Ilikuwa Ujiji. Nimepigika kinyama mimi na mwanangu Q. Ghafla mbele yangu naona bango la Uganga, kwa maelekezo hakukuwa mbali na pale. Tunafika tunapisha na wateja ( kama sikosei ni mtu na wakeze ).
Yule Mganga alikuwa ni mwanamke! Basi baada ya salam akaanza makeke yake, shida zetu akazipatia Mule mule toka mwanzo wa Safari yetu mpaka ile siku tunafika kwake! Shida ikawa moja tu! Anataka 40000, sasa nikajiuliza yaani huyu Bazazi ameona yoote lakini kashindwa kujua kama hatuna ata mia? Nikamwambia fresh Mmama we tufanyie kazi sisi tutakupa 60000 sio hiyo 40000, basi ile kainuka tu kuingia ndani kuchukua madubwana yake, mimi nikakusanya pesa 45000 zilikuwa pale kwenye ungo na kinokia Obama nikamwambia Q mwanangu hii nauli tusepe. Tukatokomea hivyo yaani mpaka Mwaloni. Tukauza kale kanokia 15000 jumla tukawa na 60, tukala 7000, tukalipia boti 6000 kwa kila mmoja. Kufika mbele mbele huko kuna kijiji kipo ndani ya Gombe, mida ya saa 1:30 ile Boti inazama, tunatumbukia kwenye lile ziwa, maji naanza kuyaona meusi mwanangu hajui kuogelea anakaba shingoni anaogopa kufa, hali inazidi kuwa tete kila nikijitahid anishike japo ukosi wa shati yule maaluni kakaza kabali......sitosahau. yule mama alitupiga kitu kizoto. Siiendelezi naishia hapa.