Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Hao wanafanana na huyo Serval Cat wanaitwa Savanah Cats, ni breed ya Serval cat na domestic cat walipandikizwa karne ya 20 huko akatokea Savanah Cat, huyu Savanah anafugika ni mpole na mwenye akili,

Ukiona kazaliwa nyumbani ujue anafugika sio wale wa porini.

Wikipedia.
Point iko hapa
Huyo paka ukimwangalia tu unajua ni hybrid
 
Ooh dear nakupenda pia [emoji847].... ni kweli napenda sana Wanyama, nimeweka chombo cha maji nje kwa ajili ya ndege wote kunywa maji, paka usiku najua wanaranda randa hunywa maji pia, najisikia faraja nikiona ndege hadi kunguru wakinywa maji niliyowawekea.
Daaah,so good....mi nataka niache kula nyama nashindwa.... Naumia wanyama wanapochinjwa
 
Daaah,so good....mi nataka niache kula nyama nashindwa.... Naumia wanyama wanapochinjwa
Anza pole pole, mimi nimeanza na nyama ya ng'ombe na mbuzi, kuku bado na ninavyopenda nyama ya kuku sasa [emoji39].... unaanza pole pole kwenye mlo wako unakua na mboga mboga nyingi kuliko nyama, hadi utazoea
 
Jangu lubhaka.
Ni paka wa kawaida tu sema baadhi ya jamii hasa kwetu Ujitani akizaliwa paka wa namna hii anafanyiwa figisu sana, yaani anakuwa na maisha ya mwituni huku nduguze wakinywa maziwa na asali hali inayopelekea kuwa adui mkubwa wa kuku, binadamu.

Nadhani kwa Kiswahili huyu ndo PAKA SHUME.

Jina Paka Shume ni hadi afanye uasi Yaani aanze ujeuri wa kutoishi nyumbani na kutotii, hana makazi maalum kwa mbwa tunasema Mbwa koko ila paka ni Paka shume. Paka shume anaweza kuwa wa aina yoyote.
 
Puma (duma)sio paka huyo anakutafuna mchana kweupe ukikutana nae anga zake.
Alafu kidwahili ndio nini?
Elimu, elimu , elimu
Naomba nikusahihishe, Puma hapatikani Afrika, anapatikana marekani kaskazini na kusini kwa majina ya cougar na mountain lion pia.
Caracal huyo, bingwa wa kuruka juu! Sio serval, lakini ni jamii hiyo hiyo ya paka mwitu pia.
 
Hata simjui jina ila hapa nyumbani kuna paka nahisi sio wa kawaida iwaje ikifika usiku anatoka nyumbani anakuja kwenye biashara yangu ni kama kanatumwa kufanya upelelezi yaana africa kuna matatizo sana.
 
Ndo huyu?

1683174457534.jpeg
 
Hata simjui jina ila hapa nyumbani kuna paka nahisi sio wa kawaida iwaje ikifika usiku anatoka nyumbani anakuja kwenye biashara yangu ni kama kanatumwa kufanya upelelezi yaana africa kuna matatizo sana.
We ndiyo mwenye matatizo.
 
Ni kweli kuna siku paka wangu alishaleta nyoka mzima hapa home [emoji23][emoji23] sasa sisi kuona ivo tukatoka nduki. Nae kuona tumetoka nduki nae akatoka nduki na kumuacha nyoka ndani[emoji51][emoji38] sasa sijui alikua anakimbia nn
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom