Kuomba nini sasa? Siendelezi sababu sio jambo la kufurahisha wala kujivunia, hapo kuna sehemu unaona kabisa sikufanya uungwana. Kwa mara yangu ya kwanza naiba, unadhani nilipenda kumuibia mganga Mkuu? Au ni sehemu ya maisha yangu? Hapana nilifanya upuuzi ule ambao umekuja nikost kwa Miaka, nimesema siendelei sababu najutia nilichokifanya na kinaniumiza mpaka leo hii. Sasa ni hivi kama unahisi ilikuwa ni rahisi kiivyo, baada ya boti kuzama kila tulichokuwa nacho kilibaki ndani ya maji. Na hata kuokoka humo ilikuwa ni miujiza tu. Unajua tulikuwa tukienda wapi? Ni safari iliyochukua zaidi ya miaka 3 kufika tulikotaka kufika. Sipendi kuendelea sababu kuna Mengi, ya kufurahisha, kusikitisha, kuchukiza na kuogopesha pia. Destination ilikuwa Canada imagine.