Hahaaaaa, tumetoka Mpanda Mjini na Fuso tukielekea kununua Mpunga kule Majimoto Mpimbwe. Mi nikowa ndio tajiri ninaeenda kununua Mpunga. Kwenye gari tulikuwa mimi, dereva na tingo. Katikati ya Safari na tukiingia Katavi National Park. Mbugani kule tunaona nyoka Mkubwa mweusi kalala Barabarani. Tingo kasema tumkanyage. Pita kumgonga, tukamkosa alikwepa. Tukaangalia nyuma, jamaa akasema tumkanyage. Dere akarudi nyuma kumgonga. Akamkosa. Dereva akaenda mbele kumgonga akamkosa. Tukageuka nyuma, hatukumuona tukaendelea na safari.
Mbeleni tunakutana na magari, dereva mmoja anaonesha chini ya gari letu kama kuna kitu. Hatukuelewa. Tunakutana na magari mara dereva mwingine anatuonesha. Hahaaa, tukajua jamaa tumelizua na amepanda/jificha chini ya gari kumbe mkia unaninginia na baadhi ya madereva waneuona.
Tukafunga vioo kwani tulihofu anaweza kupanda hadi tulipo atushambulie. Tunaendelea na safari huku tunalaumiana kwani joto linatusumbua. Mbele tumekutana na magari na dereva mwingine akatuonesha ishara kwamba kuna kitu kinaninginia. Hahaaaaaaaa tumeenda kufika pale Kibaoni kuna gets la Ushuru, wale wakusanya ushuru na raia wakala mbio.
Hahaaaaa tukasema leo twafa. Sasa tufanyaje? Tukashauriana tupige simu kituo cha Polisi Majimoto ili tulipeleke gari pale na tufungue milango alafu tule mbio kila mtu na upande wake. Tukaenda, kufika kituoni ile kufungua mlango. Kila mtu na njia yake. Kumbe yule Nyoka Koboko alichoka na akajiachia njiani ukitoka Kibaoni kwenda Majimoto. Toka siku hiyo, sikanyagi nyoka nikimuona ametulia barabarani.