Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Dar moro siku mbili usiku na mchana. Barabara hiyo ina vibwengo kama wote. Sitaweza kusahau.
Tupe kidogo Mikasa ya huko barabarani mkuu mkutembea kwa miguu toka Moro - Dar simchezo,,,

maana hii hali iliwahi kukaribia kunitokea siku moja, bado kidogo sana nitembee kwa miguu kutoka msavu hadi ubungo!

Bahati njema alitokea msamaria mmoja nisiye mjua akanisaidia nauli 5000 wakati huo nauli ya Moro - Dar ni 2500 , nilikaa stand ya msavu toka asubhi mpaka jioni bila bila,,, msamaria huyo alinipa nauli imeshakuwa jioni sana karibu saa moja na dakika zake usiku!

Nikapanda coaster ya mwisho kabisa kuja ubungo! Tukafika Ubungo mida ya saa tano usiku! Kisha nikachukua daladala hadi k/koo then nikachukua lingine la kuja home Kurasini, nilifika home saa saba usiku!

Sitasahau! Yule msamaria Mungu ambariki sana kokote aliko!
 
Coco Beach to mabibo
Mabibo hostel to kariakoo
Hizii route nimepiga Sanaa mdg mdg ty huwa na mentality ambayo nimeizoea kutoka mkoa kwmb sina ulazima wa kupanda daladal wakat na uwezo wa kutembea [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Alikuwa anatembea huyo, mimi nilitembea mwendo wa kawaida kabisa km 32 kutoka makete wilayani hadi ikonda kwa masaa 6 kasoro. Ina maana km 42 ningezimaliza kwa masaa 7 au 8 kwa kutembea.
Watu wanadhani hizi ni kamba ila kiukweli laiti Bongo kungekuwa na mashindano ya kutembea kama Ulaya naamini ningeng'oka na medani.

Picha linaanza umesomea primary & sekondari vijijinini kwa zaidi ya miaka kadhaa ukitafuta shule kwa km 23 × 2 = km 46 (kwenda na kurudi), sasa utashindwaje kutembea km 59 kwa masaa 10 tena huenda ukazidi hapo ukiweka bidii tokana na maisha uliuokulia.

Kukimbia ndiyo huwa najilazimisha kwa dakika 75 na mazoezi ya viungo dakika 10/15, bado ujana unalipa.

Kinachonihasishaga haswa ni vipi ikiwa Mungu atanijalia neema ya maisha marefu, nitafika miaka 70 nikiwa na afya njema au nitakuwa napambana na BP, KISUKARI, SONONA n.k?

NB:

Kesho huandaliwa na leo.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mikocheni Magomeni, Mbagala mpaka Keko, Posta mpaka Kimara, Posta mpaka Mabibo Sokoni.


Ilala mpaka Tabata kisha Tukamalizia Tabata mpaka Ubungo hii nilikuwa na jamaa yangu alikuja na mfuko wa Nozzle za Scania na Man Diesel tukawa tunapita madukani na gereji zote hiyo njia kuziuza safari ikaishia Ubungo Terminal ndani kwenye gari mbovu mbovu.
 
Nakumbuka siku moja nikiwa Msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.

Ila kwa bahati nzuri kukawa na boti linaenda Kigamboni siku hiyo, basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taifa tukaangalie na Mpira kati ya Yanga na Mbeya city.

Alifurahi sana tulipofika Kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya kwake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilishashtuka ila nikawa najipa moyo.

Mpaka Mpira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Kawe kariakoo kariakoo Mabibo mwenge kawe kazi ya kuuza miwa kwenye toroli miwa tunanunulia Tandale enzi hizo chezea shida wewe unatnbea kila siku zaidi ya kilometa 25
 
Achana na Dsm

Nilikuwa Mbeya maeneo ya Isanga Tankini, nikapigiwa simu kuna kitu nikifate Nzovwe maeneo ya Iyunga.

Hapo sina nauli

Nikasema sio ishu, nitapiga lwa mbwa haste haste hadi Nzovwe kupitia njia ya hapo Sokomatola, stendi kuu kushuka na kimtetemko cha meta.

Nikafika Nzovwe, mgongoni nilikuwa nimebeba Rasket ambapo ndani yake kulikuwa na vitu vyangu vya muhimu.

Nikatua Rasket nikatoa vitu vilivyokuwa ndani ya Rasket ili niweze kupanga vizuri nipate nafasi ya kuweka hicho kitu nilichokifuata.

Baada ya kukamilisha na kuona kila kitu kipo sawa, nikawaaga nikawa narudi zangu Isanga haste haste.

Nikafika mpaka home huku nikiwa nawatambia wanangu kuwa daladala ni za mademu, mwanaume lazima ukanyage lwa mbwa.

Nikatoa vile vitu kwenye Rasket, katika hali isiyoya kutarajia nikagundua kuna property moja ime miss.

Nikaanza kuvuta kumbukumbu nikagundua ule wakati nikiwa Nzovwe natoa vitu, navyoruishia ndio niliposahau kukirudishia.

Ikabidi kwanza nipige simu Nzovwe ku confirm, wakaniambia kweli nimekisahau.

Kwa hiyo nikawa na root nyingine ya kurudi tena Nzovwe lwa mbwa.
Mimi nimepiga sana route ya Old Forest mpaka Sae kule kwenye transformer za Tanesco.
 
Enzi za kwenda kuogelea Coco Beach unatoka Magomeni unapitia rafiki Kinondoni mnatembea mpaka Coco Beach, mnaogelea kisha mnasogea kwa kutembea mpaka Dar Yatch kushangaa Boti, Slip Way mkifika Msasani Fish Market hapo ni kutembea kando ya Bahari ufukweni mnapita kwa Nyerere nyuma ya nyumba, Dar Independent School, Mbalamwezi Beach, Kwa Mzee Bomani, Mzee George Kahama, Escape One Beach Mpaka Kawe Beach hiyo jioni mpo hoi.

mnarudi kwa njia za chochoro Mikocheni B, Wastaafu street, Warioba mnapita barabara ya Lucy Lameck nyuma nyuma mpaka mitaa ya Kairuki kuitafuta Morroco na Kinondoni unafika Magomeni hoi nguo zina mchanga kichwani mchanga.

Saizi kuipita route hizo kasheshe
 
1995
TEMEKE - POSTA - TEMEKE
Tena TEMEKE yenyewe ni TEMEKE mwisho, Mtaa wa Kitomondo.
 
Back
Top Bottom