Umewahi kukutana na watu wa ajabu kwenye maisha yako? Walikuwa watu wa aina gani?

Umewahi kukutana na watu wa ajabu kwenye maisha yako? Walikuwa watu wa aina gani?

Kulikuwa na mtu huyu, wakati wa kusoma chuo cha ufundi, alikua ni mtu ambaye tulikuwa darasa moja pindi tupo chuo, alikuwa ni mkimya sana na hajawahi kuchangia chochote wala kuzungumza na mtu yeyote darasani.

Alikuwa Hana makundi, alikuwa hana ushirikiano, alikuwa hana marafiki. Hakuna mtu aliyejua sehemu alipokuwa akiishi, hakuna mtu aliyejua chochote kuhusu huyu mtu isipokuwa jina lake. Tukiwa darasani alikuwa hajibu maswali ila mitihani alikuwa anapata alama za juu sana.

Alikuwa kwenye group la whatsapp la chuo na hakuwahi ku-comment chochote na siku tulipomaliza chuo alileft Group, Alikuwa haendi Kanisani/msikitini na wala hakujihushisha na dini yoyote. Tangu ile siku ya mtihani wetu wa mwisho, hakuna mtu aliyemwona au kusikia Alipo.

Alikuwa hazungumzi kamwe labda tuaze sisi kuzungumza naye, na mda mwingine anaweza kukupuuza. Kama kutakuwa na tukio fulani maeneo ya chuo mara nyingi alichangia mchango kuazia Tsh. 40,000 na zaidi, na alipenda kutumia jina la mtu asiyejulikana, hata akichangia hakuwahi kuhudhuria sherehe/tukio hilo.

Wasichana katika darasa letu walimchukia sana , kwa sababu hawakuweza kuwa naye kwa namna yeyote ile.

Wengi wetu tuliamini kuwa yeye ni Afisa Usalama anayefanya kazi katika serikali ya Tanzania ambaye lengo lake labda lilikuwa ni kufuatilia usimamizi wa chuo. Alijifanya kama mcha Mungu na aliheshimiwa na kila mtu.

"Obidux Baljidanz" alikuwa mtu asiyejulikana.

Je, ni watu gani wenye mambo ya ajabu, ambao umekutana nao?

Nliwahi kusoma na jamaa wa aina hii Uganda, darasani haendi hakuna anae jua jina lake tuliishi hostel moja kwa wiki anaonekana mara moja au mbili usiku alikua ana pesa nyingi kidogo mimi nlikua rafiki yake alikua akija ananipa pesa nyingi kuna kipindi nli ibiwa simu nikashangaa akaniletea simu mpya baada ya masomo alikuja kunitafta kwenye social media akaniambia yupo US anifanyie mchongo niende kwa kweli nlikataa sababu hakua mtu wa kufunguka
 
Duh aiseee
Karibu sana mkuu
Nliwahi kusoma na jamaa wa aina hii Uganda, darasani haendi hakuna anae jua jina lake tuliishi hostel moja kwa wiki anaonekana mara moja au mbili usiku alikua ana pesa nyingi kidogo mimi nlikua rafiki yake alikua akija ananipa pesa nyingi kuna kipindi nli ibiwa simu nikashangaa akaniletea simu mpya baada ya masomo alikuja kunitafta kwenye social media akaniambia yupo US anifanyie mchongo niende kwa kweli nlikataa sababu hakua mtu wa kufunguka
😄😄, Ulikataa mchongo mkuu, Sasa hivi ungekuwa bilionea.
 
Pale SUA 2008 kulikuwa na jamaa mmoja toka Tabora tulimuita Kenge tokana na macho yake.

Jamaa alikuwa anachagua Course zote elective hii ilimsaidia kwani alikuwa ana SUP hadi 7 kwa mwaka mmoja. Jamaa alikiwa ni slow learner.

Wakati wa probation tulikuwa tunaenda wiki 1 au 2 kabla ya kuanza SUP, yeye tunamuona anatusalimia akiwa kwenye treni pale Relini Dark City anakuja jioni na kesho ni Sup. Kesho asubuhi utamuona pale freedom square anakuja kupiga Pepa ila hajui na anauliza leo ni mtihani gani? Kuna siku hadi tumeanza paper jamaa hajafika ile tunamaliza tunaona kumbe naye alikuwepo akipiga Sup zake.

Jamaa hakugraduate nasi tokana na vimeo na aligraduate mwaka unaofuata mbele yetu, sasa yupo pale Tabora Manispaa.
 
Hapana mtu hakupi ABC anakwambia just come and get rich huko ni kujitoa mhanga, nlimwambia nna mkataba na kampuni anipe muda nita join nae baadae
😀😀, Kweli mkuu, hapo ilikuwa ni ngumu sana mkuu,
 
Hata nchi yetu inachangia kuua vipaji, Mtu wa design hiyo, ilitakiwa mapema sana, aandaliwe fani inayomfaa, Hata Forecasting.
Forecasting?😂

Mkuu ulishawahi kutana na wale watu anajitamba na huwezi mzidi, namfananisha na mayweather anakutambia na anAkuponda.

Huyu ni sababu anajua darasani nani anakuwaga wa kwanza mpaka wa10. Ila watu wengi walikuwa wanamchukia, na yeye anakuambia huwezi badilisha chochote nitakuongoza tu.

Alikuwa na akili sana, hujawahi somaga na wale watu mwalimu anampa nafasi afundishe wenzake?
 
Back
Top Bottom