko [emoji120][emoji120][emoji120] nimepata shule ya maana hasa hiyo Google.
 
Binafsi sija wahi kupotea kariakoo ni mzoefu mzuri tu, maana deilee nakuwa huko.

Kuhusu masuala ya kupotea nili wahi potea nikiwa na mwanangu mmoja kawe beach, mwaka 2019 tulitaka tutembee mpaka masaki, ambako tulikuwa hatupafahamu ili tulijue Jiji vilivyo. Bwana eeh... hatukujua tu, tulifanya makosa makubwa sana.

kwani hiyo masaki tulifika basiii.... [emoji19] Tulianza kutembea saa 6 mchana mpaka saa 1 usiku hatuja fika masaki na tulivyo ghairi kwenda msaki tukaamua kuelekea morroco tukaanza kuitafuta njia inayo weza kutufikisha Morocco nayo tukaikosa, sito sahau [emoji23][emoji119]

Bahati nzuri katika pita pita zile tukakutana na jamaa mmoja alikuwa fundi rangi tukamuuliza njia ya kwenda Morocco ni ipi...?

Akatuambia mbona mnaelekea baharini sasaa...? [emoji23] nakumbuka hayo maeneo yalikuwa pale village supermarket msaki, karibu na Tanganyika International school. (kwa sasa ni master sipotei kindezi)

Yule jamaa alikuwa msaada mkubwa sana kwetu. Mungu ali bariki tulitoboa ila hapo dira kichwani ilitoweka kabisa maana hatukuwa tunaelewa mashariki wala magharibi [emoji22] yaani kwa ufupi hatukujua tunakokwenda, niki kumbuka huwa nacheka sana. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Maana kwa sasa naishi huku huku masaki niliko potea miaka mi 3 nyuma. [emoji847]
 
Karikoo paache tu unaweza ukapotea ukazura weeeeee hadi ukaamua kuuliza mpita njia "hivi uliniona napita hapa"!?[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Halafu anakuambia mara ya tano hii nakuona
Nikadhani we kachero [emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23] nkafkiri n mm pekee angu nnayeendaga mnazi mmoja badala ya karume
 
Nini Kariakoo, mi jana usiku nimepotea Tandika sokoni kuitafuta stendi ya magari ya kwenda Gerezani
Nilishapotea mara mbili huko. Vituo vinahama sana. Nilishushwa eneo tofauti nikaamua kufuata tu watu. Ghafla naona watu wanapungua na sijafika kituo cha buza. Tandika...
 
Unadhani ishu ni kujua majina, sio ishu hiyo
Mimi nina experience ya kupotea pia na nilikaa karikoo miaka miwili

Yani siku ya kwanza nilimsindikiza mama mitaa ya aggrey kununua vyombo kwaa jili ya biashara aliyoanza
Huwezi a mini pamoja na uwenyeki wangu niliojikuta ninao baada ya kufanya manunuzi maduka kama saba na zaidi, muda wa kukusanya tulishindwa kukumbuka baadhi ya maduka yalipo, hadi jamaa mmoja wa kampuni ya usafirishaji ambaye ndio awali aliyupeleka kila duka ili kununua alipokuja na kutupeleka mote tulipopita maana yeye tulikuwa nae hiyo awali na alikumbuka hayo maduka na alifahamiana na wauzaji

Kumbuka maduka mengi ya kariakoo yana majina ila mengi pia haya a vibao vya majina ama, hayo majina yapo kwa maandishi madogo
 
Miaka hiyo rafiki yangu na mwenzake wakiwa wageni high school Dar kutoka Moshi wakapanda uda Mtoni - Kkoo. Ilikuwa weekend, kufika kkoo hawaoni soko watu wote wameshuka, wamebaki wao, wakamfuata dereva na inspekta kule mbele:
"Eti baba hili basi halifiki Kariakoo?"
"Kariakoo ipi".
"Kariakoo ya sokoni..."
Wanasema wale wababa walicheka mfululizo ikabidi wao washuke. Kukata tu kona soko hili! walisimulia tukio hili baada ya muda mrefu sana.
 
🤣🤣🤣🤣 utaachaje kucheka sasa..
Sema ukipotea ukimuuliza konda au Teja, tarajia kila mtu ajue, maana atataka aoshee kwako, ataongea kwa sauti kama kafungwa Sea Piano.
 
 
Kweli kabisa. Nilikuwa Bandarini pale nje ya ofisi ghafla sikujua niliko. Miaka hiyo wala hakuna pilika nyingi na siku zote tunazurura kuangalia meli na kwenda kula Babana Split maeneo ya Mkwepu. Nilijihisi niko mji mwingine kabisa nikawa natetemeka. St Joseph church naiona sielewi niko wapi. bahati akatokea mtu ananifahamu akaniuliza unakwenda cinema Avalon? ndio akili ikarudi .
 
🤣🤣🤣🤣 utaachaje kucheka sasa..
Sema ukipotea ukimuuliza konda au Teja, tarajia kila mtu ajue, maana atataka aoshee kwako, ataongea kwa sauti kama kafungwa Sea Piano.
Kilichotuchekesha zaidi walikuwa wajanja na watundu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…