Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Hahahah ila life bhana
Niliwahi kupigwa changa na wajanja wakaniacha kwenye waiting lounge ya pantoni pale kigamboni
Sina chochote mfukoni
Nikachapa moyo konde kigamboni hadi hadi vijibweni(nikaomba msaada wa viboti) wakanisaidia kwa masimango sana nikaibukia kurasini..nikachapa mwendo reli kwa reli kurasini,kwa aziz,mtongani nikaungia kilwa road hadi kizuiani pale nikakutana na uncle mudy akanisaidia nauli aisee

Ila nimechapa sana mwendo azania mbagala miaka hiyo
 
Tabata sanene, vingunguti ,via Nyerere road mpaka karume, posta ubungo, mpaka tabata reli via Morogoro road
 
"Nakumbuka 2006 kuna rafiki yangu alikuja Dar, ajira ilikuwa tatizo akakuta tangazo mitaa ya Chang'ombe la vijana.Kufika ofisini wakampatia vitu mbalimbali vya kuuza.
Ndani ya mwezi mmoja jozi tatu za viatu vilikuwa hoi bin taabani.
Umbali alio tembea anajua mwenyewe."
 
Mimi ni mkaziwa Tegeta ungenitafuta ningekusaidia nauli, ******"""


Wakati ninaishi Temeke, safari za miguu Tmk mpaka mbagala nimetembea sana
 
1)Posta to kawe via tanzanite bridge
2)mbezi jogoo to masaki izo one two zilikuwa nyoko sana
 
Ni miaka kama 15 imepita nilikuwa naendesha baiskeli karibu na Kanisa la St Joseph jioni ya 12:30 ghafla trafic akanisimamisha na kuniambia kwanini sitii msafara wa viongozi nikamwambia samahani sikujua kama kuna msafara,akaishika baiskeli na kutoa upepo tairi zote mbili niliikokota hadi mtoni kijichi,nilimuona ni mtu mwenye roho mbaya na sitamsahau.
 
Mara yangu ya kwanza kabisa nilitembea kwa mguu kutoka Azania Sec hadi Kurasis Chuo Cha uhasibu. Mara ya pili nikatembea kutoka Manzese hadi Kariakoo, na mara bya tatu ni kutoka Manzese kwenda chuo kikuu. Hata hivyo niltembea mara nyingi sana kutoka Sinza kwenda Chuomkikuu kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…