Umoja wa Mataifa: Afrika itakumbwa na uhaba wa ngano kutokana na vita vya Urusi na Ukraine

Umoja wa Mataifa: Afrika itakumbwa na uhaba wa ngano kutokana na vita vya Urusi na Ukraine


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vinaweza kusababisha kile alichokiita "kimbunga cha njaa" na uhaba wa chakula kote duniani.

Alisema nchi nyingi za Afrika na maskini zinategemea zaidi uzalishaji wa ngano wa Urusi na Ukraine, ambayo sasa iko hatarini kutokana na mzozo huo.

Hii ni pamoja na Burkina Faso, Somalia na Yemen ambazo tayari zinahangaika kulisha watu wao.

Bw. Guterres ametoa wito wa kusitishwa kwa vita hivyo mara moja ili kuepuka kuharibika kwa mifumo ya chakula duniani.

Pia alitangaza kifurushi cha $40m (£31m) kusaidia mamilioni ya Waukraine wanaokabiliwa na njaa na kupungua kwa usambazaji wa maji na dawa.

BBC Swahili
Afrika hatuwezi kuendelea kutegemea chakula cha kulima kama ngano kutoka Ulaya ni wakati wetu muafaka kujiongeza wenyewe kwenye kilimo cha ngano na mazao mengine ya biashara
 
Back
Top Bottom