Baada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,
Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,
Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,
Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,
Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,
Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]
Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.
Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,
Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.
Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.