Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Nakumbuka siku moja nikiwa msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.

Ila kwa bahati nzuri kukawa na bot linaenda kigamboni siku hiyo basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taiga tukaangalie na Mpira kati ya yanga na mbeya city.

Alifurahi sana tulipofika kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya ksake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilisha shtuka ila nikawa najipa moyo.

Mpaka Moira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Mamaee. Sitasahau magomeni hadi makoka jeshin kwenda kurudi .duhh tumepitia mengi
 
Nakumbuka siku moja nikiwa Msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.

Ila kwa bahati nzuri kukawa na boti linaenda Kigamboni siku hiyo, basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taifa tukaangalie na Mpira kati ya Yanga na Mbeya city.

Alifurahi sana tulipofika Kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya kwake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilishashtuka ila nikawa najipa moyo.

Mpaka Mpira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Kutoka Saba Saba hadi Kariakoo
 
Tabata to Manzese, hizi ruti nimefanya sasa nilipokuwa nasoma shule ya msingi zile siku za weekend nikipewa nauli sipandi daladala. Ila kubwa kuliko nilitoka Kiwanda cha Cement cha Wazo kule Tegeta hadi Mwenge nikiwa na miaka 12 tu. Ilikuwaje... Nilikuwa naishi Tabata nasoma Manzese na enzi hizo daladala zinatoka Buguruni zinapitia Tabata zinaishia Ubungo halafu napanda la Ubungo kwenda Kariakoo nashukia Manzese. Hivyo natakiwa kupanda Mabasi mawili, ile usumbufu wa makonda kuwakataa wanafunzi na kubadilisha magari muda unakwenda ikawa nikipata gari la lift napanda kuepuka huo usumbufu. Nikajenga mazoea, siku hiyo likaja basi la kiwanda cha Cement cha wazo nikapanda, kumbe lile gari likichukua wafanyakazi halisimani ni moja kwa moja hadi kiwandani. Nashangaa kufika Ubungo basi limeshika njia ya kwenda Mwenge na kwa utoto wangu sikuwa na ujasiri wa kuuliza gari inakwenda wapi au lisimame wanishushe. Aisee moja kwa moja hadi Kiwandani. Nashangaa watu wanashuka na kutawanyika na mimi sikuwa na jinsi nikashuka. Bahati nzuri basi ilisimama nje ya geti la kuingia kiwandani. Nikafuata barabara ya basi ilipotoka hadi Tegeta, nilikuwa sipajui kabisa Tegeta na nikawa na hofu nisipange gari nyingine nisije kupotea tena. Nikatembea kwa Miguu hadi Mwenge nikasikia wanatangaza magari ya Kariakoo nikapanda hadi Kariakoo kisha nikapanda basi la kwenda ubungo nikarudi nyumbani Tabata. Siku nzima nilimaliza na ilikuwa ni kipindi cha mitihani ya kufunga muhula. Sikusema nyumbani niliogopa ila shuleni nilidanganya nimefiwa wakanipa mitihani ya siku nisiokuja nikafanya peke yangu. SITOSAHAU!!!
Ulikua unafanya mazoezi ya uchokoraa?
 
Back
Top Bottom