Mkuu kwa hapa naomba nipingane na wewe kwa uzoefu wangu binafsi.
Mimi nimeshakutana na mademu kama wawili wenye mapenzi ya kupitiliza. Wa kwanza alikua ni mtoto wa kiarabu kachanganya na mbondei wa Tanga. Yule mtoto alikua ni mzuri balaa! Hiyo rangi tu kwanza, halafu alibarikiwa shepu ya maana, nywele mpaka mgongoni. Yeye mwenyewe ilikuaga tukigombana ananiambia "hivi we unajua mi matajiri wanaonisumbua hapa mjini ni wangapi..?" Na mimi namjibu kwa kiburi "we wanawake wanaonisumbua mimi je, ukiwajua si utazimia wewe!" ππ. Yule demu pamoja na usumbufu wake ila nilivumilia nae zaidi ya mwaka kwa jinsi alivyokua pisi, ila mwisho uzalendo ukanishinda nikabwaga manyanga.
Wa pili huyo demu alikua anafanana sana na Wema Sepetu yule wa miaka ya 2000 kuanzia sura, shepu hadi mwanya ni kama Wema kabisa kasoro sauti tu ndio ya kichaga. Huyu nae alikua na mapenzi mpaka basi. Usumbufu hadi kero. Kikubwa zaidi kilichonifanya nikamuacha ni baada ya kuanza kufakamia ma bia na manyama choma akaanza kufutuka likitambi aah nikaona hapa hapa.. japo hadi leo huwa tunawasiliana ila kuna jamaa kamuoa.