binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 11,201
- 28,642
Yaani mi nilikua sijawahi kuona, ila nilivyojaribu yako fresh kabisa.Ndo maana yakee, mbna tunakula sanaa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani mi nilikua sijawahi kuona, ila nilivyojaribu yako fresh kabisa.Ndo maana yakee, mbna tunakula sanaa.
Nguniani ya kipome tamu sana na ugali au wali, na parachichi pembeni a.k.a katapelaMbeya inaotwa nguniyani (ngunyani), unapata imepikwa na karanga za kusaga...hatariiii
Ila viazi vitamu unakula mkuu!?Michembe
Na mi kwa mara ya kwanza niliyaona mbeya yanapikwa kama mboga nikala nlikua ugenini nliona yako poa. Na kukaa SGD mboga iliyonishinda ni moja tu mlenda.Majani ya maharage iringa huko, nilishangaa ila nilivyo onja nikaona mbona fresh tu. Kwetu singida majani ya maharage hayaliwi.
Japo mimi wa singida ila mlenda hapana aisee! Japo kuna watu wanaupenda "kweri kweri", namshukuru Mungu kwangu baba nanii nae hauelewi kwahiyo haupikwi kabisa. 😅Na mi kwa mara ya kwanza niliyaona mbeya yanapikwa kama mboga nikala nlikua ugenini nliona yako poa. Na kukaa SGD mboga iliyonishinda ni moja tu mlenda.
Kweli hatuli aiseeMajani ya maharage iringa huko, nilishangaa ila nilivyo onja nikaona mbona fresh tu. Kwetu singida majani ya maharage hayaliwi.
Yanaliwa vizuri tyuuh.Yaani mi nilikua sijawahi kuona, ila nilivyojaribu yako fresh kabisa.
Mimi mchunga ulinishinda.Kuna sista duu wa masaki alikuja home akashangaa nakula ugali maharage akauliza hapa kuna shule ya boarding?
Iringa kuna mboga inaitwa mkalifya,na uroho wangu wote nilichemsha, ni chungu kuliko uchungu wenyewe
Morogoro pia yapoKuna madude nilipata kuyaona Zanzibar, wanayaita mashelisheli aisee yale hata kama nina njaa kali kiasi gani huwezi kunilisha.
Uyole kuanzia miaka ya 2005 kushuka chini kabla hapajachangamka wenyeji walikuwa wanakula wale panzi wakubwa wanaita paralila wenyewe, na mapanya makubwa hivi yanapenda kula viazi shambani.Kweli tembea uone
Nilikwenda Bangkok nikawa natembea usiku barabarani ambapo ndio kumekucha kwa mama lishe yaani vyakula ambavyo maisha yangu sijaona watu wanakula ila baadhi tu
Nimeona Meza wakiuza panzi wa kukaanga, mende wale wakubwa wa mabuchani ( sio wa chooni) hawa ni weusi
Pia nimeona mapaja ya vyura, popo wakiwa wamebanikwa mpaka unatamani uonje
Yaani ni mitaa mizima wamejaa na wao wanavyofakamia
Nimeona nyoka wa kila aina wakipikwa mchuzi na wa kukaangwa
Nge ndio usiseme kuna wengine wanachanganya wadudu tofauti tofauti
Unaona kabisa wanavyo enjoy kama sisi kwenye mishikaki
Kwa sasa demand ni nyingi sana wamejiongeza na kutengeneza sehemu za kuwalea na kufuga aina zote za wadudu View attachment 2582049View attachment 2582050View attachment 2582051View attachment 2582052
Majani ya Magimbi kule Tukuyu ni mboga, inaitwa Lyombo.Mi nikishangaa kuona watu wanakula yale majani ya magimbi.
Majani flani hivi mapana hivi, nikishangaa kumkuta jirani anayaandaa kwa kupikwa.
Kumuuliza anasema yanaliwa ila sio yale yaliyokomaa sana.