Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vinaweza kusababisha kile alichokiita "kimbunga cha njaa" na uhaba wa chakula kote duniani.
Alisema nchi nyingi za Afrika na maskini zinategemea zaidi uzalishaji wa ngano wa Urusi na Ukraine, ambayo sasa iko hatarini kutokana na mzozo huo.
Hii ni pamoja na Burkina Faso, Somalia na Yemen ambazo tayari zinahangaika kulisha watu wao.
Bw. Guterres ametoa wito wa kusitishwa kwa vita hivyo mara moja ili kuepuka kuharibika kwa mifumo ya chakula duniani.
Pia alitangaza kifurushi cha $40m (£31m) kusaidia mamilioni ya Waukraine wanaokabiliwa na njaa na kupungua kwa usambazaji wa maji na dawa.
BBC Swahili