Umewahi kukuta watu wanakula chakula gani ukakishangaa?

Kuna majani mengine yanajiotea tu, ni jamii ya mlenda wanayaita mlenda mgunda, nimewahi kula kipindi nipo Morogoro. Huo mlenda ukimix na maharage ndo balaa, utatafuna mpaka vidole
 
Mi nikishangaa kuona watu wanakula yale majani ya magimbi.
Majani flani hivi mapana hivi, nikishangaa kumkuta jirani anayaandaa kwa kupikwa.

Kumuuliza anasema yanaliwa ila sio yale yaliyokomaa sana.
 
Mchunga unaliwa maeneo mengi tu vijijini huko. Kuna majani fulani yanaitwa mwidu niliona watu wa kijiji cha msolwa morogoro wanaomba kuingia hifadhini seluu ili kuyachuma kwa ajili ya mboga wakati kijijini kwetu ni chakula cha mbuzi na ngombe
 
Hakuna chakula nimewahi shangaa maana kwa kutembea nilikotembea mi huwa kikiwa na chumvi na Mimi nikiwa na njaa ni twende TU.
Sema Kuna wale konokono nadhani nikienda Chicago nitawala huwa napenda maandalizi yake hasa wakiandaa wa Irish
 
Mchunga unaliwa maeneo mengi tu vijijini huko. Kuna majani fulani yanaitwa mwidu niliona watu wa kijiji cha msolwa morogoro wanaomba kuingia hifadhini seluu ili kuyachuma kwa ajili ya mboga wakati kijijini kwetu ni chakula cha mbuzi na ngombe
Mie niliona Lushoto wanakula majani ambayo huwa tunalisha sungura (wao wanaitwa mbwembwe ama kavovo)
 
Zambia wanakula yale mawashawasha yenye manyoya yanayowasha Yana rangi rangi halafu yanatisha na tukuyu wanakula panya buku.
 
Wamakonde wanakula Chavichavi na wale konokono wa baharini ,pia ming'ong'o(ipo kama mizizi naionaga sana mbagala wanauza kwenye sahani kina mama) huwa wanaokula hivyo vitu siwaelewi.
 
Matembele enzi hizo sikuyafahamu wala sikujua kuyatofautisha na marando nilipokuta yamepikwa sehemu nikashangaa kuwa wanakula marando(majani ya ambayo mizizi yake inatoa viazi vitamu)
Marando Numbisa hii Rwamishenye kwa wasomi those days .
 
Wamakonde wanakula Chavichavi na wale konokono wa baharini ,pia ming'ong'o(ipo kama mizizi naionaga sana mbagala wanauza kwenye sahani kina mama) huwa wanaokula hivyo vitu siwaelewi.
mkuu hiyo mizizi inaitwa ming'oko, mdogo wangu wakike alileta nyumbani ikiwa mibichi wakichemsha nikaonjaa, dooh! ile mivitu haina ladha kabisa.

wanasema inaongeza hisia za mapenzi kwa mwanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…