Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaniiiii!!! Sura iliyopita tumejifunzaa "penye nia Pana njia" tuambie kifupi sura ya tisa inataka tujifunze Nini? Hivyo tu! AsanteSababu ya ishu ya hatimiliki sura ya tisa sitaiweka. Tumalize na sura ya kumi.
10% unayojilipa una save kwa ajili yakuja kuwekeza hapo baadae,Sijaelewa kidogo hapo anaposema inatakiwa ujilipe 10% ya mapato yako. Je ansmaanisha ndani ya hiyohiyo 10% ndio uweze kumudu matumizi ya kila siku? Na nyingine uwekeze izalishe ndani ya hiyohiyo 10%?. Na vipi kuhusu 90% inayobaki?. Mlioelewa tafadhali mtueleweshe sisi wa Std 4.
Sura ya tisa inahusu profesa wa lugha za kale wa Uingereza. Huyu alipata maandishi ya Dabasir kutoka kwenye magofu ya Babiloni. Akayatafsiri na kushangaa yaliyoandikwa. Akaamua kutumia formula ya mule ya kulipa madeni na kusave hela. Ilimsaidia sana. So ni kama muendelezo wa sura ya muuza ngamia.Jamaniiiii!!! Sura iliyopita tumejifunzaa "penye nia Pana njia" tuambie kifupi sura ya tisa inataka tujifunze Nini? Hivyo tu! Asante
Mungu ni mwema!! amekuleta utumike kwa wakati sahihi!"Watu wengine wachache waliuzwa asubuhi ile. Ilipofika mchana, Godoso akaniambia kuwa mchuuzi wa watumwa alikuwa kachoka na hakutaka kukaa usiku mwingine pale. Hivyo, ikifika jioni atawachukua watumwa waliobaki na kwenda kuwauza kwa mnunuzi wa mfalme. Nilikata tamaa nilipoona mtu mmoja mnene na nadhifu akija na kuuliza iwapo kati yetu kuna mtu ana ujuzi wa kuoka mikate.
"Nilimsogelea na kumwambia, 'kwanini muoka mikate bora kama wewe unatafuta mwingine ambaye hatakuwa na ujuzi wa juu kama wewe? Huoni kuwa ni rahisi kumfundisha mtu ambaye yuko tayari ili aweze kutengeneza kwa kiwango kama chako? Niangalie vizuri mimi, mimi ni kijana, nina nguvu na nina bidii ya kazi. Nipe nafasi nami nitafanya kila niwezalo kukuzalishia fedha na dhahabu."
"Mtu yule alivutiwa na maelezo yangu na akaanza kubishana na yule mchuuzi. Hapo mwanzo yule mchuuzi alikuwa hana hata habari na mimi lakini aliposikia nataka kununuliwa akaanza kunipamba kwa sifa. "Huyu ana afya njema na tabia njema pia.' Nilijihisi kama ng'ombe aliyenona anayetaka kuuzwa kwa mchinjaji. Baada ya muda walikubaliana bei, nilifurahi sana. Nilimfuata bwana wangu huku nikiwaza kuwa nina bahati kuliko watu wote katika Babeli.
"Makazi yangu mapya niliyapenda. Bwana wangu, Nana-Naid alinifundisha jinsi ya kusaga shayiri kwenye jiwe, jinsi ya kuwasha moto kwenye jiko la kuokea na jinsi ya kusaga unga laini wa ufuta kwaajili ya keki za asali. Makazi yangu yalikuwa kwenye ghala la nafaka. Kulikuwa pia na mtumwa mwanamke mzee aliyekuwa akitunza nyumba, aliitwa Swasti. Swasti alinipenda sana. Alinipatia chakula cha kutosha na alifurahi nilipokuwa nikimsaidia kazi ngumu.
"Hapa nilipata fursa niliyokuwa nimeitafuta sana, fursa ya kumpendeza bwana wangu huku nikiwa na matumaini ya kupata njia ya kuwa huru tena.
"Nilimuomba Nana-Naid anifundishe jinsi ya kukanda na kuoka mikate. Alinifundisha na alifurahi jinsi nilivyokuwa najituma. Nilipoelewa hili kikamilifu nikamuomba anifundishe jinsi ya kutengeneza keki za asali. Baada ya muda mfupi nikawa ndiye muokaji mkuu. Mmiliki wangu alifurahia kukaa na kupumzika siku nzima, lakini hiki suala halikumpendeza Swasti, alikuwa akitingisha kichwa na kusema, 'binadamu kukaa bila kazi si jambo jema kwa afya yake.'
"Kutoka hapo nikaanza kufikiria namna ya kujipatia kipato ili niweze kununua uhuru wangu. Kazi ya kuoka iliisha mchana, nikawaza iwapo Nana-Naid atanikubalia kwenda kutafuta kazi ya kufanya baada ya hapo na kisha tugawane malipo yangu. Lakini wazo lingine likanijia, 'kwanini usitengeneze keki nyingi za asali na uzitembeze kwa watu wenye njaa kwenye mitaa ya jiji?"
"Nikamueleza Nana-Naid mpango wangu nikisema: 'iwapo ningeweza kutumia muda wa baada ya kumaliza kazi kukuzalishia pesa utakubali tugawane pesa nitakayopata ili niweze kujinunulia mahitaji madogomadogo?
"Hilo halina shida,' alinijibu. Nilipomwambia mpango wa kutembeza keki za asali alifurahi sana.
"Hivyo ndivyo itakavyokuwa,' aliniambia. 'Ukiuza keki mbili kwa senti moja mimi nitachukua nusu senti kwaajili ya kulipia unga, asali na kuni za kuokea. Nusu itakayobaki, mimi nitachukua robo na wewe robo.'
"Nilifurahi sana kwa ukarimu wake wa kuniruhusu kubaki na robo ya mauzo yangu. Usiku ule nilifanya kazi kwa bidii kutengeneza sinia kwaajili ya kuuzia. Nana-Naid alinipatia moja ya nguo zake kuukuu ili nionekane nadhifu na Swasti alinisaidia kuishona na kuifua.