Kabla ya kuchangia kwenye Uzi huu wa mkuu
Kilatha , naomba ku declare interest kuwa Mimi ni professional and practicing medical Dr. Nina uzoefu wa kufanya kazi kwenye hospitali za Umma na binafsi, mjini(DSM) na peripheral.
Baada ya kusoma Uzi wako, nimelazimika kumsikiliza mh Waziri Mara tatu kujua msingi wa hoja yako. Niliyoyabaini:
Mosi, uelewa wako kwenye moja ya nguzo za maadili na miiko ya udaktari ' Non maleficence' una kasoro. Ni kweli, wewe ni public health specialist or whatever, lakini umeshindwa kudadavua principle hiyo with respect to kile Waziri amezungumza.
Pili, uzoefu wako kwenye masuala ya Upatikanaj na ukusanyaji wa damu salama ni mdogo. Huenda ninyi ndo wale ambao immediately after internship mlisoma MPH, so uzoefu wenu kwenye ground ni mdogo Sana.
Tatu, ama hufahamu majukumu ya Waziri au umeamua umseme tuu kwa kuwa ulikusudia walau kuwa na Uzi hapa Leo. Binafsi, sioni kosa lolote kwa Waziri kuhamasisha watu kujitolea damu. Na sera ya wachangiaji wa damu wa hiari kupewa kipaumbele pale wanapokua na mahitaji ya damu, hili sio suala la Ummy. Ni mkakati wa muda mrefu wa damu salama ambapo mchangiaji hupewa kitambulisho ambacho akienda nacho sehemu yoyote atatambulika na endapo akihitaji damu, atapatiwa Kama ipo hospitalini hapo. Ni mkakati wa muda mrefu, hata kabla mh Waziri hajawa Mbunge.
Baada ya kumsikiliza mh Waziri, nami naomba niunge mkono maagizo yake kwa kusema:
1. Serikali kuhakikisha mifuko ya damu inapatikana bure itarahisisha shughuli nzima ya ukusanyaji damu, na huenda ikaongeza idadi ya watu wanaochangia damu kwa hiari. Kwa sababu, Kuna baadhi ya sehem mfuko mmoja/tupu unauzwa Tsh 10000, so hii itasaidia kupunguza mzigo kwa familia ya mgonjwa.
2. Suala la mgonjwa anayeongezewa damu kuhimizwa kuwa na watu wa kufanya replacement ya damu hio. Kila mmoja wetu atakubaliana na Mh kuwa, hakuna kiwanda Cha damu zaidi ya mwili wa mwanadamu. Na kuwa, kibongo bongo kumwambia mtu achangie damu Wakati haumwi, majority hatuna utayari huo, utasikia kila mtu,' hata mimi niliyonayo hainitoshi'. So, tukisema mtu aongezewe tuu theni tutegemee damu inayokusanywa na timu za ukusanyaji damu salama, hatutoboi. Tumewahi kujaribu Hilo, kukatokea shortage kubwa and huenda some of people humu walipoteza relatives kwa kukosa damu. so, tuache kuingiza siasa kwenye afya za watu, twende na uhalisia. Nikiwa hospitali mojawapo mjini ambako suala la replacement lilikua linawekewa mkazo Sana, ilikua nadra kusikia mama mjamzito amekufa kwa kukosa damu, which is different to the peripheral nilipokua, ambako walikua wakizua utaratibu wa lazima wa ndugu kufanya replacement. Kwa mwaka mmoja, tulishuhudia zaidi ya vifo vya akina mama 30 vitokanavyo na Uzazi na wengi wakifa kwa kukosa damu.
Tuwe wakweli, tuache kuingiza siasa kwenye kila Jambo. Tumuunge mkono Mh Waziri, tumshauri kwa staha na tuzitumie elimu zetu kwa manufaa ya Umma.
Asante.
KAMWENE.