Mnaenda Mbali sana yanii,mimi hadi na leo hii sijawahi kuwaelewa watu wanaokula MLENDA aina yoyote ya MLENDA hata ungekua unakatiwa katiwa ndani noti za ten ten,nisingewahi thubutu kula.
Hadi na Leo hii sijawahi waelewa Walevi wanaotumia vinywaji vikali (ngumu kumeza) sijawahi waelewa na sitoacha washangaa wanakunywa wanapata ladha gani.
Nimeshawahi onja sana vinywaji vyao ila hamna ladha naiona zaidi ya mateso kwenye kumeza mpka harufu.
Nyie mnaokunywa vilevi vitamu vitamu sina mashaka nanyi, Tuko pamoja eneo hilo.
Ila Mshangao wangu ni zaidi kwa wale wanaokunywa tena za bei ndefuuu achana na vi common vya mtaani kwa mangi, Naongelea maboss wa ma grants na madude hatari hatari. Mnanisurprise kila iitwayo leo.