Umewahi kukuta watu wanakula chakula gani ukakishangaa?

Umewahi kukuta watu wanakula chakula gani ukakishangaa?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Tembea ujionee, kwenye jamii kuna vyakula vya aina tofauti tofauti, kuna vingine vya unaona kabisa ni vya ajabu ila jamii husika inakula na kuvifuhia kabisa.

Nimewahi kwenda kijiji fulani nikakuta wanakula majani fulani ambayo kwetu tunayatumia kama maua ila kwao ni mboga pendwa kabisa.

Pia mara ya kwanza kuja Pwani na kukuta watu wanakula mchunga kama mboga napo nilishangaa sana kwa kuwa kwetu ni majani ya kulisha sungura si chakula cha binadamu.

Vivyo ivyo kuna watu wanakuja kwetu wanashangaa kukuta tunakula baadhi ya vitu kama askari wa mchwa na tunafurahia utamu wake kabisa nk.

Umewahi kuona chakula gani kwenye jamii ya ugegenini ukashangaa kujua kuwa ni chakula?

1679986515430.png

Askari wa mchwa​
 
Back
Top Bottom