Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

wanabodi
heshima yenu wakuu!
Mie nina wazo iwapo mtaridhia ama litawapendeza
nafikiri kuwa mleta uzi
akimaliza kuleta kitabu chote
I mean sura zote!

Basi ni vizuri tukawa na utaratibu wa kufanya uchambuzi sisi kwa sisi!
Mjadala huru
Kuanzia sura ya 1 hadi ya mwisho.
Ili maswali yawepo, maoni, ushauri, mapendekezo pia

Then Mwisho kabisa tunapendekeza kwa pamoja
Jina la kitabu kinachofuata.
Haya ni mawazo yangu tu ila nisameheni iwapo nimewakwaza!
 
MTU MWENYE BAHATI KULIKO WOTE KATIKA BABILONI


Mbele ya msafara wake alikuwepo Sharru Nada. Alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana katika jiji la Babylon. Alipenda kuvalia nguo nzuri na za kisasa. Pia alipendelea wanyama wazuri na hata farasi aliyempanda alikuwa ni wa aina bora kabisa katika Arabia. Kwa kumuangalia mtu asingeweza kujua kuwa umri wake ulikuwa umesonga. Pia ilikuwa ni vigumu zaidi kugundua kuwa hakuwa na amani moyoni mwake.

Safari ya kutoka Damasko hadi Babiloni ilikuwa ni ndefu na yenye magumu mengi sana. Lakini hili silo jambo lililomhangaisha. Pia njiani kulikuwa na makabila katili ya waarabu wa jangwani ambao muda wote walikuwa wanatamani kupora misafara ya wafanyabiashara matajiri. Lakini hawa pia hakuwaogopa sababu alikuwa na walinzi wa kutosha.

Kilichomhangaisha ni kijana aliyekuwa kapanda farasi pembeni yake. Kijana huyu alikuwa ametoka naye Damasko, jina lake Hadan Gula. Hadan Gula alikuwa ni mjukuu wa mshirika wake wa siku nyingi katika biashara, Arad Gula. Moyoni alikuwa akihisi ana deni kwa Arad Gula, deni ambalo alihisi asingeweza kulilipa kamwe. Alitamani kufanya kitu kumsaidia mjukuu wake lakini hakujua cha kufanya na hasa ni kutokana na kijana mwenyewe.

Kila akiangalia hereni na pete alizoavaa yule kijana aliwaza,
"Inakuwaje huyu anafikiri vito huvaliwa na wanaume lakini ni mkakamavu kama babu yake? babu yake hakuvaa na kujipamba namna hii."
Pamoja na hayo bado akawa ameamua kumchukua na kumsaidia kujenga maisha yake. Baba yake alikuwa ametapanya mali zote zikizoachwa na babu yake.

Hadan Gula alimkatisha mawazo yake kwa kusema. "Kwanini unafanya kazi kwa kujitesa. Kwanini mara zote unasafiri na msafara wako wa biashara? Kwanini hupumziki na kufurahia maisha?"

Sharru Nada akatabasamu na kusema. "kufurahia maisha? Ungekuwa wewe ndiyo mimi, ungefanya nini ili kufurahia maisha?"

"Ningekuwa tajiri kama wewe ningeishi kama mwana mfalme. Nisingejitaabisha kusafiri jangwani kwenye joto. Kila shekeli inayoingia ningeitumia kufurahia maisha. Ningevaa nguo za gharama na kujipamba kwa vito adimu. Hayo ndiyo yangekuwa maisha yangu, maisha matamu."

Baada ya kusema na kusikia hayo wote wakacheka.

"Babu yako hakuvaa vito." Alisema Sharru Nada kwa kushutumu lakini akaona si sawa, akabadili na kusema kwa utani. "Inamaana hautakuwa na muda wa kufanya kazi?"

"Kazi ni kwaajili ya watumwa," alijibu Hadan Gula. Sharru Nada aliuma meno kwa hasira lakini hakusema neno. Waliendelea kusafiri kimyakimya hadi walipofika kwenye mteremko unaoelekea kwenye bonde pana sana. Hapa Sharru Nada alisimamisha farasi wake na kumuonyesha Hadan Gula bonde la kijani lililokuwa linaonekana kwa mbali. "Unaona lile bonde? Angalia kwa mbali utaona ukuta wa Babiloni, ule mnara ni mnara wa hekalu la Beli. Kama macho yako yako vizuri utaona moshi kutoka kwenye moto unaowaka daima juu ya mnara huo.

"Kwa hiyo pale ndiyo Babiloni? Siku zote nilitamani kuona mji tajiri zaidi duniani," alisema Hadan Gula . Huu ni mji ambao babu yangu alianza kujenga utajiri wake. Kama angekuwa hai tusingekuwa tunahangaika."

"Kwanini unataka roho yake ikae duniani kuliko muda uliopangwa? Wewe na baba yako mnaweza kuendeleza kazi yake nzuri."

"Bahati mbaya sisi hatuna kipaji kama chake. Baba yangu na mimi hatujui siri ya utajiri wake."

Sharru Nada hakujibu kitu bali alianza kuongoza farasi wake kwa uangalifu kushuka bondeni. Nyuma yao ulifuata msafara mkubwa uliokuwa ukitimua vumbi jekundu. Baada ya mwendo wakafika kwenye barabara ya kwenda Babiloni na wakaishika kuelekea kusini kupitia kwenye mashamba ya umwagiliaji.

Kulikuwa kuna wanaume watatu wakilima shambani. Sharru Nada aliwaangalia na kuhisi kama amewahi kuwaona sehemu, jambo la ajabu kabisa! Yaani mtu apite shambani baada ya miaka arobaini na awaone watu wale wale wakilima! Lakini kuna kitu kilikuwa kinamwambia ndiyo wale aliowaona miaka arobaini iliyopita. Mmoja kwa mikono isiyo na nguvu alikuwa ameshikilia jembe la kulimia na wengine walisimama pembeni ya ng'ombe wakiwachapa kuwaongoza. Miaka arobaini iliyopita aliwaonea wivu watu hawa. Wakati huo alitamani angekuwa wakulima wale na ingetokea wangesema wabadilishane kazi angekubali kwa mikono miwili! Lakini sasa hali ilikuwa tofauti. Kwa kujivuna akaangalia msafara wake wa biashara, ngamia na punda walikuwa wamejaa mizigo ya thamani kutoka Damasko. Pamoja na wingi wa mali ile lakini ilikuwa ni sehemu tu ya mali zake.

Alimuonyesha Hadan Gula wale wakulima na kusema, "bado wanalima shamba lile lile walilokuwa wanalima miaka arobaini iliyopita?"

"Kwanini unafikiri ni wakulima walewale?"
"Niliwaona palepale," akasema Sharru Nada huku kumbukumbu zikimjia kwa kasi, hakujua kwanini kumbukumbu za zamani hazimwachi, ghafla akaona sura yenye tabasamu ya Arad Gula ikimjia. Hapo akaona kikwazo cha kufikia akili ya yule kijana mbinafsi na asiyejali kikiondoka.

Aliwaza jinsi ya kumsaidia kijana yule mwenye kujikweza na mwenye mawazo ya kutumia na kununua vito tu. Ana kazi nyingi ambazo angeweza kumpa mtu aliyetayari kufanya kazi lakini si yule anayeona kufanya kazi ni kujishusha. Hata hivyo bado alihisi ana deni kwa Arad Gula. Hivyo anatakiwa kumsaidia yule kijana kwa uwezo wake wote na si kumsaidia kishingo upande. Yeye na Arad Gula hawakuwa watu wa kufanya mambo kishingo upande.

"Unataka kufahamu jinsi mimi na babu yako tulivyoanza ushirika, ushirika uliotuletea faida kubwa?" Alimuuliza Hadan Gula.
"Kwanini usiniambie jinsi unavyopata shekeli za dhahabu? Hilo ndilo ninalotaka kusikia," alisema Hadan Gula.

Sharru Nada hakujali jibu hilo na kuendelea kusema. "Mara ya kwanza kuonana na wale watu wanaolima nilikuwa na umri kama wako tu. Msafara wetu ulipita karibu na shamba lao. Mzee mmoja aliyeitwa Megiddo ambaye tulikuwa tumefungwa pamoja alisema kwa kejeli kuhusu ulimaji wa wale watu, alisema. '''Ona wale wavivu wanavyolima. Mshika jembe hakandamizi jembe lifike chini na muongoza ng'ombe hafuati njia vizuri. Watapataje mavuno mazuri kama wanalima hovyo hovyo namna hiyo?'

"Unasema Meggido alikuwa kafungwa pamoja na wewe?" Aliuliza Hadan Gula kwa mshangao.
"Ndiyo, tulifungwa ringi za shaba shingoni na mnyororo mrefu ulituunganisha. Baada ya Megiddo alifuata Zabado, mwizi wa kondoo. Huyu nilimfahamu toka nipo Haroun. Mwisho alikuwa mtu tuliyemwita Haramia sababu hakutuambia jina lake. Tulidhani atakuwa ni baharia kwa sababu alikuwa amejichora tatuu ya nyoka aliyejikunja kifuani mwake kama ambavyo mabaharia hujichora. Tulikuwa tunatembea watu wanne wannne tukiwa tumeunganishwa pamoja kwa minyororo.

"Ulikuwa mtumwa?" Aliuliza Hadan Gula akiwa haamini.
"Babu yako hajawahi kukuambia kuwa nimewahi kuwa mtumwa?"

"Alikuwa anakuongelea mara nyingi lakini hajawahi kugusia hili."

"Babu yako alikuwa ni mtu unayeweza kumuamini kutunza siri hata iwe nzito kiasi gani. Bila shaka na wewe ni mtu ninayeweza kukuamini, sivyo?" Sharru Nada aliongea hayo huku akimkazia macho Hadan Gula.
"Usiwe na shaka, sitasema chochote, lakini hili jambo limenishangaza sana. Ilikuwaje hadi ukawa ntumwa?"

Sharru Nada akabinua mabega na kusema, "mtu yeyote anaweza kuwa mtumwa. Ilikuwa kamari na pombe ndivyo vilivyonitia matatizoni. Nilikuwa mhanga wa matendo ya hovyo ya kaka yangu. Kaka yangu limuua rafiki yake katika ugomvi. Baba yangu aliniweka kama dhamana kwa yule mjane ili kumlinda kaka yangu dhidi ya mkono wa sheria. Aliposhindwa kupata pesa ya kunikomboa yule mama kwa hasira akaniuza kwa mfanyabiashara ya watumwa."

"Hiyo siyo haki kabisa!" Akasema Hadan Gula. "Sasa uliwezaje kuwa huru?"
"Hilo tutalizungumza baadaye kidogo. Acha tuendelee na hadithi yangu.
 
Ni kitabu kizuri sana, kinasema mtu mwenye bahati ni yule anayetake risk lakini anatake risk kwa jambo ambalo ana ujuzi nalo.
Hadi sasa kwangu ni kama dhambi nisipo save angalau asilimia 10% ya pesa yoyote nitakayo pata, huwa naita pesa ya Arkad.
 
Tulipokuwa tunapita, wale wakulima walituzomea. Mmoja wao akavua kofia yake na kuinama kwa dhihaka na kusema, "karibuni Babiloni wageni wa mfalme. Mfalme anawasubiria kwenye kuta za jiji na amewaandalia karamu. Tofali za udongo na supu ya vitunguu. Hapo wakulima wote walicheka kwa sauti kubwa sana.

"Haramia alipandwa na hasira na kuwatukana. 'yule mtu anamaanisha nini nini kusema mfalme anatusubiri kwenye kuta za jiji?' nilimuuliza Haramia.
"Anamaanisha kwenda kufanya kazi ya kubeba tofali kwenye ujenzi wa kuta za jiji hadi mgongo uvunjike. Kabla ya kuvunjika mgongo unaweza pigwa hadi kufa. Mimi siwezi pigwa, nitawaua.

"Haniingii akilini kuongelea kuhusu bwana kumpiga hadi kumuua mtumwa wake anayefanya kazi kwa bidii na kwa kujituma. Mabwana hupenda watumwa watiifu na huwatunza vizuri" alisema Megiddo.

'"Nani anataka kufanya kazi kwa bidii?' alihoji Zabado. 'wale wakulima ni watu wenye akili. Hawafanyi kazi kujichosha, wanategea ila wanajifanya wanafanya kazi kwa bidii.'

'''Huwezi fika popote kwa kutegea kazi,' alipinga Megiddo. Ukilima hekari moja kwa siku ni kazi ya kutosha na bwana anajua hilo. Lakini ukilima nusu hekari tu, huo ni utegezi. Mimi si mtegezi, napenda kufanya kazi kwa ufanisi. Sijutii kuwa na rafiki mzuri kama kazi. Kazi imeniletea vitu vyote vizuri nilivyowahi kumiliki, shamba, ng'ombe, mazao na vingine vyote.'

'''Sasa viko wapi vitu hivyo?' aliuliza Zabado kwa kejeli. 'Mi naonelea ni jambo la akili kutegea kazi. Kama tukiuzwa kufanya kazi kwenye ujenzi wa ukuta mimi nitakuwa mbeba maji au kazi zingine rahisi, wewe unaependa kazi utakuwa ukivunja mgongo kwa kubeba tofali, alimaliza kusema Zabado na kuachia kicheko cha dharau.

"Usiku ule sikuweza kulala, nilikuwa na uoga mkubwa sana. Nilikuwa nimelala karibu na sehemu walipokuwa walinzi, watu wote walipokuwa wamelala nikamsogelea mlinzi wa zamu ya kwanza aliyeitwa Godoso. Godoso alikuwa mmoja ni aina ya wale waarabu katili sana. Hakujali kitu wala hakuwa na huruma. Kama akikupora pesa atataka akuchinje pia.

'''Godoso naomba uniambie kitu kimoja,' nilinong'ona. 'Tukifika Babiloni tutauzwa kwaajili ya kazi ya kujenga ukuta?'

'''Kwanini unataka kujua?' aliuliza Godoso kwa udadisi.

'''Ina maana huelewi?' nilimwambia kinyonge, mimi bado ni kijana, nataka kuishi. Sitaki kufanya kazi au kupigwa hadi kufa huko kwenye kuta. Kuna uwezekano nikapata bwana mwema?'

'''Nitakwambia kitu,' alisema Godoso kwa kunong'ona. Wewe ni mtu mzuri, hujanisumbua kwa lolote. Mara nyingi tunaenda kuuza watumwa kwenye soko la watumwa. Sasa nisikilize kwa makini, wanunuzi wakija waambie wewe ni mfanyakazi mwenye bidii na unapenda kufanya kazi kwa bwana mwema. Wafanye watake kukununua. Usipofanya hivyo kesho yake utajikuta kwenye kazi ya kubeba tofali, kazi ngumu sana.'

"Baada ya Godoso kuondoka nilijilaza mchangani huku nikiangalia nyota na kufikiria kuhusu kazi. Niliwaza iwapo nitaweza kuifanya kazi kuwa rafiki yangu kama Megiddo alivyosema kuwa rafiki yake mkubwa ni kazi. Niliona ili niepukane na kwenda kutumikishwa kwenye kuta lazima niifanye kazi kuwa rafiki yangu.

"Megiddo alipoamka nikamueleza ile habari. Hilo ndilo lilikuwa tumaini letu pekee la kuepuka mateso ya kufanya kazi kwenye ujenzi wa ukuta. Mchana wa siku hiyo tulikaribia kuta za jiji la Babiloni. Tuliona watu wengi wako kwenye mistari, wengi kama siafu. Walikuwa wakipanda na kushuka kwenye mteremko mkali kupitia njia zilizopindapinda. Tulivyokaribia zaidi tulishangaa kuona maelfu ya watu wakifanya kazi. Kuna waliokuwa wakichimba bwawa. kuzunguka ukuta na wengine wakifyatua tofali. Wengi wao walikuwa wakibeba tofali kwenye vikapu wakiwapelekea wajenzi.
"Wasimamizi waliwatukana walioonekana kutegea na waliwachapa kwa mijeledi wale ambao hawakufuata mistari. Watumwa wengine walionekana kutembea kidhaifu na wengine wakianguka na wasiweze kuinuka tena. Hawa walipigwa mijeledi ili kuwaamsha na kama walishindwa kuamka basi walisogezwa pembeni ya njia ambapo waliendelea kuugulia. Baada ya muda waliburuzwa mpaka kwenye rundo la miili mingine iliyokuwa inasubiria maziko yasiyo na heshima. Moyo ulininyong'onyea na kikatetemeka kwa uoga nilipoona mambo hayo. Niliwaza kuwa hali hiyo ndiyo inayonisubiri iwapo nitashindwa kununuliwa kwenye soko la watumwa.

"Ilikuwa kama Godoso alivyosema. Tulichukuliwa mpaka ndani ya jiji na kufungwa kwenye jela ya watumwa. Asubuhi ilipofika tulipelekwa na kufungiwa kwenye mahabusu za soko la watumwa. Hapo watumwa wengi walijikusanya pamoja kwa woga na ni mijeledi ya walinzi ndiyo iliyoweza kuwagawa. Mimi na Megiddo tuliongea na kila mnunuzi aliyeweza kutusikiliza.
"Yule mchuuzi wa watumwa alileta wanajeshi kutoka kikosi cha ulinzi wa mfalme. Hawa walimfunga Haramia na kumpiga kikatili alipokuwa akikataa. Nilimuonea huruma walipokuwa wakiondoka naye.

"Megiddo alihisi kwamba naye ataondoka muda si mrefu hivyo wanunuzi walipokuwa mbali akanisisitiza jinsi kufanya kazi kwa bidii kutakavyonipa manufaa hapo baadaye. 'Wengine wanachukia kazi, wanaifanya kuwa adui yao. Ni vyema uifanye kama rafiki yako. Jitahidi uipende. Usijali hata kama ni ngumu kiasi gani. Mtu anayetaka kujenga nyumba nzuri hatawaza sana juu ya uzito wa nguzo au umbali wa kufuata maji ya kujengea. Niahidi kuwa iwapo utapata mnunuzi mzuri basi utafanya kazi kwa bidii yako yote. Hata kama hata thamini kazi yako wewe usijali. Kumbuka kuwa kazi ikifanywa vizuri inamnufaisha anayeifanya. Inamfanya kuwa mtu bora.'

Aliacha kuzungumza pale mkulima mmoja aliposimama karibu yetu na kuanza kutuchunguza.
"Megiddo alimuuliza kuhusu shamba lake na mazao yake. Haikuchukua muda yule mkulima akaona kuwa Megiddo atamfaa. Baada ya mabishano makali kuhusu bei, mkulima yule alitoa pochi kubwa kutoka mfukoni, alilipa na kuondoka na Megiddo.
 
"Watu wengine wachache waliuzwa asubuhi ile. Ilipofika mchana, Godoso akaniambia kuwa mchuuzi wa watumwa alikuwa kachoka na hakutaka kukaa usiku mwingine pale. Hivyo, ikifika jioni atawachukua watumwa waliobaki na kwenda kuwauza kwa mnunuzi wa mfalme. Nilikata tamaa nilipoona mtu mmoja mnene na nadhifu akija na kuuliza iwapo kati yetu kuna mtu ana ujuzi wa kuoka mikate.

"Nilimsogelea na kumwambia, 'kwanini muoka mikate bora kama wewe unatafuta mwingine ambaye hatakuwa na ujuzi wa juu kama wewe? Huoni kuwa ni rahisi kumfundisha mtu ambaye yuko tayari ili aweze kutengeneza kwa kiwango kama chako? Niangalie vizuri mimi, mimi ni kijana, nina nguvu na nina bidii ya kazi. Nipe nafasi nami nitafanya kila niwezalo kukuzalishia fedha na dhahabu."

"Mtu yule alivutiwa na maelezo yangu na akaanza kubishana na yule mchuuzi. Hapo mwanzo yule mchuuzi alikuwa hana hata habari na mimi lakini aliposikia nataka kununuliwa akaanza kunipamba kwa sifa. "Huyu ana afya njema na tabia njema pia.' Nilijihisi kama ng'ombe aliyenona anayetaka kuuzwa kwa mchinjaji. Baada ya muda walikubaliana bei, nilifurahi sana. Nilimfuata bwana wangu huku nikiwaza kuwa nina bahati kuliko watu wote katika Babeli.

"Makazi yangu mapya niliyapenda. Bwana wangu, Nana-Naid alinifundisha jinsi ya kusaga shayiri kwenye jiwe, jinsi ya kuwasha moto kwenye jiko la kuokea na jinsi ya kusaga unga laini wa ufuta kwaajili ya keki za asali. Makazi yangu yalikuwa kwenye ghala la nafaka. Kulikuwa pia na mtumwa mwanamke mzee aliyekuwa akitunza nyumba, aliitwa Swasti. Swasti alinipenda sana. Alinipatia chakula cha kutosha na alifurahi nilipokuwa nikimsaidia kazi ngumu.

"Hapa nilipata fursa niliyokuwa nimeitafuta sana, fursa ya kumpendeza bwana wangu huku nikiwa na matumaini ya kupata njia ya kuwa huru tena.
"Nilimuomba Nana-Naid anifundishe jinsi ya kukanda na kuoka mikate. Alinifundisha na alifurahi jinsi nilivyokuwa najituma. Nilipoelewa hili kikamilifu nikamuomba anifundishe jinsi ya kutengeneza keki za asali. Baada ya muda mfupi nikawa ndiye muokaji mkuu. Mmiliki wangu alifurahia kukaa na kupumzika siku nzima, lakini hiki suala halikumpendeza Swasti, alikuwa akitingisha kichwa na kusema, 'binadamu kukaa bila kazi si jambo jema kwa afya yake.'

"Kutoka hapo nikaanza kufikiria namna ya kujipatia kipato ili niweze kununua uhuru wangu. Kazi ya kuoka iliisha mchana, nikawaza iwapo Nana-Naid atanikubalia kwenda kutafuta kazi ya kufanya baada ya hapo na kisha tugawane malipo yangu. Lakini wazo lingine likanijia, 'kwanini usitengeneze keki nyingi za asali na uzitembeze kwa watu wenye njaa kwenye mitaa ya jiji?"

"Nikamueleza Nana-Naid mpango wangu nikisema: 'iwapo ningeweza kutumia muda wa baada ya kumaliza kazi kukuzalishia pesa utakubali tugawane pesa nitakayopata ili niweze kujinunulia mahitaji madogomadogo?
"Hilo halina shida,' alinijibu. Nilipomwambia mpango wa kutembeza keki za asali alifurahi sana.

"Hivyo ndivyo itakavyokuwa,' aliniambia. 'Ukiuza keki mbili kwa senti moja mimi nitachukua nusu senti kwaajili ya kulipia unga, asali na kuni za kuokea. Nusu itakayobaki, mimi nitachukua robo na wewe robo.'
"Nilifurahi sana kwa ukarimu wake wa kuniruhusu kubaki na robo ya mauzo yangu. Usiku ule nilifanya kazi kwa bidii kutengeneza sinia kwaajili ya kuuzia. Nana-Naid alinipatia moja ya nguo zake kuukuu ili nionekane nadhifu na Swasti alinisaidia kuishona na kuifua.
 
Sijaelewa kidogo hapo anaposema inatakiwa ujilipe 10% ya mapato yako. Je ansmaanisha ndani ya hiyohiyo 10% ndio uweze kumudu matumizi ya kila siku? Na nyingine uwekeze izalishe ndani ya hiyohiyo 10%?. Na vipi kuhusu 90% inayobaki?. Mlioelewa tafadhali mtueleweshe sisi wa Std 4.
10% unayojilipa una save kwa ajili yakuja kuwekeza hapo baadae,
ili uwekezaji huo uweze kukuingizia kipato na kipato utakachopata kutokana na uwekezaji pia utakuwa unatunza si chini ya 10% akiba kwa ajili ya kuwekeza tena.

90% ndiyo utakayotumia katika matumizi yako lazima (matumizi muhimu) na sio matamanio.
Mfano: kodi ya nyumba, chakula, umeme etc.

Kumbuka asilimia 10 ni kianzio cha chini , so unaweza kusave zaidi kama kipato chako ni kikubwa,

Au unaweza kujinyima kufanya matumizi ya matamanio zaidi baada ya kuorodhesha matumizi ya muhimu tu.
So inaweza kuwa 20% una save kwaajoli yakuja kuwekeza baadae.
80% kwaajili ya matumizi /bills za kila siku
 
Jamaniiiii!!! Sura iliyopita tumejifunzaa "penye nia Pana njia" tuambie kifupi sura ya tisa inataka tujifunze Nini? Hivyo tu! Asante
Sura ya tisa inahusu profesa wa lugha za kale wa Uingereza. Huyu alipata maandishi ya Dabasir kutoka kwenye magofu ya Babiloni. Akayatafsiri na kushangaa yaliyoandikwa. Akaamua kutumia formula ya mule ya kulipa madeni na kusave hela. Ilimsaidia sana. So ni kama muendelezo wa sura ya muuza ngamia.
 
"Kesho yake nilioka keki za asali za ziada. Zilivutia na kutamanisha sana ndani ya sinia. Niliipokuwa natembea nilipaza sauti nikitangaza biashara yangu. Mwanzoni hakuna mtu aliyeonekana anazitaka na nikaanza kukata tamaa kuendelea kutembeza. Muda ulivyokwenda watu njaa zikawashika na ndani ya muda mfupi nikawa nimeuza kila kitu.

"Nana- Naid alifurahishwa sana na mafanikio yangu na akanilipa robo yangu. Nilifurahi sana kuanza kuingiza kipato. Megiddo alikuwa sahihi aliposema kuwa mabwana huthamini kazi nzuri za watumwa wao. Usiku ule sikulala kwasababu ya furaha. Nilikuwa nikiwaza ni kiasi gani nitapata kwa mwaka na nitahitaji miaka mingapi kuweza kununua uhuru wangu.

"Baada ya kuuza kila siku kwa muda fulani nikapata wateja wa kudumu. Mmoja wao alikuwa si mwingine bali babu yako, Arad Gula. Alikuwa akizunguka mji wote, nyumba kwa nyumba akiuza mazuria. Alikuwa akiongozana na punda wa mizigo pamoja na mtumwa wake mweusi. Alikuwa akinunua keki nne, mbili za kwake na mbili za mtumwa wake. Mara zote walisimama na tulizungumza hadi walipomaliza kula.

"Siku moja babu yako aliniambia kitu ambacho sitakuja kukisahau. 'Kijana napenda keki zako lakini zaidi napenda jinsi unavyofanya biashara yako. Moyo kama huo utakufikisha mbali sana kwenye mafanikio.'

"Lakini wewe Hadan Gula sidhani kama unaelewa umuhimu wa maneno hayo ya kufariji kwa kijana mtumwa. Kijana aliye mpweke ndani ya jiji kubwa akijitahidi kwa kila hali kujitoa katika aibu ya utumwa"

"Niliendelea kuweka zile senti kwa muda wa miezi mingi. Nilianza kuhisi uzito wake kwenye pochi niliyofunga kwenye mkanda kiunoni. Kama Megiddo alivyokuwa amesema, kazi ilijithibitisha kuwa rafiki yangu wa karibu zaidi. Nilikuwa na furaha sana lakini Swasti alianza kuwa mtu mwenye wasiwasi mwingi. "Ninapatwa na wasiwasi kwa sababu bwana wetu anatumia muda mwingi sana kwenye nyumba ya kuchezea kamari,' alisema.

"Siku moja nilikutana na Megiddo mtaani, nilifurahi sana. Alikuwa anawaongoza punda watatu waliobeba mboga kuelekea sokoni. 'Naendelea vizuri sana,' aliniambia. 'Mmiliki wangu anafurahishwa na kazi yangu na sasa kaniweka kuwa msimamizi. Si unaona hadi ananiamini kwenda sokoni kuuza? Pia ana mpango wa kuniletea familia yangu. Kufanya kazi kwa bidii kumenisaidia kutoka ndani ya matatizo. Siku moja itanisaidia kujinunulia uhuru wangu mwenyewe na kuweza kumiliki shamba langu mwenyewe tena.'

"Siku zilivyokwenda biashara ilizidi kushamiri. Nana-Zaid alikuwa kila siku akinisubiria nirudi kwa hamu. Nikifika alihesabu pesa na kuzigawa. Pia alinihimiza kutafuta masoko zaidi ili kuongeza mauzo.

"Mara nyingi nilikwenda nje ya jiji kuwauzia wasimamizi wa watumwa waliokuwa wakijenga ukuta. Sikupenda hali ya kule lakini wasimamizi walikuwa wateja wazuri sana. Siku moja nilishangaa kumuona Zabado akiwa amesimama kwenye mstari akisubiri kikapu chake kiwekwe tofali. Alikuwa amechoka na mgongo wake ulipinda ukiwa na makovu na vidonda vya mijeledi ya wasimamizi. Nilimuonea huruma na kumpatia keki ambayo aliila kwa pupa kama mnyama mwenye njaa kali. Kwa jinsi alivyoziangalia keki kwenye sini kwa uchu niliondoka haraka kabla hajanipora sinia langu.

"Siku moja babu yako, Arad Gula aliniuliza, 'kwanini unafanya kazi kwa bidii sana?' Ni kama tu swali uliloniuliza leo, unakumbuka? Nilimwambia ambacho Megiddo aliniambia kuhusu kazi na jinsi ambavyo kazi imekuwa rafiki yangu mzuri. Nilimuonyesha pochi yangu yenye pesa kwa kujivuna itna kumwambia kuhusu mpango wangu wa kununua uhuru wangu.

'''Utakapokuja kuwa huru utatafanya kazi gani?' aliniuliza.

'''Nina mpango wa kuwa mfanyabiashara,' nilimjibu.

'''Hapo Arad Gula aliniambia jambo ambalo sikuamini masikio yangu. 'unafahamu kuwa na mimi ni mtumwa? Hii biashara nipo kwenye ushirika na bwana wangu.'''

"Ishia hapohapo!" Aling'aka Hadan Gula. "Siwezi endelea kusikiliza ukimvunjia heshima babu yangu. Babu yangu hakuwa mtumwa," alisema Hadan Gula huku macho yamemuiva wa hasira.

Sharru Nada alikuwa mtulivu na kuendelea kusema. "Namheshimu babu yako kwasababu aliweza kujitoa kwenye matatizo na kuwa raia wa maana sana katika Damasko. Si wewe mjukuu wake ni wa aina hiyo? Je, ni mwanaume unayeweza kuukabili ukweli mchungu au ni mtu anayependezwa na uongo wa kufurahisha?"

Hadan Gula alikaa vizuri juu ya farasi wake na kwa sauti ya chini na huzuni akasema. "Babu yangu alipendwa na watu wote. Amefanya mema yasiyo na idadi. Njaa ilipoingia si ni yeye aliyetumia pesa zake kununua nafaka Misri? Si ni yeye aliyetuma msafara wake kuzisafirisha hadi Damasko na kuwagawia watu ili wasife njaa? Sasa leo unaniambia alikuwa mtumwa wa kudharaulika huko Babiloni!"

"Sharru Nada alijibu "kama angeendelea kuwa mtumwa angekuwa mtu wa kudharaulika. Lakini alipotumia jitihada zake kujitoa na kuwa mtu mashuhuri katika Damasko Miungu ilifuta aibu yake na kumpa heshima yao."

"Baada ya kuniambia kuwa naye ni mtumwa akanieleza jinsi ambavyo kwa siku nyingi amekuwa na hamu ya kununua uhuru wake. Sasa amepata pesa za kutosha kununua uhuru wake lakini anawaza kuhusu kazi ya kufanya. Hivi karibuni biashara yake ilikuwa imeyumba na alikuwa anaogopa kuondoka kwa bwana wake na kujitegemea.

"Nilipinga vikali kusitasita kwake na nikamwambia, huna sababu nzuri ya kuendelea kuwa chini ya bwana wako. Hebu onja tena hali ya kuwa mtu huru. Kuishi kama mtu huru na kufanikiwa ukiwa huru. Amua kile unachotaka kufanya na ukikifanya kwa bidii utakifanikiwa. Kazi itakusaidia kufikia malengo yako. Aliondoka huku akinishukuru kwa kumsuta juu ya kusita kwa moyo wake.'
 
"Watu wengine wachache waliuzwa asubuhi ile. Ilipofika mchana, Godoso akaniambia kuwa mchuuzi wa watumwa alikuwa kachoka na hakutaka kukaa usiku mwingine pale. Hivyo, ikifika jioni atawachukua watumwa waliobaki na kwenda kuwauza kwa mnunuzi wa mfalme. Nilikata tamaa nilipoona mtu mmoja mnene na nadhifu akija na kuuliza iwapo kati yetu kuna mtu ana ujuzi wa kuoka mikate.

"Nilimsogelea na kumwambia, 'kwanini muoka mikate bora kama wewe unatafuta mwingine ambaye hatakuwa na ujuzi wa juu kama wewe? Huoni kuwa ni rahisi kumfundisha mtu ambaye yuko tayari ili aweze kutengeneza kwa kiwango kama chako? Niangalie vizuri mimi, mimi ni kijana, nina nguvu na nina bidii ya kazi. Nipe nafasi nami nitafanya kila niwezalo kukuzalishia fedha na dhahabu."

"Mtu yule alivutiwa na maelezo yangu na akaanza kubishana na yule mchuuzi. Hapo mwanzo yule mchuuzi alikuwa hana hata habari na mimi lakini aliposikia nataka kununuliwa akaanza kunipamba kwa sifa. "Huyu ana afya njema na tabia njema pia.' Nilijihisi kama ng'ombe aliyenona anayetaka kuuzwa kwa mchinjaji. Baada ya muda walikubaliana bei, nilifurahi sana. Nilimfuata bwana wangu huku nikiwaza kuwa nina bahati kuliko watu wote katika Babeli.

"Makazi yangu mapya niliyapenda. Bwana wangu, Nana-Naid alinifundisha jinsi ya kusaga shayiri kwenye jiwe, jinsi ya kuwasha moto kwenye jiko la kuokea na jinsi ya kusaga unga laini wa ufuta kwaajili ya keki za asali. Makazi yangu yalikuwa kwenye ghala la nafaka. Kulikuwa pia na mtumwa mwanamke mzee aliyekuwa akitunza nyumba, aliitwa Swasti. Swasti alinipenda sana. Alinipatia chakula cha kutosha na alifurahi nilipokuwa nikimsaidia kazi ngumu.

"Hapa nilipata fursa niliyokuwa nimeitafuta sana, fursa ya kumpendeza bwana wangu huku nikiwa na matumaini ya kupata njia ya kuwa huru tena.
"Nilimuomba Nana-Naid anifundishe jinsi ya kukanda na kuoka mikate. Alinifundisha na alifurahi jinsi nilivyokuwa najituma. Nilipoelewa hili kikamilifu nikamuomba anifundishe jinsi ya kutengeneza keki za asali. Baada ya muda mfupi nikawa ndiye muokaji mkuu. Mmiliki wangu alifurahia kukaa na kupumzika siku nzima, lakini hiki suala halikumpendeza Swasti, alikuwa akitingisha kichwa na kusema, 'binadamu kukaa bila kazi si jambo jema kwa afya yake.'

"Kutoka hapo nikaanza kufikiria namna ya kujipatia kipato ili niweze kununua uhuru wangu. Kazi ya kuoka iliisha mchana, nikawaza iwapo Nana-Naid atanikubalia kwenda kutafuta kazi ya kufanya baada ya hapo na kisha tugawane malipo yangu. Lakini wazo lingine likanijia, 'kwanini usitengeneze keki nyingi za asali na uzitembeze kwa watu wenye njaa kwenye mitaa ya jiji?"

"Nikamueleza Nana-Naid mpango wangu nikisema: 'iwapo ningeweza kutumia muda wa baada ya kumaliza kazi kukuzalishia pesa utakubali tugawane pesa nitakayopata ili niweze kujinunulia mahitaji madogomadogo?
"Hilo halina shida,' alinijibu. Nilipomwambia mpango wa kutembeza keki za asali alifurahi sana.

"Hivyo ndivyo itakavyokuwa,' aliniambia. 'Ukiuza keki mbili kwa senti moja mimi nitachukua nusu senti kwaajili ya kulipia unga, asali na kuni za kuokea. Nusu itakayobaki, mimi nitachukua robo na wewe robo.'
"Nilifurahi sana kwa ukarimu wake wa kuniruhusu kubaki na robo ya mauzo yangu. Usiku ule nilifanya kazi kwa bidii kutengeneza sinia kwaajili ya kuuzia. Nana-Naid alinipatia moja ya nguo zake kuukuu ili nionekane nadhifu na Swasti alinisaidia kuishona na kuifua.
Mungu ni mwema!! amekuleta utumike kwa wakati sahihi!
 
"Siku moja nilitoka nje ya jiji tena, nilishangaa nilipokuta umati mkubwa wa watu umekusanyika. Nilipomuuliza mtu mmoja kuna nini alinijibu, 'hujasikia? Kuna mtumwa amemuua mlinzi hivyo amekamatwa na atachapwa hadi afe kwa uhalifu wake. Hata mfalme mwenyewe atakuwepo hapa leo!'

"Watu walikuwa wengi sana wakiwa wamezunguka nguzo ya kumfunga mtuhumiwa anayechapwa. Niliogopa kusogea karibu nisije mwaga sinia langu la keki. Nilipanda juu ya ukuta uliokuwa unajengwa na kuangalia kutoka juu. Siku hiyo ndiyo nilipata bahati ya kumuona Nebkadneza akiwa amepanda gari la kuendeshwa kwa farasi, gari la dhahabu. Sijawahi ona mtu aliyekuwa kapambwa ghali kiasi kile. Kwenye nguo zake kulikuwa dhahabu ikining'inia na nguo za hariri.

"Sikuweza kuona anayechapwa lakini niliweza kusikia kilio chake. Niliwaza inakuwaje mfalme wetu mwema anaruhusu ukatili kama ule na cha kushangaza alikuwa anacheka na kutaniana na watu wengine mashuhuri. Hapo nilifahamu kuwa alikuwa ni katili sana na pia nikaelewa ni kwanini wale watu hufanyishwa kazi ya kujenga ukuta kama wanyama.

"Baada ya mfungwa yule kufa, mwili wake ulitundikwa kwenye nguzo kichwa chini miguu juu ili kila mtu aone. Watu walipopungua nilisogea kuona mwili ule. Kwenye kifua chake niliona tatuu ya nyoka aliyejikunja. Alikuwa ni Haramia!

"Siku niliyokutana tena na Arad Gula alikuwa amebadilika sana. Alikuwa mchangamfu na alinisalimia. 'Tazama mtumwa aliyekuwa unamjua sasa ni mtu huru. Tayari biashara yangu inakua na mke wangu ana furaha. Yeye ni mtu huru pia, mpwa wa bwana wangu. Amenishauri tuhamie mji ambao hakuna mtu anayejua kuwa nimewahi kuwa mtumwa. Anataka watoto wetu wasikue na aibu kuwa baba yao alikuwa mtumwa. Kazi imekuwa msaidizi wangu mkubwa, imenirudishia kujiamini na kuongeza uwezo wangu wa kufanya biashara.'

Nilifurahi kuwa ushauri wangu ulikuwa umemsaidia.

"Siku moja jioni Swasti alinifuata akiwa mwenye wasiwasi sana: 'Bwana wetu ana tatizo, nina wasiwasi juu yake. Miezi kadhaa iliyopita alipoteza pesa nyingi kwenye mchezo wa kamari. Mkulima ambaye humletea nafaka na asali hajamlipa. Pia alikopa pesa sehemu na hajalipa. Watu hao wana hasira juu yake na wameanza kumtishia.'''

"Kwa nini tunajihangaisha na matatizo yake. Sisi si walezi wake,' nilisema bila kufikiri.

'''Kijana mpumbavu! Huelewi chochote. Amekuweka wewe kama dhamana kwa mkopesha pesa. Chini ya sheria, mkopeshaji anaweza kukuchukua na kukuuza. Mimi sielewi cha kufanya, Nana-Naid ni bwana mzuri, hata sielewi kwanini amejiingiza kwenye matata haya?'

"Swasti alikuwa sahihi kabisa kuwa na wasiwasi. Asubuhi moja nilipokuwa naoka mikate mkopesha pesa alifika akiwa na mtu mwingine aliyeitwa Sasi. Yule mtu aliniangalia na kusema kuwa nitafaa.

"Yule mkopesha pesa hakusubiri bwana wangu arudi bali alimwambia Swasti amjulishe kuwa amenichukua. Nilichukuliwa nikiwa na nguo nilizovaa tu na pochi yangu ya pesa kwenye mkanda.

"Nilichukuliwa kama vile mti unaong'olewa toka msituni na kimbunga na kutupwa baharini. Matumaini yangu yalipotea. Kwa mara nyingine kamari na bia ziliniletea matatizo.

"Sasi alikuwa ni mkatili na mtu asiye na mzaha. Alipokuwa ananiongoza kupita jijini nilimueleza kuhusu kazi nzuri niliizomfanyia Nana-Naid na nikamwambia kuwa natumaini kumfanyia kazi nzuri pia. Majibu yake yalikuwa ya kukatisha tamaa kabisa. Alijibu:

"'Sipendi hii kazi na bosi wangu haipendi kata kidogo. Mfalme amemuagiza anitume nikajenge sehemu ya mfereji. Ameniambia ninunue watumwa wengi na wafanye kazi kwa bidii ili iishe haraka. Boh! Mtu anawezaje kumaliza haraka kazi kubwa namna ile?"

"Piga picha ya jangwa lisilo na miti bali vichaka vidogovidogo vya hapa na pale. Jua linawaka hadi maji kwenye mapipa yanakuwa ya moto na hayanyweki. Tena piga picha msururu wa watu wakishuka chini unakochimbwa mfereji na kutoka wamebeba vikapu vizito vya udongo toka asubuhi hadi usiku unapoingia. Vuta picha chakula kimewekwa ndani ya karai refu na tumejipanga tukila kama nguruwe. Kulikuwa hakuna hema wala kitanda cha nyasi. Hayo ndiyo maisha niliyoishi. Pochi yangu ya fedha niliichimbia sehemu nilipoweka alama lakini sikuwa na matumaini iwapo nitakuja kuichimbua.

"Mwanzoni nilifanya kazi kwa bidii lakini kadri miezi ilivyozidi kwenda nilianza kukata tamaa.
Nilipatwa na homa kutokana na joto kali na nikapoteza hamu ya kula. Usiku nilikuwa nikijigeuza geuza tu kwa kukosa usingizi.

"Katika taabu ile nilikumbuka maneno ya Zabado, 'kutojivunja mgongo kwa kutegea kazi'. Hapo nikakumbuka hali niliyomuona nayo kwa mara ya mwisho. Nikaona kuwa mbinu yake haisaidii kitu.

"Nikamkumbuka Haramia na ujeuri wake. Nikawaza iwapo nipambane na kuua. Lakini kumbukumbu ya mwili wake uliojaa damu ikaniambia kuwa mbinu yake haisaidii kitu.

"Mwishowe nikakumbuka mara ya mwisho niliyoonana na Megiddo. Mikono yake ilikuwa imekomaa kwa kufanya kazi kwa bidii lakini uso wake ulikuwa ni wenye furaha sana. Mbinu yake ndiyo ilikuwa bora zaidi.
 
"Lakini nilikuwa nimefanya kazi kadri ya uwezo wangu. Hata Megiddo mwenyewe asingeweza fanya zaidi ya pale. Sasa kwa nini kazi hiyo haujaniletea mafanikio?
Je, kweli ni kazi ndiyo iliyompatia Megiddo mafanikio au ni baraka za Miungu? Inamaana nitafanya kazi maisha yangu yote bila kufikia malengo yangu, furaha na mafanikio? Maswali haya yote yalizunguka kichwani mwangu lakini sikuwa na jibu. Kwa kweli nilikuwa nimechanganyikiwa.

"Siku kadhaa mbele niliona kama uvumilivu wangu umefika mwisho na maswali yangu bado kupata majibu ghafla niliitwa kwa Sasi. Tarishi alikuwa ametumwa kunipeleka kwa bwana wangu ndani ya Babiloni.

Nilichimbua pochi yangu na kuifunga kwenye nguo zangu zilizochanikachanika na kuondoka.
"Tulipokuwa safarini nilihisi kama kimbunga kinanichukua na kunipeleka huku na huku. Ilikuwa kama naishi kwenye maneno ya ajabu yaliyopendwa kuimbwa nyumbani kwetu Haroun.

Linamuangukia mtu kama kimbunga
Linampeleka kama tufani
Hakuna anayejua anakoelekea
Hakuna ajuaye mwisho wake


"Inamaana mimi nimeandikiwa kuadhibiwa maisha yangu yote? Ni magumu gani mapya yananisubiri?

"Fikiria jinsi nilivyoshangaa kumkuta Arad Gula kwenye ua wa nyumba ya bwana wangu akinisubiri. Alinisaidia kushuka na kunikumbatia kama vile nilikuwa ndugu yake tuliyepotezana siku nyingi.

"Tulipokuwa tunaondoka nilikuwa namfuata kama vile mtumwa amfuatavyo bwana wake lakini hakuruhusu hilo. Alizungusha mikono yake kwenye mabega yangu na kusema. 'Nimekutafuta kila sehemu. Nilipokuwa karibu kukata tamaa nikakutana na Swasti ambaye alinisimulia habari ya mkopesha pesa ambaye naye alinionyesha kwa aliyekuwa akikumiliki sasa. Tulibishana sana kuhusu bei na imenigharimu pesa nyingi kukununua lakini sijutii lolote. Falsafa yako na biashara yangu vimeniwezesha kupata mafanikio haya.

'''Ni falsafa ya Megiddo si yangu,' nilimkatiza

'''Ni yako na Megiddo, asanteni nyote. Tunaelekea Damasko na ningependa uwe mshirika kwenye biashara yangu, utakuwa mshirika ukiwa mtu huru.' Alisema hayo kwa furaha huku akitoa bamba lililoandikwa hati ya kununuliwa kwangu. Aliinua bamba lile juu na kulitupa chini ambapo lilivunjika vipandevipande. Hapo alivikanyagakanyaga vile vipande hadi vikawa vumbi tupu.

"Machozi ya furaha yalinitiririka. Nilitambua kuwa nilikuwa mtu mwenye bahati kuliko watu wote katika jiji la Babiloni.

"Kama ulivyoona, katika nyakati za taabu kazi ilithibitika kuwa ndiye rafiki yangu wa kweli. Utayari wangu wa kufanya kazi kwa bidii uliniokoa nisifanye kazi ngumu ya kujenga ukuta. Pia ulimvutia babu yako hadi akanifanya kuwa mshirika wake."

"Je, pia ni kazi ndiyo ilikuwa ufunguo wa siri ya mafanikio na utajiri wa babu yangu?" Aliuliza Hadan Gula.

"Ndiyo ufunguo pekee aliokuwa nao nilipokutana naye kwa mara ya kwanza." Alijibu Sharru Nada. "Babu yako alipenda kufanya kazi. Kutokana na hilo Miungu ilipendezwa naye na ikambariki.'

"Sasa nimeona," akasema Hadan Gula. Kazi ilivutia rafiki zake wengi ambao walistaajabia kazi zake na mafanikio iliyoyaleta. Kazi ilimletea heshima aliyofurahia katika Damasko. Kazi ilimletea yote hayo. Ajabu nilifikiri kazi ni kwaajili ya watumwa."
"Maisha yana vitu vingi ambavyo binadamu anaweza kufurahia," alisema Sharru Nada. "Kila kitu kina mahala wake. Nafurahi kuwa kazi si kitu cha watumwa tu, ingekuwa hivyo ningekuwa nimenyimwa kitu kizuri sana maishani mwangu. Ninafurahia vitu vingi lakini hakuna ninachofurahia kama kazi."

Sharru Nada na Hadan Gula waliongoza farasi wao hadi kwenye ukuta mrefu wa jiji la Babiloni. Hapo waliingia ndani ya jiji kupitia lango kubwa. Walivyokuwa wanaingia walinzi wa lango walisimama kikakamavu na kumsalimia Sharru Nada kwa saluti...... Kwa kujiamini Sharru Nada aliongoza msafara wake kupita lango la jiji hadi kweny mitaa ya jiji.

"Siku zote nimetamani kuwa kama babu yangu," alisema Hadan Gula. "Lakini sikuwahi jua kuwa alikuwa ni mtu wa aina gani hasa. Kwa kuwa umenieleza sasa natambua. Hilo limenifanya nimheshimu zaidi na kutaka kuwa kama yeye hata zaidi. Nina wasiwasi siwezi kukulipa kwa kuniambia siri ya mafanikio yake. Kuanzia leo nitaitumia siri hiyo. Nitaanza kidogokidogo kama alivyoanza. Hilo ni jambo la manufaa kuliko mapambo ya vito na nguo nzuri.

Baada ya kusema hayo Hadan Gula alitoa hereni toka masikioni mwake na akavua pete toka vidoleni. Hapo akaongoza farasi wake na kugeuza. Kwa heshima kubwa akaanza kumuendesha farasi wake akiwa nyuma ya Sharru Nada.


MWISHO
 
Back
Top Bottom