mimi nina babu yangu na uzuri anajulikana sana sana viunga vya mwahako,mwakidila,bagamoyo na mchukuuni hata mwarongo alikotokea mama kimbo wanamjua sana sana ni maarufu
Kisa chenyewe, nina ndugu zagu arusha walikua wana jirani yao anaumwa maradhi ya kuchanganyikiwa, yan vikipanda ni wa kufunga kamba,bas sjui ilikuaje mana ilitokea tu nilimpigia kaka angummoja akanambia sista niko tanga ila niko ndani ndani maramba huku nikimaliza nitakucheki nije nyumbani tukaongea kidogo tukaagana hapo hakunambia kilichomleta tanga bila taarifa ni nini
bas sku ya pili yake akanipigia akaniambia wamemleta mtoto wa jiran yao kwa mganga lakini wapo muda karibu wiki ila hawaoni nafuu yoyote zaidi ya kupoteza pesa hapo wazo la huyo babu yangu halikunijia nikamueleza mama yangu juu ya mkasa wao mama ndio kunikumbusha akanambia kwa nini usiwapeleke kwa babu yako wakajaribu mimi sasa nikamwambia mama mh wasipofanikiwa si yatakua yale yale lakini moyo ukanisukuma wasaidie kuwapeleka
nikampigia kaka nikamwambia kam vipi waje mjini tufunge safar kwa huyo babu kweli walikuja tukaenda tukiwa mimi, kaka zangu wawili,mgonjwa na mama yake,lakini kabla hatujatoka nikampigia babu nikamuuliza kama yupo kuna watu wana shida akanambia nipo njoo tukaenda
tulimkuta nje akatukaribisha ndani tukaingia kilingeni kwake, nikawatambulisha then wakaanza kujieleza shida yao bas babu alichukua tu karatas nakalam akawa anamuangalia yule kijana anaandika akanikabidhi list akanambia hizi ni dawa nazitaka lakini utakayokosa nipigie nendeni maduka ya dawa za asili tena akanambia ziko ghali lakini kazitafteni hizo dawa , tukarudi nyumbani mimi na kaka zangu hao had ngamiani sokoni kuna duka maarufu kwa dawa za asili katika ile list kulikua na mbegu za bangi na dawa kama mbili ambazo wao hawana muuzaji akanambia hizi hatuna, palepale nikampigia babu kumpa mrejesho akanambia nunueni zilizopo hizo nyingine ntazitafuta tukanunua tusirudi nyumbani straight had kwake tukaziacha akasema njoni kesho mje chukua dawa zenu
hio siku jioni yake vikapanda ambapp kesho ndio tukachukue dawa kaka wa watu katoka barabarani ikapita carry akaipanda kwa nyuma, ifahamike huyu kaka ni mgeni, hajawah kufika tanga yeye wala mama yake, hajui anaenda wapi lakini kulikua na watu walimuona wakatupigia kelele yule mgeni wenu amepanda gar inaelekea barabara ya pangani ikabidi kaka zangu wachukue boda kuiwah wakaikuta njiani wakaipigia honi wakasimam wakamchukua mgonjwa wao wakamleta ikabidi afubgiwe chumbani, ni alikua anaongea usiku kucha ukilala ukiamka unamsikia anaongea anaitaja majina yake matatu kwa kurudia rudia kulipokucha baada ya chai tukabebana had kwa babu akapwa za kupaka,za kujifusha za kuoga za kunywa
alitumia mchana na jioni hio siku alilala vibaya mno na kule kwa babu mimi ndio nikawa nauliza tatizo nn babu akajibu huyu ana mtoto wa kijini kichwani sasa alivuta bangi na huyo jini hapatan nazo ndio anamletea hizo shida hakutaka hata mia moja alichojibu akasema akimaliza hizo dawa babu apewe taarifa kuna watu hawana ustaarabu tangu waondoke kurudi arusha had leo kimyaaaaa