Jambo hili nafikiri lingesubiri kwanza na lisifanyike kabisa katika ofisi na hospitali za umma. Kwa sababu Daktari ameajiliwa na kusaini mkataba wa kutumikia umma wa watanzania kwa muda wote atakaohitajika hospitalini kuhudumia wagonjwa.
Hatua hii na ruhusa hii ya Waziri ni hatari Sana kwa watanzania wanyonge wasio na uwezo wa kumuona daktari kwa muda huo wa ziada. Kwa kuwa hii inaweza kuwafanya madaktari na watumishi wa Afya kugeuza hospitali za umma Kama hospitali binafsi katika koti la hospitali ya umma, pia hatua hii itazolotesha utoaji wa huduma kwa watanzania wanyonge ili kuwalazimisha waje muda wa ziada ambapo gharama lazima ziwe za juu Sana
Watanzania wengi watapoteza maisha kwa kukosa huduma Bora na kukosa hela ya kumuona daktari muda huo ambao dactari atasema Ni wa ziada na anatakiwa alipwe hela kwa makubaliano binafsi,pia hatua hii itawafanya baadhi ya madaktari kupunguza ufanisi muda wa kazi ili wawavute wagonjwa wengi muda wa ziada wanaojuwa watajipatia pesa Yao binafsi.
Hospitali za umma zibaki kuwa hospitali za umma tu na siyo kufanya hivyo,Kama serikali inaona vipato vyao yaani mishahara na stahiki zingine haziwatoshi Basi iwaongezee mishahara zaidi,marupurupu, fedha za over time iwalipe kwa wakati,iboreshe mazingira ya hospitali kwa kuhakikisha vifaa Tiba,Dawa na wahudumu wa Afya wapo wa kutosha ili wasielemewa na mzigo wa kuhudumia wagonjwa.
Tunaweza kufanyia majaribio maeneo mengine lakini katu na kamwe hatupaswi kuleta mzaha Wala majaribio na Afya za watanzania wanyonge, hatupaswi kuweka maisha ya watanzania rehani,hatupaswi kuwatelekeza watanzania kwa kuweka hospitali ndani ya hospitali,mfumo ndani ya mfumo pasipo hata maandalizi ,hili nasema hapana Tena hapana.maisha yetu watanzania nayafahamu Sana na hata Mimi nikiona mzazi wangu anaumwa huwa Namuomba Mungu amponye maana hatuna uwezo wa kugharamia au kubeba gharama kubwa pale tutakapo hitajika kufanya hivyo.
Hospital za umma ziendelee kuboreshwa na kuwaboreshea maslahi watumishi wake ili kuongeza morali ya kazi lakini siyo kwa njia hiyo pendekezwa na mh Waziri ummy mwalimu, nasema jambo hili lisifanyike na pia viongozi wetu wa kisiasa yawapasa kuwa makini katika utoaji wa matamko kwa kuwa mengine yanaweza kuleta athari kubwa Sana hasa kwetu wa kipato Cha chini ambao hatuna uwezo wa kuwaona madaktari huo muda wa ziada.
Unafikiri Ni Daktari yupi ambaye hatapenda kuwekeza muda wa ziada kuhudumia wagonjwa? Unafikiri Daktari yupi ambaye hatawashawishi wagonjwa wake muda wa ziada? Unafikiri daktari atafanya kazi kwa juhudi muda wa kazi Kama ule wa ziada? Sasa Kama tunaruhusu hili kufanyika kulikuwa na kunakuwa na haja gani ya kupiga marufuku maduka ya watu binafsi kuwa karibu na hospitali za umma?
Mimi Nafikiri Kama serikali inalenga kuwaongezea vipato madaktari wetu ambao nami pia nawapenda ,Kuwaheshimu na kuthamini mchago wao Basi ingejikita katika kuwaongezea maslahi yao na kuboresha zaidi mazingira ya kazi.
Namshauri mh Waziri wangu kutengua kauli yake kabla haijaanza kufanyiwa kazi,.Nasema kuwa Afya za watanzania Ni muhimu Sana,sisi uwezo wetu wa kipato Ni mdogo Sana na ndio maana wengi Sana hatuna hata tu bima ya Afya Wala kuwa na uwezo wa kufanya vipimo binafsi vya Afya walau kila mwaka,chonde Sana serikali yangu nawaombeni Sana katika hili kutuonea huruma wanyonge nakutambua kuwa Afya ndio mtaji wetu.