Umewahi kukutana na tukio la kuagiza kitu mtandao halafu ulicholetewa ni tofauti na ulichoagiza?

Umewahi kukutana na tukio la kuagiza kitu mtandao halafu ulicholetewa ni tofauti na ulichoagiza?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
1780904619233.png
Mimi niliwahi kuagiza nguo Kariakoo ilikuwa suti niliiona mtandaoni. Itoshe kusema nilichokiona nikakiagiza na nilicholetewa ni vitu viwili tofauti. Ile nguo ikabidi niigawe hata sikuivaa na ilikuwa ni ya tukio. Mpaka leo siwezi kuagiza nguo mtandaoni mpaka nikajihakikishie mwenyewe.

Majibu ya swali hili yaambatane na picha kabisa :forsenLaughingAtYou:​
​
 
Enzi hizo kikuu imepamba moto niliagiza sana viatu, urembo na vitu ya mtoto vikawa vinakuja kama picha zilivyo na quality nzuri.

Siku moja nikajiroga nikaagiza feni, ilikuwa nzuri, ina mambo kibao baada ya wiki 2 delivery anakuja na kabox kadogo ameshika mkononi nikamwambia au mmekosea mzigo sijaagiza kitu mbona hapo nategemea box kubwa la feni.

Akaniambia mzigo ni wako una jina lako nikahisi labda kuna kakitu niliagiza nkasahau kufika ndani kafungua mweeh ni kafeni kadogo ka kushika kwenye kiganja na nilinunua zaidi ya 80k.
 
Mpaka leo siwezi kuagiza nguo mtandaoni mpaka nikajihakikishie mwenyewe.
Kuna mother boss lady tajiri aliagiza viatu kwa delivery ilikua hapa hapa bongo dsm viatu alivipenda basi yule dada ambae anauza online akavituma kwa bodaboda Google map location delivery package mzigo ukafika alipie kwa lipa namba asaini mzigo umefika na mengineyo km kutoa feedback kwenye page n so on, sasa mzigo umefika kuukagua akakuta sio kile kitu aliagiza sema yule jamaa wa delivery alikua na roho nzuri sana yaan angekua kijana mwingine ingekua issue kwa hio ikabidi mother amwambie yule jamaa wa delivery akachukue viatu vyote km vile avilete yeye achague nyumbani pale jamaa kweli kaenda kajaza kwenye bag kaja navyo viatu km vyote ili mother aanze kujaribu kimoja kimoja mpaka apate anachokipenda na ikawa hivyo akapata anachokipenda ambacho kinamtosha vizuri akamlipa jamaa jamaa akaenda

End of the story.
 
Niliwahi kuagiza lamp shade. Kwenye picha ambayo nilichagua inaonekana ni standard size lamp shade, iliokuja ilikuwa half the size. Nimegundua wauzaji wa online wanatumia sana camera tricks.
😁 Pole. Endeleeni kutoa ushuhuda ili mimi ambae sijawahi kuagiza nisijaribu. Kifupi mtu mwenye hela za mawazo hatakiwi kuagiza mtandaoni, ni sawa na kubet
 
Back
Top Bottom