Niliwahi kwenda Tabora Ziba papo Igunga ila ni jirani na Nzega nilishangaa wana chakula flani hivi viazi vigumu vimekauka wenyewe wanavitafuna nilishangaa sana sijawahi ona aisee ila nilishangaa
Pia kipindi niko Ngaramtoni Arusha nishawahi ona Mmasai anakula nyama flani hivi ya kwenye nundu bila kupikwa nilishangaa sana
Kipindi nakua nishawahi enda Mbinga vijijini huko somewhere LIpilipili jirani na Mpepai Ruvuma kuna sehemu wanakula Nyani anakaangwa fresh tu anapigwa kama mbuzi tu afu unyama
Mtwara huko Nachingwea wanachoma panya wa porini na anapigwa joto kali safi kabisa ana
Dar maeneo ya mbagala nilishangaa kuona miguu ya kuku mautumbo na kichwa yanauzwa na wateja kama wote (sikua najua)
Nilikulia Uganda na kusoma huko so nilivyomaliza Primary school nilikujaTanzania nyumbani. Sasa nikiwa dining nasubiri msosi cuz kulikuepo na hotpot moja na si kawaida,
Mara nashanga bro anapakua na kula.Then nikamuuliza mbona unakula tu mboga akasema this food is called makande. Niligoma kula, chakula gani kina mahindi na maharage.Ilibidi nipikiwe kingine.