Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Inasikitisha sana watu kuwaua hawa jamaa. Bahati nzuri nchi inasehemu kubwa ya hifadhi vinginevyo wangeisha. Elimu ya kutosha itolewe. Tumekuwa wakatili sana kwa wanyama.
 
Kuna siku moja wakati tunasafisha shamba nilikutana na watoto wameterekezwa watoto wa mondo, wakati bado nina tafakari nikiwa nina wasi kuingia territory ya mnyama chui au duma bila tahadhari wakawa wamefika watu kadhaa, bila hata kuuliza hawa vijana walikula rungu za kutosha wale watu wakidai weshaibiwa sana kuku zao so wamemkomesha mama yao aliewaterekeza hawa watoto, ni moja ya jamii ya wanyama wenye kisasi na binadamu sana
wanakuwaga na mikia mirefu kuliko paka wa nyumbani na pia ni warefu zaidi.. macho yao usiku ukiwamulika na tochi yanang'aa zaid ya paka wa nyumbani.
 
Wewe ni mwongo. Huyo mnyama wa porini anazaliwaje nyumbani? Isitoshe ni miongoni mwa wanyama wasioonekana hovyo. MWONGO MKUBWA WEWE.
Mkuu ni elimu tu na kutokujua mambo ndiomaana kaandiKa hivo[emoji1787][emoji23].. jamaa kaandika sirias kabisa kama vile anachokisema ni sahihi[emoji23].

Huyo jamaa anafananisha rangi tu ya paka wa porini na wale paka wenye rangi hiyo ambao hufukuzwa nyumbani
 
Jangu lubhaka.
Ni paka wa kawaida tu sema baadhi ya jamii hasa kwetu Ujitani akizaliwa paka wa namna hii anafanyiwa figisu sana, yaani anakuwa na maisha ya mwituni huku nduguze wakinywa maziwa na asali hali inayopelekea kuwa adui mkubwa wa kuku, binadamu.

Nadhani kwa Kiswahili huyu ndo PAKA SHUME.
Mtaani utotoni alikuwepo mmoja wa hivi. Na kweli aligeuka adui wa binadamu, vyakula na mifugo midogo midogo, alisumbua sana.

Iliundwa kamati ya vijana pamoja na mbwa kadhaa, ile vita ilikuwa balaa sanaa, maana wale mbwa kwanza aliwakalisha vibaya sana, alivimba wote tulisogea pembeni ila mwisho wa siku mwanaharamu yule alipelekwa anapostahili baada ya battle kali sana
 
Usidhani. Hilo ndo jina lake halisi = PAKA SHUME.
 
Anaitwa MONDO.. famous Kwa jina la "wild cat"
Anakula panya kama kawaida, sema anakula adi kuku,kanga Kwa kuwinda..

Apo ni mkubwa...sio kama giant cat wengine yani chui,tiger
 
Mtaani utotoni alikuwepo mmoja wa hivi. Na kweli aligeuka adui wa binadamu, vyakula na mifugo midogo midogo, alisumbua sana.

Iliundwa kamati ya vijana pamoja na mbwa kadhaa, ile vita ilikuwa balaa sanaa, maana wale mbwa kwanza aliwakalisha vibaya sana, alivimba wote tulisogea pembeni ila mwisho wa siku mwanaharamu yule alipelekwa anapostahili baada ya battle kali sana
Kabla ya vita kuanza ni lazima mkazibe matundu ya vichuguu vya karibu. Nilikwaga mwenyekiti wa kamati hii zamani zile. Ikitokea akaingia ndani ya kichuguu,basi matundu mengine yatazibwa,Linabaki 1,unakokwa moto kupitia hilo tundu,pilipili kichaa bila kusahaulika alafu ilo tundu linazibwa pia. Hatorudi tena.
 
Jangu lubhaka.
Ni paka wa kawaida tu sema baadhi ya jamii hasa kwetu Ujitani akizaliwa paka wa namna hii anafanyiwa figisu sana, yaani anakuwa na maisha ya mwituni huku nduguze wakinywa maziwa na asali hali inayopelekea kuwa adui mkubwa wa kuku, binadamu.

Nadhani kwa Kiswahili huyu ndo PAKA SHUME.
Huyo ni paka wa porini anaitwa Serval
 
Back
Top Bottom