Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Vifutu hao. Wapo sana Iringa na alininusuru nikiwa mdogo huko Moro. Nilimkanyaga ni Mungu tu aliniepusha kwani yule kifutu(Viper) ndio nyoka mwenye sumu zaidi duniani.
Mbona wengine wanasema black mamba ndo anasumu kali
 
Vifutu hao. Wapo sana Iringa na alininusuru nikiwa mdogo huko Moro. Nilimkanyaga ni Mungu tu aliniepusha kwani yule kifutu(Viper) ndio nyoka mwenye sumu zaidi duniani.
Kwa Afrika nyoka hatari na mwenye sumu kali kuliko wote ni Koboko tu na kwa Tanzania wanapatikana kwa sana Tabora.
 
Wakati Pinda akiwa PM, Alikuja kwao nami nikaambiwa nipeleke trekta la Kikundi kule kwao Kibaoni alilokuwa akienda kukabidhi kwa Kikundi. nNikiwa kama msaidizi wake Jimbo nikasema siendi na gari binafsi wala la msaidizi wake, niliomba nipande trekta nikiongozana na Dereva mmoja wa Halmashauri ya Mpanda kipindi hiko.

Hahaaaa, tuloanza safari pale Mpanda saa 10 Jiono na tulitoka vizuri Mpanda mjini hadi sitalike. Tukaingia Katavi National Park na safari ikaendelea. Ile kabla ya kufika Daraja la Mto Kavuu kama saa 12:30 Jioni, tukakutana na kundi la Simba kwani siku hiyo mvua ilinyesha na walitoka kwenye majani na kuja barabarani.

Hahaaaaa tupo kwenye trekta jamaa anaendesha mi nimekaa pale kwenye mud guard. Simba wakashangaa lile trekta na wakaanza kutukimbizia. Hahaaaaa, tulilia na kusali sana siku ile maana jamaa walitukimbiza na wakawa wanapanda/rukia/dandia trekta pale nilipokaa mimi kwenye mud guard ila tairi lilikuwa refu wakashindwa kufika. Walitukimbiza kama mita 50 hivi then wakatuacha. Tangu siku ile niliogopa na kuheshimu sana muda wa kutembea kule hifadhini. Yaani huwa napita mchana na sio jioni kuanzia saa 11. Hatari.
 
Mamba mto ruvu korogwe tumetoka kucheza mpira sa moja kasoro hyo nijisogeze ruvu nipige maji ile nimesaula nijirushe mtoni sijui nini kilinifanya nikaahirisha nigeuke nyuma upande wa kulia kwngu namkuta mzee anajisogeza taratiibu anakuja mtoni.
 
Kwa Afrika nyoka hatari na mwenye sumu kali kuliko wote ni Koboko tu na wanapatikana kwa sana Tabora.
Unachanganya bro, kuna nyoka mwenye sumu kali na nyoka mwenye uwezo wa kugonga mara nyingi. Koboko anagonga hata mara 50 bro kwani akigonga, meno yake hayatoki baada ya kugonga ila.kifutu ndio nyoka mwenye sumu zaidi duniani.

Koboko wapo kanda ya ziwa na waliletwa (Imported) na wazungu ili kukabiliana na Panya kwenye Plantations za Karanga. Nilikutana nao sana kwenye majiko(Maburn) ya Tumbaku huko katavi.
 
Mbona wengine wanasema black mamba ndo anasumu kali
Black mamba ana sumu kali ila Google bro uone kati ya Koboko na Kifutu(Viper) yupi ana sumu kali. Koboko ni mkali, ana hasira kali na anang'ata bila kuachia Jino na ana uwezo wa kuua/kung'ata ng'ombe hata 50 kwa wakati mmoja.
 
Whatsapp image, January 30,2024.
actually ni mwaka 2022 nyoka aligongwa na gari then tukapita pembeni yake na boda iliogofya sana
kwa imani yangu ya kirasta siwezi kuua chochote pia kitaaluma mimi ni muhifadhi siwezi kuua mnyama haijalishi ni wa hatari namna gan as longer as yuko kwa makazi yake ya asili
 
Tulikua safarini kwenda Botswana ila ni camp to camp porini.
Selous ndo nikaona mambo.
Puma ushawai kumuona?
NYati, Simba .
 
Hahaaaaa, tumetoka Mpanda Mjini na Fuso tukielekea kununua Mpunga kule Majimoto Mpimbwe. Mi nikowa ndio tajiri ninaeenda kununua Mpunga. Kwenye gari tulikuwa mimi, dereva na tingo. Katikati ya Safari na tukiingia Katavi National Park. Mbugani kule tunaona nyoka Mkubwa mweusi kalala Barabarani. Tingo kasema tumkanyage. Pita kumgonga, tukamkosa alikwepa. Tukaangalia nyuma, jamaa akasema tumkanyage. Dere akarudi nyuma kumgonga. Akamkosa. Dereva akaenda mbele kumgonga akamkosa. Tukageuka nyuma, hatukumuona tukaendelea na safari.

Mbeleni tunakutana na magari, dereva mmoja anaonesha chini ya gari letu kama kuna kitu. Hatukuelewa. Tunakutana na magari mara dereva mwingine anatuonesha. Hahaaa, tukajua jamaa tumelizua na amepanda/jificha chini ya gari kumbe mkia unaninginia na baadhi ya madereva waneuona.

Tukafunga vioo kwani tulihofu anaweza kupanda hadi tulipo atushambulie. Tunaendelea na safari huku tunalaumiana kwani joto linatusumbua. Mbele tumekutana na magari na dereva mwingine akatuonesha ishara kwamba kuna kitu kinaninginia. Hahaaaaaaaa tumeenda kufika pale Kibaoni kuna gets la Ushuru, wale wakusanya ushuru na raia wakala mbio.

Hahaaaaa tukasema leo twafa. Sasa tufanyaje? Tukashauriana tupige simu kituo cha Polisi Majimoto ili tulipeleke gari pale na tufungue milango alafu tule mbio kila mtu na upande wake. Tukaenda, kufika kituoni ile kufungua mlango. Kila mtu na njia yake. Kumbe yule Nyoka Koboko alichoka na akajiachia njiani ukitoka Kibaoni kwenda Majimoto. Toka siku hiyo, sikanyagi nyoka nikimuona ametulia barabarani.
 
Back
Top Bottom