Umewahi kuchapwa/kupigwa na mzazi/mlezi?

Mzee wako hakutaka mchezo na shemeji yake[emoji15] [emoji15]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole mkuu..same story tofauti yetu ni kidogo sana... Mie imenifanya nashindwa kujiamini, najitibu taratiibu..
Pole Sana. Tell us about it tunaweza kukusaidia.
Mamaangu alikua anajua kupiga si kitoto ila nashukuru hakua na lugha abusive.
Leo mm na my young sister ndio tunaomuhudumia katika maradhi yake.
Tusingeweza Kama asingetuadhibu mwanzoni, kwani tungeharibikiwa.
 
Kweli kabisa mkuu. Kuna Mzee jirani yetu alikuwa analaani watoto Wa miaka 10. Eti umelaaniwa wewe na kizazi chako.[emoji15] [emoji15] yaani ajabu,maneno yote mabaya anawaambia wanae Wa kuwazaa kabisa
Mbaya sana maneno huumba
 
Mzazi fanya yote lakini sio kutumia lugha mbaya kwa watoto!!! Ulimi unaumba na unawaharibu kisaikolojia
 
Dah asee umenikumbusha mbali sana,
Nakumbuka nkiwa chalii nliwahi kuiba mashine ya Mzee yakunyolea ndevu nkijua ndani haina wembe ...
Nikaipitisha kwenye nyusi za upande mmoja nkawa Bonge LA kituko bmkubwa aliponiona akahis namuiga kipind ana tengeneza nyusi zke ' aseeh kipigo nlichokipata kila nkikumbuka roho inauma sana aseeh, nahis alinionea mm nlifanya nkiwa na akili za kibashite bmkubwa amenipa adhabu akijua ni makonda daaah.
 
Mkuu she died from cancer, ila alilala chini miezi miwili lakini mwaka mzima aliugua sana.

Yani nyumba ilikuwa ni full of stress, yani tangu wadogo maisha yaliandamwa na vipigo vikali vikali, imagine nikiwa drs la pili tayari nilikuwa namuogopa mama, mbaya zaidi Tabia ya kunyimwa chakula ikapelekea udokozi Wa hela sasa ohoooo! Fimbo jamani tena ukiwa uchi. Wakati mwingine upupu anauweka kwenye Gunia alafu unavua nguo unaambiwa uingie humo, alikuwa ana pesa ila haya hazionekani( nahis hata mungu alichukia) hakuwahi kukaa na sisi km binti zake au rafiki zake,... Tukiwa tunatoka shuleni jioni nilimuangalia my lovely twin nikawa naona jinsi sura yake inavyojaa hofu wakt wenzetu wanashangilia kwa kelele "kwaheri mwalimuuuuu"... Simanzi asubuhi hakuna chai, shuleni mchana hakuna msosi, na ukikaa vibaya Nyumbani pia mnaweza kuacha kupika..
Alikuwa MTU Wa kutafuta kasoro muda wote MTU Wa kubeza, majirani walipenda kutupa msaada Wa chakula ila waliogopa ukali wake. Heeeeee!!!!!! Nilikuwa nikijiona Mie siyo MTU kabisa, nikawa naogopa hadi watoto wadogo.. Kuna Sikh moja alitufungia nje hadi asubuhi tukajibanabana kwenye magofu na baridi na mbu[emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
Alianza kupunguza ukali na kupiga tulipoenda kidato cha 5 Mie nilienda musoma nikakaa hukohiko hadi nikamaliza, twin akichaguliwa arusha... From there tulijitambua kuwa na die ni mabinti wazuri, tukaanza kuheshimiana na kupendana zaidi,
Tulifaulu chuo kikuu, mwaka Wa kwanza mama aligundulika kuwa ana maradhi ya cancer, nilimuuguza kwa UPENDO MKUBWA SANA, KWA GHARAMA KUBWA KWA KUJITOA BILA KINYONGO!! 2014, Aliaga dunia. Mungu amrehemu na ampumzishe kwa amani.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] watu wengine bwana.
 
Mama ameanza kunichapa nkiwa mdogo sana nakumbuka nlikuwa sijaanza hata shule nlienda kwa watu nkawa nimesimama mlangoni wao wanakula mi naangaliaa....Mhehe yule alinibebaa akanipeleka nyumbani akanivua nguo zotee akanifunga mezani miguu na mikono kile kipigo nlichopokeaaa....mpaka leo huwa siwezi kwenda kwa watu na huu utu uzima
 
Mmmh I see
 
Mungu amponye mama na aendelee kuwaimarisha .
 
Pole dear, Mungu awatie nguvu mdumishe Upendo Apumzike kwa Amani mama .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…