Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

G/Mboto from Mzambarauni via Jet via Buguruni via Tabata Relini, nikatokea Ubungo, nikanyooka hadi Shekilango hadi Sinza Vatcan..... hii ilikua 1994, na mwisho wa daladala toka K/Koo, Posta nk ilikua ni pale G/Mboto Mzambarauni kabla ya Scolla House haijajengwa kmmk walahi...
Mkuu isiwe tulikuwa tunaishi nyumba moja!
 
Hahahahah unaweza ukafika ila uhakika wa kuamka kesho mzima ndio hakuna🤣
Hii siku ni kwel niliumwa sana maana ni kama week 3 zilikua zimepita toka nipate ajali ndogo maeneo ya Moroco mguu wa kushoto ukashtuka uliteguka kidogo.
Siku hii sasa baada ya kutembea sana nikaushtua...kesho yake ilkkua siku kuu ya Idd nilishinda nimelal tuuu😂😂😂
 
Hii siku ni kwel niliumwa sana maana ni kama week 3 zilikua zimepita toka nipate ajali ndogo maeneo ya Moroco mguu wa kushoto ukashtuka uliteguka kidogo.
Siku hii sasa baada ya kutembea sana nikaushtua...kesho yake ilkkua siku kuu ya Idd nilishinda nimelal tuuu😂😂😂
Dah pole sana. Mimi nakumbuka siku nilikadiria Mwenge nikatembea hadi Victoria pale. Nilijuta 🤣🤣🤣
 
Mliman city to Keko machungwa (Dealers) kupitia bara bara ile ya magari ya kwenda mbagala kupitia Taifa (sijui ndo Mandela road!!) Halafu ilikuwa usiku wa manane, tukitoka kwenye show ya wasanii na wanavyuo vikuu vilivyoko dar.

Ile show ambayo Mond aliwatuma wasanii wake wote wa wcb halafu yeye hakutokea, nadhani ilikuwa 2018 au 2017
 
Nakumbuka siku moja nikiwa Msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.

Ila kwa bahati nzuri kukawa na boti linaenda Kigamboni siku hiyo, basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taifa tukaangalie na Mpira kati ya Yanga na Mbeya city.

Alifurahi sana tulipofika Kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya kwake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilishashtuka ila nikawa najipa moyo.

Mpaka Mpira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Mazizini Mombasa to chang'ombe via Tazara
 
Daaaah mmenikumbusha mbali sana
1) nilikuwa nakaa kigambon mjimwema isitoshe nilikuwa mgeni wa jiji na mdogo kiumI baada ya kupata lift toka kibaha lilipokuwa gari la mjomba lilipokuwa limeharibika na kupewa lift mpka ubongo kipindi hicho nakumbuka dar nilikuwa najua njia mbili tu yaani mandela road na nyerere road kwakua tulikuwa tunazitumia Mara kwa Mara hivo nilitoka ubongo via mandela mpka tazara Kisha nikaikamata nyerere road mpka ferry nikashika pantoni Kisha nikaendelea kuitafuta mjimwema

2) gongolamboto mpka mnazimmojq hizi nimezaliwa sana mpka nikazizoea

3) kinondoni manyanyq mpka tabata barakuda

UMASIKINI NIKITU KIBAYA NA HAUMPENDEZI MTU TUUKATAE KWA NGUVU ZOTE
 
Back
Top Bottom