Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Nilivunjika mguu mbeya mjini nikaenda hospital wakadai inabidi niukate nikatonywa na waja wema niende ILEJE nikaenda nikaungwa mguu kienyeji mpaka leo natembea.

VIPI NIMUITE MGANGA MSHIRIKINA?!

Kwamba ningemuomba huyo Mwenyez Mungu nisingekatwa mguu.
Kupitia yy mwenye enzi alie mkuu kupita vyote alinena na wewe kwa kutumia wale waja waliokwambia nenda ileje hakika ukuu wake umetukuka
 
sijawai kusikia ana mizimu wala majini
Yeye hutuambia ni dawa za asili alifundishwa akiwa mdogo kusaidia kupata mifungo iliopotea , kuikinga mifugo dhidi ya wanyama wakali
na kujua mtu aliekwenda safari ya mbali kama bado yupo hai ama alishakufa

Dawa hizo pia hutumika kuwaita watoto waliokwenda mjini kutafta maisha na kusahau kurudi kijijn kusalmia wazee ,unambiwa ukifanyiwa hizo dawa utatafta kila njia urudi kwenu hata kwa mkopo ama kutembea kwa mguu

Na kuna ingine alinambia ikitokea hataki mtoto wake aende kutafuta maisha mbali na nyumban anachota unyayo wake anamix dawa na kwenda kuufunika na chungu
kuanzia hapo aliefunikwa hawez hata kufikiria kusafiri wala kwenda kuishi mbali na nyumbani.
Duuuuuu
 
mimi nina babu yangu na uzuri anajulikana sana sana viunga vya mwahako,mwakidila,bagamoyo na mchukuuni hata mwarongo alikotokea mama kimbo wanamjua sana sana ni maarufu

Kisa chenyewe, nina ndugu zagu arusha walikua wana jirani yao anaumwa maradhi ya kuchanganyikiwa, yan vikipanda ni wa kufunga kamba,bas sjui ilikuaje mana ilitokea tu nilimpigia kaka angummoja akanambia sista niko tanga ila niko ndani ndani maramba huku nikimaliza nitakucheki nije nyumbani tukaongea kidogo tukaagana hapo hakunambia kilichomleta tanga bila taarifa ni nini

bas sku ya pili yake akanipigia akaniambia wamemleta mtoto wa jiran yao kwa mganga lakini wapo muda karibu wiki ila hawaoni nafuu yoyote zaidi ya kupoteza pesa hapo wazo la huyo babu yangu halikunijia nikamueleza mama yangu juu ya mkasa wao mama ndio kunikumbusha akanambia kwa nini usiwapeleke kwa babu yako wakajaribu mimi sasa nikamwambia mama mh wasipofanikiwa si yatakua yale yale lakini moyo ukanisukuma wasaidie kuwapeleka

nikampigia kaka nikamwambia kam vipi waje mjini tufunge safar kwa huyo babu kweli walikuja tukaenda tukiwa mimi, kaka zangu wawili,mgonjwa na mama yake,lakini kabla hatujatoka nikampigia babu nikamuuliza kama yupo kuna watu wana shida akanambia nipo njoo tukaenda

tulimkuta nje akatukaribisha ndani tukaingia kilingeni kwake, nikawatambulisha then wakaanza kujieleza shida yao bas babu alichukua tu karatas nakalam akawa anamuangalia yule kijana anaandika akanikabidhi list akanambia hizi ni dawa nazitaka lakini utakayokosa nipigie nendeni maduka ya dawa za asili tena akanambia ziko ghali lakini kazitafteni hizo dawa , tukarudi nyumbani mimi na kaka zangu hao had ngamiani sokoni kuna duka maarufu kwa dawa za asili katika ile list kulikua na mbegu za bangi na dawa kama mbili ambazo wao hawana muuzaji akanambia hizi hatuna, palepale nikampigia babu kumpa mrejesho akanambia nunueni zilizopo hizo nyingine ntazitafuta tukanunua tusirudi nyumbani straight had kwake tukaziacha akasema njoni kesho mje chukua dawa zenu

hio siku jioni yake vikapanda ambapp kesho ndio tukachukue dawa kaka wa watu katoka barabarani ikapita carry akaipanda kwa nyuma, ifahamike huyu kaka ni mgeni, hajawah kufika tanga yeye wala mama yake, hajui anaenda wapi lakini kulikua na watu walimuona wakatupigia kelele yule mgeni wenu amepanda gar inaelekea barabara ya pangani ikabidi kaka zangu wachukue boda kuiwah wakaikuta njiani wakaipigia honi wakasimam wakamchukua mgonjwa wao wakamleta ikabidi afubgiwe chumbani, ni alikua anaongea usiku kucha ukilala ukiamka unamsikia anaongea anaitaja majina yake matatu kwa kurudia rudia kulipokucha baada ya chai tukabebana had kwa babu akapwa za kupaka,za kujifusha za kuoga za kunywa

alitumia mchana na jioni hio siku alilala vibaya mno na kule kwa babu mimi ndio nikawa nauliza tatizo nn babu akajibu huyu ana mtoto wa kijini kichwani sasa alivuta bangi na huyo jini hapatan nazo ndio anamletea hizo shida hakutaka hata mia moja alichojibu akasema akimaliza hizo dawa babu apewe taarifa kuna watu hawana ustaarabu tangu waondoke kurudi arusha had leo kimyaaaaa
Pm yako umefunga naomb uni pm
 
....Mlango ukafunguliwa,wana kama 5 hivi walikuwa wanasubiri kufanya test kabla ya kuanza kuzifunga puli.
Mapema asubuhi mzigo ukahamishiwa Kigamboni ndanindani huko.
Kuna mjengo ndichi kimyaa.....
Mzigo ukafungwa,wana na vibegi vyao wakagawana kila mtu na njia yake.
Dah cha ajabu mzigo ukawa hauuziki
Funzo:Mungu yupo na anaepusha
 
Kuna mtu mashuhuri kwlei enzi za magu aliletewa zengwe, mtadhani nawaseti ila ni true story alienda kwa mtaalam mmoja mimi kumuona sikuamini mama nakutana nae wakati nilizoea kumuona kwenye tv[emoji23]

Haikuchukua muda mrefu lile zengwe liliondoka jamani

Nimewashuhudia wakurugenzi na mke wa balozi mmoja akiwa kwa mtaalam kuset mambo yake[emoji23]
Sooo truee

Hahah wapo wengi sana
Mimi nilikutana na halima mdee kipindi cha seke seke lake la covid19 si umeona jambo lake limetulia mjini hapa watu wapo busy kwa sangoma[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ni story kweli ya jamaa yangu wa karibu sana.

Mkewe alianza kuumwa pressure akiwa na ujauzito wa miezi 6.

Wiki nyumbani, wiki hospitali yalikuwa ndiyo maisha yake.

Tulifikia wakati tulishauri daktari atoe mimba mama apone. Daktari alikataa kabisa. BP ilikuwa inapanda hadi 180.

Huwezi amini, alijifungua salama japokuwa mtoto alikuwa njiti.

Cha ajabu, baada ya kujifungua tu, tumbo lilijaa mara mbili ya alipokuwa na mimba. Alivimba miguu kiasi cha kushindwa hata kusimama. Daktari anasema licha ya hali hiyo, hawaoni tatizo lolote katika kupima na hata BP imerudi hadi 110.

Ikawa mshikemshike, hali tete. Si mgonjwa wala watunzaji na daktari mwenyewe tumekata tamaa. Ndipo mmoja wa ndugu akasema nitatenda dhambi mgonjwa apone.

Alikuwa mkristo wa imani ya juu. Wale wa kusali na kulala kanisani. Alikwenda kwa witch doctor. Hakupewa chochote zaidi ya kuambiwa arudi hospitali na kwamba atajua yeye cha kufanya na mgonjwa baada ya saa 3 atasimama.

Alipofika hospitali mgonjwa alishazima. Anasubiriwa tu akate moto.

Baadaye akawa kama ameshtuka fulani, akafungua macho. Akaonekana kurejea uzimani.

Kweli baada ya saa 4 hivi, mgonjwa aliweza kusimama kwa kujitegemea. Akawa mzima tena.

Sote tulimwamini yule witch doctor. Shemeji yetu mzima hadi leo, tena kwa gharama ya sh. 30000/= tu.

Haya mambo yapo kama mtu haamini haizuii mambo kufanyika
Mlokole mwenyewe alienda kutenda dhambi inamaana maombi yalikwama
 
Waganga wazushi tu niliibiwa simu ktk mazingira ya kutatanisha simu kala na gharama sn.

Ss mm sio mtu wa ulozi kama mshana jr, akaja mwanangu mmoja na kuniambia anipeleke kwa mganga hiyo simu aliyeiba atarudisha.

Tumefka kwa sangoma baada ya kuelezea shida zetu mixer akasaga majanimajani si jui ni ya aina gani akasema nichemshe ninywe simu itarudi.

Sasa nipo njiani najiuliza simu aibe mwingine mijani ya dawa ninywe mie, halafu kuna uhusiano gani Kati ya kurudi kwa simu na mm kunywa Yale majani

Aahh kudadeki niliitupilia mbali ile mijani na mpaka ss siamini ulozi na hiyo simu nishasamehe[emoji3061]

Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣 Aisee hatari sii mchezo
 
Hahah wapo wengi sana
Mimi nilikutana na halima mdee kipindi cha seke seke lake la covid19 si umeona jambo lake limetulia mjini hapa watu wapo busy kwa sangoma[emoji28][emoji28][emoji28]
Sasa hizi ndumba kwa nini tusiwaloge wazungu jamani na sie tutawale dunia au wao mganga wao hatari kuliko wetu
 
Kwa kuwa ni shuhuda ntatoa yangu ,Ila staki pm au judgement, haya ni mambo yaliyopita tulifanya ,tusiaemane vibaya.

Kisa Cha kwanza kilitokea 2010 hapo, nlikuwa kijana Sana Ila mganga huyo yupo Ila jina wala namba sitoi. Nlikuwa nauza spare parts za Mercedes ,Faw ,Howo n.k kwa duka la jamaa kutoka turkey hapa dar,nenda keko uulize jina la Mchopa wa spare parts utapewa story ucheke uanguke .
Ss nlikuja kujua kazi nikataka kumpiku boss, mshkaji wangu akanieleza kuhusu mganga fulani Chipu, Sumbawanga mpaka namba nikapewa. Yule mshkaji alipofatlia nkajidai mambo ya mganga staki Ila kimya kimya weekend moja nlisepa kwenda kule mwenyewe .
Ikumbukwe mkoa wa rukwa wala sumbawanga nlikuwa sijawahi kanyaga, nliposhuka stendi nkaulizia kuulingana na maelezeo ya yule braza mpaka kijiji nkakipata , nikiwa almost kufika kwa yule mganga (sitaki kumtaja jina) nlipatana na mbwa alikaa Kama amechizika hvi ,aisee nlitoka mbio akinifukuza ,nliingia ndani ya compound nkihema nikipiga kelele ,kukatokea yule mganga akamfukuza tule mbwa Kisha kunipa karibu .
Kufupisha, Mzee aliniongoza kwa kichaka chake nkapata jiwe limeegemea mti kando Kuna kijumba kidogo na hapo tulipokaa nakumbuka kulikuwa na kisu kina damu Yaani kichafu ,dhahiri kuonyesha kafara watu walikuwa wanafnya pale.
Kimbunga kilianza pale Mzee aliponiuliza ntakacho nkamwambia nataka kumzidi boss niwe tajiri, akaongea mambo yake Kisha lile jiwe likageuka bibi kikongwe ,alinipa kile kisu akaniambia Kama mm ni jasiri na nataka Mali nichukue kisu kile kisha nifuate kinjia fulani kulikuwa hapo ,kile ntapata kife.
Kushika njia Ile nlipatana na kuku nkampita sikushkanisha ,nilipoendelea mbele bila kupata kitu nkakumbuka nliambiwa kile ntapatana nacho ,nilirudi faster Sana.
Mzee yule kuku tulikimbizana ktk ya nyasi ile kumshika nlikata bawa ila akapepea na hio moja mbali sikumpata ,hii tukio ilipita Kama 2 hours hvi nikimkimbiza kuku yule.
Kurudi nlipata kile kibibi kinacheka balaa,nlirudi nimeshika pande LA bawa nlilokata natoka jasho sana ,akaniambia mwanangu una roho ngumu ,nenda mambo yako yatakuwa sawa ,Ila nisiwai kula kitimoto.
Long story short pale keko nilichakata mbususu nyingi Sana Tena Sana ,yule bosi alipanda ndege na familia Yao hawajarudi mpaka leo aisee .
Aliyopo pale kwa ss nijamaa anaitwa shafa ,anauza matunda kando Kuna stationary ya jamaa anaitwa dula wananikumbuka Sana tu .
Nlikuja jisahau nkala sausage one day nkiwa na Dem fulani kisu ,wanawake Yaani wapuzi ,aliponilisha tu moyo ulipasuka nkakumbuka vile nliambiwa , kila kitu kilienda na hewa mpaka zile pisi nlizokuwa zanikimbiza ...Ila nlijenga nyumba moja kubwa Sana mpaka Leo wazazi na dada zangu wanaifaidi , ujana aisee stosahau .
Leo hii nishamaliza masomo nina Mali Ila sijafikia enzi zile .
Walioko keko nenda kwa dula , au Rick Ross bonge fulani anaendesha bajaji pale ,muulize jina Mzee wa mbususu au Mchopa wa spare utapewa bonge LA story kunihusu enzi hizo .
Kwa nliowakosea enzi zile ,nisameheni Bure ni kiburi cha pesa tu na ujana , uchawi upo Ila Kama unajua kuplay smart nao
Eeh kwa hiyo downfall yako ni kutokana na mbususu🤣🤣🤣🤣 aise pole sana
 
Mkuu Mimi bibi yangu mzaa mama alijitibu mwenyewe vidonda vya tumbo Sasa hivi anakula vyakula vyote na Hana vidonda tena yeye sio mganga Hana kibuyu Wala majini ila Kuna aina ya magonywa anaweza kuyatibu Tena Kwa mda mfupi sana Sasa ili kuwahakikishia Hilo nitatoa namba zake Kwa mwenye shida zifuatazo pumu watoto na watu wazima wadada wanaopata mimba zinatoka baada ya muda mfupi vidonda vya tumbo ngiri au mwenye shida ya korodani moja kuvimba vyote nilivyoeleza Nimeshuhudia akiwasaidia watu na wakapona kabisa ndani ya week moja mgonywa wa vidonda ataweza kula maharage week moja pia ishu ya mimba Nina ushahidi usio na shaka kama yupo humu mwenye shida moja wapo nilizotaja Niko tayari kumuungansha nae asipopona aje kunizodoa hapa hapa kwenye huu Uzi yeye anapatikana kilimanjaro ingependeza kama Kuna mtu aliko kilimanjaro nimwelekeze anako ishi Sababu ni maarufu kidogo Kwa ishu hizo note yeye hafanyi Bure anachaji kitu kinaitwa kinda pori sababu yeye ni mkulima anaacha kazi zake anaingia porini kutafuta dawa Hana dawa ya mvuto Hana dawa ya mapenzi Hana dawa ya nuksu hatoi majini Hana limbwata Hana dawa ya utajiri ila yeye ana tibu magonywa Zaid na Hana tamaa
Vipi anatibu sie wazee wakushusha wadhungu ndani ya sekunde 120 walau tusegee moaka sekunde 300
 
Inalogwa ila system ya kibenki iliasisiwa na Illuminati wa kiyahudi na ndio wanamiliki pamoja na zile familia nyingine za uingereza asilimia zaidi ya 90 ya uchumi wa Dunia nzima.

Hiyo familia iliyoanzisha Banking system inaitwa Rothschild. Tukirud kwenye suala lako la Bank hailogwi ni sawa na mchezaji wa timu ya Mkoa wowote Tanzania. Ambayo haijafuzu hata ligi kuu Ya Bara kutaka kucheza na Real madrid, ama Arsenal.

Dunia ina siri nzito sana sana sana.
Eeh kwa hiyo waganga hawawezi i a hela zilizokuwepo vault za nmb crdb wala benki kuu?
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo wakati nasoma A level kuna mkasa ulinipata, kwanza kuna manzi nilikutana nae katika mazingira ya usafiri kipindi hicho naenda school A level akawa rafiki yangu sana ukafikia kipindi akawa ananiambia mazingira ya kwao namna yalivyo, baba yake alikuwa mwananjeshi na mama yake alikuwa mwalimu bahati mbaya wote walifariki katika vipindi tofauti sasa familia yao ikawa inapitia changamoto kidogo ya kiuchumi... Njia pekee wakaona wamuozeshe binti huyu ambaye alikuwa rafiki yangu kwa tajiri mmoja wa madini kule mikoa ya kusini alikuwa anafanya biashara ya madini Msumbiji na kule Kusini mwa Tz baaadae akanishirikishabas friends kwamba hayuko tayari kuolewa na mtu asiempenda wala kuolewa as mke wa pili na mtu mzima hivyo nimsaidie.. mimi nikiwa form 5 mwishoni nikatafuta namna ya kumpeleka kwetu ili akasikilizie wakati anatafuta hatma ya maisha yake, KOSA KUBWA. nikamfanyia shopping nikampanga maza nikampa nauli(pocket money yangu) akasepa. Ikawa kama nimemtorosha aisee toka siku hiyo nikaanza kuumwa Class nashindwa kusoma n.k nikiwa nje au room niko fresh nikienda tu assembly au sehemu yenye mkusanyiki wa watu nadodondoka sasa hali hiyo ikaendelea siku moja niko uwanjani nikadondoka nikapelekwa hospital wakanicheck kila kitu negative, wakanitundika drip ya gluccose sijui nikarudi shule niko poa. siku hiyo nimetoka hospital nikarudishwa shule hapo mwezi wa 2 huo necta mwezi wa 5 kwa hiyo nikawa mtu wa shule hospital hivyo hivyo.. nakumbuka siku hiyo pepa ya pre necta ya kwanza kabisa tulikuwa tunachokua Geogy tulifanga paper DH kwa hiyo tulikuwa wengi CBG, HGL, HGK n.k.. mzee akasema nirudishwe Dar nifanyinwe uchunguzi hospital... Tukaenda Mnazi mmoja Hospital, Muhimbili, Aghakan na jibu likapatikana pale Ccbrt mwisho wa siku wakasema naumwa macho nikapewa na miwani nikasepa shule, nimetoka Home dsm fresh tu ile nafika stand ya mkoani kushuka tu hapo hapo ngoma ikaaanza nikadondoka hospital.. mwisho wa siku hospital wakasema huyu sio wa hapa fanyeni namna, mzee Rc na maza mshahidi wa yehova wakawa hawahamini hayo mambo wakasema nitapoa tu kwa muujiza, nikarudishwa shule, nakumbuka jumapili yake tulikuwa na mahafali ya dini siku hiyo nimeamka fresh nimeoga vaa suti yangu nyeusi nawahi church, nimetoka na wana tumechelewa sana sasa nimefika church wana fasta wakazama kanisani, mimi nilikuwa tycs sasa siku hiyo kwaya ya shule ndio ilikuwa inahudumu ikabidi nikakae pale nyuma yao maana sikufanya mazoezi, ile nakaa tu naona nguvu zinaisha yaani kama mtu ananisukuma nikaanguka .. kuja kushtuka niko hospital aisee nilimwaga machozi hapa maana nikaona sio bure, sasa kuna maza mmoja alikuwa mpishi pale school wa waalimu, yeye pamoja na Headmaster wakaona wanipeleke kwa mtaaamu.. alikuwa ni mbibi wa kiisilamu, nilikaa siku 4 pale siku ya kwaanza nilipigwa dua pale balaa, kesho yake mkuu akaleta mayai, maji fulani hivi sijui yanaitwaje, mkaa, na chumvi akatengeneza dawa, nikapakwa na kunyweshwa atimaye nikawa niko poa.. wakanipa jaribio next ilikuwa ni mahafali ya shule nikafanya fresh tu nikawa poa, assemly nikienda niko poa na paper nikapiga..

Sasa bwana kumbe yale maujinga yote familia ya yule binti ndio walinifanyia kisa nimemtorosha binti yao( mdogo wao) wamekosa hela ndio maana nao wakaona wanikomeshe, baadae yakaisha na paper ya necta nikapiga ilibaki kidogo nifeli ila mambo yakaenda poa Ustadhati alinisave...

Story ndefu duh
Aisee mbususu noma so mateso yote hayo mbususu🤣🤣🤣🤣🤣 mtakufa vijana kisa utelezi.
Sasa bimkubwa jehovas witness hawakuleta mwanagalizi wa mzunguko aje kukuombea au mzee wa kutaniko?
 
Kuna vitu vikubwa viwili vinafuana. Usasa na ukale.. maisha ya sasa yako mjini miji ilikojengeka. Vijana wanaopenda sana kwenda kuyaishi haya. Wanatoka makwao huko nchimbilimbi kwenda mjini kuyatafta. Ukale nao unataka watu wake.. Babu zetu wanaona kale yenye thaman mnoo. Wazaz hawataki watoto waende mjini. Uchawi pia nia sayansi kale ndio mana umefungamana sana na kupinga maendeleo ya kisasa (husda).
Kuna movie Moja hiv ya Amerindian inazungmzia hili. Mzaz hataki mwanae aende mjini ili ameithishe uchawi dogo anaondoka Kwa kutoroka kutafta maisha. Anafanikiwa na kuwa mtu mmoja mkubwa sana kwenye kampeni ya Sheria huko. Siku anayaorudi kutembelea kwao anaanza kukumbana na uchawi unaomsubiri arudi.
Inaitwaje hii movie? Sir Midabwada
 
Back
Top Bottom