Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

road to road mzee mpaka tandika, hapo nikapata shortcut moja nikatokea stendi ya shamba mbele ya mtongani kidogo, baada ya hapo ni kunyooka mpaka mbagala.

safari ilianza saa 12 jioni nikafika saa 6 usiku nilikuwa napumzika pumzika njiani umo
Ina maana ulipitia njia ya kimara ubungo then riverside then vetenari then changombe hospital then tandika sokoni then njia ya stend ya shamba ukatokea darajani mtongani then msikitini then misheni mpaka sabasaba afu mdogo mdogo mpaka kizuiani,zhakiem afu rangi tatu?????
 
Kutoka keko mpaka kinondoni kwenda na kurudi, kutoka kijitonyama makumbusho hadi pasta masaa manne. Kutoka kariakoo mpaka mpaka makumbusho, makumbusho kwenda kawe, makumbusho kwenda mwenge na kurudi. Joto la dar unatembea kwa miguu mpaka vest inalowa jasho linaambukiza shati. Maji yananyweka sana jiji hili. Ni jiji kubwa sana kutembea kwa miguu ni shughuli pevu kulimaliza. Utoke kimara mpaka posta, gongolamboto kwenda kawe, kawe kwenda mbagala kwa miguu utachemsha tu
 
42km kwa mkimbiaji nzuri na kimashindano ni masaa 2+
Weweeee 59km kwa masaa 10 ilikuwa n milima gani hiyooo ulipanda mkuu
Ni kipaji alichonijalia Mungu mbali na mazoezi ninayofanyaga, ingawa sometimes nakimbiaga kwa zaidi ya dakika 70-75 lakini zoezi la kutembea huwa naenjoy sana.

NB:

Huwa naamka saa 8 au saa 9 usiku kutembea umbali namna hiyo.

Nilitokea Pugu, nikanyooka hadi Njiapanda Segerea, Kinyerezi hadi Magufuli Stand Mbezi mwisho na kugeuka.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ni kipaji alichonijalia Mungu mbali na mazoezi ninayofanyaga, ingawa sometimes nakimbiaga kwa zaidi ya dakika 70-75 lakini zoezi la kutembea huwa naenjoy sana.

NB:

Huwa naamka saa 8 au saa 9 usiku kutembea umbali namna hiyo.

Nilitokea Pugu, nikanyooka hadi Njiapanda Segerea, Kinyerezi hadi Magufuli Stand Mbezi mwisho na kugeuka.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nane hadi tisa usiku ni mida ya matukio mengi ya uhalifu , kuwa makinibusije ukauwawa au kupata kesi mbaya ya jinai
 
Posta 2 magomeni, sevaral times! Fire to mnazi mmoja many times
 
Mchakato wa kupata hati ya kusafiria ulinifanya nitembee kwa mguu kutoka Kurasini hadi Mlimani City mchana wa juakali.

Ilikua hivi:-
Tangu wakati niko chuo nilihangaikia sana suala la kuwa na passport ili niweze ku "access fursa za dunia." (Najichukulia kama mwananchi wa dunia, na sio mwananchi wa kipande kidogo cha dunia kiitwacho Tanzania pekee)

Kwangu mimi, kutokua na passport ilikua ni kama kifungo (nilijifananisha na mbuzi aliyefungwa kamba shingoni na kamba hiyo kufungwa kwenye mti). Hivyo kuwa na passport ingekua kama kuikata ile kamba na kuweza "kula majani" popote pale ambapo ningeweza kufika. A passport, was that important to me.

Kulingana na vigezo vya kuipata nyaraka hiyo ya kusafiria kuwa vingi, basi nilikumbana na "nenda rudi" nyingi sana hadi namaliza chuo sikufanikiwa kabisa kuipata hati hiyo.
Michakato hiyo (nenda rudi zisizozaa matunda) ilipelekea kupoteza pesa, kupoteza matumaini na furaha yangu.

Baada ya kupita kama mwaka mmoja na nusu hivi, kwa mbinde sana nilitimiza vigezo vya kuomba passport (japokua nilikua sina uhakika navyo sana kama "vitanivusha") na kwa mbinde zaidi nikapata pesa ya kugharamia mchakato huo.

Siku hiyo nimeenda pale uhamiaji makao makuu Kurasini, baada ya foleni kubwa, hatimaye nilifanikiwa kuhudumiwa majira ya saa saba mchana.
Nyaraka zangu zilipokelewa, zikakaguliwa, nikaambiwa nilipie, nikachukuliwa maelezo, nikapigwa picha na kuchukuliwa alama zangu za vidole na hatimaye nikaambiwa hati yangu itakua tayari baada ya siku 14.

Wakuu sikuamini, nilipata WEPESI WA AJABU. Yaani mwili ulikua soft, light and energetic. Namtabasamia kila mtu aliye mbele yangu.

Nikaanza tu kutembea, a joyful walk, napita tu vituo vya daladala sina habari, yaani nilikua ni kama kichaa mpya mjini. Juakali la saa saba kuelekea saa nane, saa tisa linaniwakia sina habari mimi.

Nilienda kusimama Mlimani City, Samaki Samaki kwa kaka mkubwa Carlito nilipoagiza Pepsi bariiiiiidi inayoambatana na glasi zenye mabarafu na vipande vya malimao.

Moral of the strory;-
Kufanikisha jambo (lolote lile) mara baada ya kulipambania kwa muda mrafu, kunaambatana na RAHA FULANI ambayo haielezeki.

Asanteni.

Pia aione Mwifwa
Chai
 
Nane hadi tisa usiku ni mida ya matukio mengi ya uhalifu , kuwa makinibusije ukauwawa au kupata kesi mbaya ya jinai
Huwa naamini nimezaliwa siku 1 na nitakufa siku 1 ambayo imepangwa na aliyenileta duniani.

Pia natokaga;

• Mwenge Mlalakuwa, Buguruni, Tazara hadi Gongo la Mboto. Kwa masaa matatu.

• Bandarini Posta hadi Gongo la Mboto.

• Chanika Zingiziwa hadi Gongo la Mboto.

• Mbagala Zakeem hadi Airport.

• Uhasibu, Mtongani kwa Aziz Ally, Tandika, Buza, Airport. Banana.

MOROGORO:

• Kihonda, Modeko, Msamvu, Masika.

• Mazimbu B (Solomoni), Tupendane, Stendi Mafiga, Misufini, Boma road, Stendi kuu ya zamani, Masika, Chamwino.

Huwa napenda sana kutembea hasa usiku au alfajiri kuepuka jua na naenjoy kama natalii vile.



Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Humu sijaona ruti ndefu ya mtu hata moja, mimi nilikuwa natoka kibamba mpaka kibada na ni kila siku, nilikuwa natembea bila kujua kuwa ni mbali mpaka pale nilipozoea jiji zima nazunguka kwa miguu tu, sikuwahi kupanda daladala mpaka narudi kijijini kwetu Magera, Morogoro.
Chai
 
Back
Top Bottom