Hii niseme ni karma,
Kuna manzi alikua mrembo sana, typical chuga girl. Mara nyingi akiongea utasikia maneno kama "huyu chalii anazingua" au "fata mambo yako eroo" na swaga zingine zinazofanana na hizo.
Mzuri kweli kweli ila sasa ukiwa unaongea naye kuna mzuka fulani unapotea kwenye maongezi maana usela wake umezidi mpaka unahisi kama anajifanyisha!
Basi bhana,
Huyu binti tulikua naye course moja wakati ule. Kutokana na nature ya course yetu wanaume walikuwa wengi sana kuzidi wanawake. Na hata hao wanawake wachache waliopo wengi walikua wagumu kasoro yeye tu ndio alikua mng'ao.
Macho yakawa mengi sana kwake, hadi washikaji zangu wa karibu wakawa wanapambania kombe. Kati yao kuna mmoja alimuelewa sana, ile kumuelewa manzi kiasi cha kuwaza kumuoa kabisa kama akikubali. Na huyo mshikaji alikua room'ate wangu kwaiyo mara nyingi alikua ananiambia anachomuwazia bibie. Na alikua free kwa sababu mimi sikuwahi kuonesha interests yoyote kwa yule binti. So hakuniona kama competitor!
Sasa kwa sababu wapambanaji ni wengi, yule manzi akaanza kuwa na kiburi; ile kuwa na "ego" au "arrogant" kama mnavyosema wasomi! Kwaiyo akawa kama amechoka ku play a "good girl" character kwenye movie ya wahuni maana wakiambiwa vizuri hawaelewi wao ni kukomaa tu. Ikafika hatua ukisogeza pua anakukatia kipande cha maneno mabovu utayachambua mwenyewe mbele ya safari (niligundua hili wakati tunapiga story za hapa na pale na masela huku tukichekana siku zinasonga).
Nilikuja kupangiwa naye group moja la majadiliano baada ya vipindi. Sasa kwa sababu najua hali ilivyo kuhusu yule binti, basi muda wote ambao tulikua karibu, mimi nikawa nakaa kwenye mada husika tu, siendi nje wala sisogei pembeni. Akaamua kunikatia jina fulani tuseme "A Serious Guy". Akahitaji niwe na contacts zake kwa ajili ya updates za muhimu, nikawa nazo!
Shetani ndiye aliyeleta akili za kutengeneza simu ili aondoke hadi na wale wenye aibu ya kutenda dhambi hadharani; kila siku nawambia muwe nazo makini hamsikii, shauri yenu!
Mada za mwanzo zilikua on point lakini mdogo mdogo zikaanza kupinda. Mara movie fulani, mara nyimbo fulani, mara nilikuona maeneo yale ulikua unafanya nini. Nikaanza hadi kujua akiumwa, akimeza dawa, na akipona. Sasa wakati haya yanaendelea jamaa yangu yeye hajui. Ila yeye daily anani update amemnunulia sijui zawadi gani ya birthday, ili amuombe watoke out na mambo mengine kibao, mimi kazi yangu kuitikia tu na kumtia moyo.
Sasa mambo ya kwenye simu yalivyozidi kuwa mengi, na mimi nikaanza kumuwazia anayowaziwa na wengine. Au sio bhana? Kwani kuna ubaya gani na mimi mporipori nikilamba asali? Hapo ameshaanza kunitumia na vi picha vyake vizuri vizuri. Moyo huu usukume damu tu. Nikaanza kukolea na yeye akanizamisha mazima!
Route za kumtembelea kimya kimya mida ya usiku zikaanza. Najificha ficha nisije nikaonekana. Sijui warembo wanakua"ga na shida gani na typical shamba boys, they always got s'thing for them! Kumtembelea kukanoga, nikawa sipati usingizi mzuri nisipomuona usiku hata kama nimeshaonana naye mchana.
U busy ulivyozidi jamaa yangu akaanza kuwa suspicious. Nadhani labda kwa sababu dots zake zilikua haziungi vizuri. Akiniuliza kuhusu manzi (kwa sababu anajua tupo kundi moja) namjibu tu anaendelea poa. Akiniomba nichunguze kama kuna mshikaji yupo na manzi tayari ndio maana yeye anapotezewa nampa tu matumaini kuwa manzi bado hana mtu. Dah, kumbe pale uzi wake unapokatika ndipo unapounga wangu. Penzi ni kama harufu ya bangi ukivuta lazima usanukiwe tu, sikuchukua round, bulalifuu.
Mwamba nimechanga karata zangu vizuri najua kila kitu kipo sawa, nashangaa siku moja naamshwa ahsubui napewa hongera na room'ate. Ya nini tena? Kumbe manzi kani post huko facebook kaniita "secret admire". .. aiseeee
Jamaa ananiongelesha huku machozi yanamlenga lenga.
"Mwanangu siku zote tunakaa wote hapa nakueleza mambo yangu kumbe unanizunguka?"
Kastori ni karefu kidogo, ngoja ninywe maji, narudi kumalizia...