Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Ni kweli anafugika.
Kilicho7bisha mimi kugundua kuwa zile tabia za mwituni hutokana na kugeuzwa kuwa adui tulimpuuzia mmoja akaishi tu nyumbani,alikuwa vyema tu km wengine,mlinzi,muaminifu na msafi pia. Sema zile imani zetu dhidi ya paka wa rangi hizi ndizo upelekea na wao kubadili mienendo ili waishi.
Upo sahihi, ukishaishi porini ni lazima uishi kwa mapambano ili usife, tabia hubadilika kulingana na mazingira,

I wish nimpate mmoja niishi nae[emoji7]
 
Jangu lubhaka.
Ni paka wa kawaida tu sema baadhi ya jamii hasa kwetu Ujitani akizaliwa paka wa namna hii anafanyiwa figisu sana, yaani anakuwa na maisha ya mwituni huku nduguze wakinywa maziwa na asali hali inayopelekea kuwa adui mkubwa wa kuku, binadamu.

Nadhani kwa Kiswahili huyu ndo PAKA SHUME.
Mbona anaonekana mkubwa sana kama chui?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kumuona anapita juu ya ukuta tukakutana uso kwa macho, nikamuita ule mlio anaoitwa paka alitoka ndukii, sijamuona tena hadi leo. Nilisikitika sana maana nilitaka tuongee japo kwa dakika kadhaa nimpe na chakula pia. 🥲
Mmhhh kwa profile yako ya ku grind papuch lazima akuogope usijempa kazi asiyoiweza ndio maana akasepa
 
Huyu ni Paka Mkubwa.

Wanaishi sana porini. Wanakula wanyama wadogo kama sungura na nyoka. Wakati nachunga nimewaua wengi sana tu. Wanavizia vitoto vya kondoo na kuviiba..

Ila ni waoga wa binadamu. Vimepotea kweli, zaidi ya miaka 20 sijaviona tena.
 
Mkuu sisi waswahili tumekosa maneno kiasi kwamba tunadhani neno paka huwakilisha mnyama 'nyau', lakini paka "cats" ni jina linalobeba familia ya aina ya wanyama wengi ambao kwa pamoja huitwa paka...
Wapo wengi kama simba, simbamangu, duma, chui, mondo, 'jaguar', 'puma', domestic cat (huyu ndio paka wa nyumbani)
Simbamangu ndio yupi huyo?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Anazaliwa ila anaitwa "Kimbulu" hafugiki huyo anatabia za wanyama wa mwituni anakula vifaranga hatari.

Akizaliwa anapigwa rungu hapo hapo that is why ni adimu kupatikana
Wewe ni mwongo. Huyo mnyama wa porini anazaliwaje nyumbani? Isitoshe ni miongoni mwa wanyama wasioonekana hovyo. MWONGO MKUBWA WEWE.
 
Ni kweli kuna siku paka wangu alishaleta nyoka mzima hapa home 😂😂 sasa sisi kuona ivo tukatoka nduki. Nae kuona tumetoka nduki nae akatoka nduki na kumuacha nyoka ndani😬😆 sasa sijui alikua anakimbia nn
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Mlimshitua.

Paka akimuona nyoka ni lazima amuue,7bu ni kwamba viumbe waliowengi wakijaribu kutembea hata kwa ku nyatnyata kwa lengo la kumfikia paka aliyesinzia haiwezekani.
Pengine ni kutokana na smelling power aliyonayo ama wave frequency humfika haraka,lkn nyoka anaweza kumfikia paka na pengine kumdhuru.

Kwa7bu hiyo sasa,paka anajua kabisa kuwa nyoka ni adui wake hatari sana kuliko wengine wote hivyo adhabu ya kifo inamfaa.
 
Jangu lubhaka.
Ni paka wa kawaida tu sema baadhi ya jamii hasa kwetu Ujitani akizaliwa paka wa namna hii anafanyiwa figisu sana, yaani anakuwa na maisha ya mwituni huku nduguze wakinywa maziwa na asali hali inayopelekea kuwa adui mkubwa wa kuku, binadamu.

Nadhani kwa Kiswahili huyu ndo PAKA SHUME.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna siku moja wakati tunasafisha shamba nilikutana na watoto wameterekezwa watoto wa mondo, wakati bado nina tafakari nikiwa nina wasi kuingia territory ya mnyama chui au duma bila tahadhari wakawa wamefika watu kadhaa, bila hata kuuliza hawa vijana walikula rungu za kutosha wale watu wakidai weshaibiwa sana kuku zao so wamemkomesha mama yao aliewaterekeza hawa watoto, ni moja ya jamii ya wanyama wenye kisasi na binadamu sana
 

Attachments

  • Screenshot_20230328-081457.png
    Screenshot_20230328-081457.png
    1.2 MB · Views: 3
  • Screenshot_20230328-081502.png
    Screenshot_20230328-081502.png
    1.3 MB · Views: 4
  • Screenshot_20230328-081436.png
    Screenshot_20230328-081436.png
    1.1 MB · Views: 3
Back
Top Bottom