Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Way back 2020 nilikua napitia msoto sijawahi ona katika maisha yangu hata kula ilikua tabu.

Kuna jamaa alinitapeli 200000 kwa makubaliano ya kuniingiza yapi merkezi sgr nikapige kazi .

Sina ishu yeyote mjini.

Mwenye nyumba alikua ananidai mpka mtaa mzima ulikua unajua afu alivyokua mshenzi alikua ananipigia simu kupita majirani unaona unaletewa tu simu ongea .

Ex wangu alikua ananitishia kuniroga kisa nimemchezea na kumuacha anitoge niwe maskini,nisipate mtoto na mashine isisimame.

Kuna jirani yangu alinishauri nikasafishe nyota na akanielekeza pa kwenda nilikataa mbele yake ila kiukweli nilufata ushauri wake bila yeye kujua.

Nilienda kwa mgaga kwa malengo matatu,ex wangu asiniroge na anisahau,mwenye nyumba asinidai kodi hadi nitakapoipata na mdeni wangu anilipe au anipe kazi.

Kiukweli hakuna nilichofanikiwa zaidi ya kuukimbia mji wa Morogoro

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Acha uzwazwa. Ingekuwa hao waganga hawasaidii chochote wangekuwa wameshafunga shughuli zao maana wangekosa wateja. Ukiona duka linashamiri ujue wateja wapo na wanafurahia huduma za muuzaduka.
Kuna rafiki yangu mwaka flan alikodi jiko la kupika supu, chips, na chakula bar uko manzese, sasa mwenyewe aliniambia alifungua hiyo biashara kichwa kichwa'' sasa akawa hapati mauzo biashara ngumu na hapo alipo kodi kuna Guest na ikifika usiku ombaomba wote wa mjini wanaenda kulala hapo gest lakini wakitaka kula wanaenda kula sehemu nyingine, jamaa alisema ombaomba wanapesa sana ikifika usiku wana gawana magawio pesa nyingi, Sasa huyo rafiki yangu ikabidi aende kwa mganga na mganga akamwambia apeleke kichwa cha mbuzi ili atengenezewe dawa baada ya kutengenezewa dawa ikabidi aende akakifukie saa saba usiku mbele ya biashara yake'' ugumu unakuja sehemu yenyewe watu wanashelewa kulala na tena wale ombaomba ndiyo wanakaa mpaka saa nane na yeye kaambiwa akafukie saa saba na isizidi muda huo, ikabidi jamaa afosi Kibishi achimbe afukie kichwa cha mbuzi, kuanzia hapo akawa anauza sana na wale ombaomba wakitoka kuomba uko mjini wananunua chakula sana. lakini Biashara za kuhusicha uganga siyo nzuri ukijisahau kwenda ku renew madawa biashara inakufa gani ukijifanya urudi kwenye mfumo wa kawaida wa biashara bila mganga biashara inakufa Fasta, yani maisha ya kutegemea waganga ni mateso na unaishi kwa hofu na mashaka ata ukikuta panya kafa tu kikawaida au ukute ata kitu kigeni maeneo ya biashara lazima utakumbilka kwa mganga. Kuna Mama mmoja mme wake hakuonekana nyumba wiki moja huyo mama ikabidi aende kwa mganga badala ya kwenda polisi au Hospitali.
 
Nakubali kabisa maelezo yako. Ukishakuwa wa kwenda kwa waganga, kila tukio utalihusisha na ushirikina hata la kawaida. Mwisho wa yote utaharibikiwa. Lakini ni ukweli pia kuna waganga wa kweli ambao husaidia sana hata kwa tiba ya magonjwa na matapeli pia wapo. Kazi ngumu ni namna ya kuwatofautisha.
 

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nisaidie kuniunganisha nipate ajira nateseka sana mwaka wa tatu huu sina kazi nna family na majukumu
 
Tunaojitokeza mara nilisaidiwa, mara niliacha na kurudi kwa Mungu, ni mbwembwe tu, waliokaa kimya ndio wenyewe na Siri zao.
Eti utasikia mtu nilienda kwa mganga ila saivi nimeokoka, wakati unaendelea kufanya upumbavu na matakataka yako ya ujuaji kwa kujifanya wao ndio wao eti watoto wa mjini. Hawa watu wa namna hii ni wapumbavu tu halafu wanakipawa cha kutunga stori ili akulengeshe uingie PM ujae akupige, mimi nasema hawa wote wanaofanya hivi ni makubwa jinga tu na wataendelea kubaki makubwa jinga tu kama imekuuma fanya chochote unachotaka mfyuu Mshana Jr
 
[emoji1787]
 

Dah! Vip lakini huko uliko maisha?
 
Madam naomba ni pm mawasiliano yake maana kuja mambo nahitaji kuyatatua ni magumu sana kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…