Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Kufunga madeni nilisidiwa huko kigoma lakini watu wa nmb ilibidi nihangaike na kuweka zuio bank hailogwi
Inalogwa ila system ya kibenki iliasisiwa na Illuminati wa kiyahudi na ndio wanamiliki pamoja na zile familia nyingine za uingereza asilimia zaidi ya 90 ya uchumi wa Dunia nzima.

Hiyo familia iliyoanzisha Banking system inaitwa Rothschild. Tukirud kwenye suala lako la Bank hailogwi ni sawa na mchezaji wa timu ya Mkoa wowote Tanzania. Ambayo haijafuzu hata ligi kuu Ya Bara kutaka kucheza na Real madrid, ama Arsenal.

Dunia ina siri nzito sana sana sana.
 
Miaka hiyo ndio bodaboda zinaingia ingia kuna mwanangu wa haswa haswa,alipewa moja awe analeta hesabu.Shida ya mwanangu mtu wa kilaji sana na kamti pombe.Kwa kifupi alipoteza boda ya watu.Mwenyewe hakukubali akadai chombo yake haipotei kifala so sijui digala alienda kwa mtaaalamu.Mwana akawa analalamika anahisi ametwishwa boda mabegani hawezi kuamka wala kutembea ilikua ni kamzozo.Kila nikikumbuka haingii akilini nahisi kama kulikua mipango mingi hapo kati ambayo hatukuijua.
Hee!. Ilibidi mfanye moango wa malipo mkachangishana poleni.. Wengine wako serious na vyao.
 
Ukinipa pesa chafu ya chuma ulete au ya kuharibu ridhiki yangu najua. Mikono inaanza kuuma, mikono inakuwa ya moto ghafla, kichwa kitauma, macho kuwa mazito , mikono kuwa na kigugumizi pia.

Ukija kuniwangia Lazima nikuone ndotoni na nishtuke kutoka usingizi

Nikikikanyaga uchawi Lazima miguu iwe mizito ghafla .
Duu mie hizi Ni story ama Kuna ukweli
 
Nilienda kwa mganga ni sheikh yupo migo migo kusema ukweli hakunisaidia kupata ajira ndio kwanza mambo yalizidi kuwa meusi.

Ila dawa zake ukichoma na ukioga wanawake unafanya kuwakimbia simu zinaita kutwa nzima na mtaani mpaka unatongozwa. Demu alikupiga kibuti miaka imepita unaona annanzisha convo inbox

Sema ilinikuta sina nguvu nikawa nawapotezea ingekuwa enzi zangu nna mkwanja sijui ingekuwaje.
Mikumi mkono wa kushoto ana tumbo kubwa yule muhuni tu
 
Nilikuwa nasafirisha mkaa mpaka dar bila vibali!

Nikikaa mbele ya gari trafiki na watu wa maliasili hawaioni gari mpaka Dar.

Kwa nin niliacha....with time mganga aliniambia kwa sasa nadaiwa sadaka ya damu ya mbuzi watatu, nikatoa
Baadae akaniambia nipate mimba niitoe nimpelekee.

NIKACHAPA LAPA ILA NILIZULUMIWA HELA, VIWANJA, GARI nikabaki kama mwanafunzi wa secondary

Namshukuru MUNGU nimeanza upya bila ndumba
Nyongeza: Kwa huyo mganga nilikutana na vigogo kadhaa wa mashirika na idara za serikali na NGO ...wakuu wa vyombo vya usalama.

UNAJUA KWA NIN WATU WANANUNUA VX?

UKIONA mtu ana Vx posta anatoka kazini saa 9:30 anakimbia kwa mganga , anajigangua asubuhi saa tisa ,kumi anaanza Safari kurudi kazini.

Nilishangaa kuona VX kibao zikiingia usiku nikawauliza hawa wote ni watoto wa hiki kijiji, mmebarikiwa...jibu hawa ni mabosi na vigogo wa posta.
Hukumuliza kwanini yeye hana hata VX moja?
 
Back
Top Bottom