Umoja wa Ulaya yaimwagia sifa Tanzania. Yaahidi kuendelea kumwaga mapesa

Naomba unisaidie kuelewa. Hiz
Hizi wanazotupatia ni misaada au mikopo? Naomba ufafanuzi kabla hatujasonga mbele.
 

Bado hujaelewa vizuri, hata huyo Rodney nadhani hujamuelewa (kama umesoma hicho kitabu chake). Ni kwamba, kwa sasa wanatoa hicho wanachoita 'misaada' ili wachukue vingi na kwa urahisi zaidi, kwa njia ya mbali mbali hasa kwa kupitia mikataba yenye masharti ambayo mara nyingi hayawekwi wazi. Mikopo naye inakuja na riba pamoja na masharti mbali mbali yenye lengo la kuendeleza agenda za watoaji.

Huwo ni mkakati maalum wa kiuchumi na ni sehemu ukoloni mamboleo. Kiongozi yoyote wa Afrika atakayepinga hilo lazima apate misukosuko sana.

Usishangilie hata siku moja unaposikia umepewa 'misaada'. Hao wanaotoa wana shida nyingi tu ndani ya nchi zao. Na hata hawana habari na hicho unachosema 'kurukdisha sehemu ya walichoiba'. Ajenda yao ni kutafuta namna ya kuchukua kwa urahisi zaidi.
 
Mwislam akinitembelea nyumbani kwangu nikampikia kitimoto atanishukuru sana kwa ukarimu wangu lakini ataniambia kwa unyenyekevu kabisa kuwa dini yake inakataza kula nyama hiyo na ataomba wapewe watoto wale sisi tukiendelea na mazungumzo yetu. Baada ya mazungumzo yetu tutaagana kirafiki kwa kukumbatiana na kutakiana kheri lakini akisha ondoka na kufika mbali ataanza kunitukana sana kwa kumpikia kitimoto huku nikijua yeye ni Rashid. Wafadhiri hawa wanamwaga hizo fedha kwa Wananchi ziwasaidie katika maendeleo yao ndo maana hawatoi pesa zao kwenda kwenye Miradi ya wakubwa kama vile SGR, Stiegler's Gorge, Madege, Busisi, Chato International Airport na mingine. Wafadhiri wana watu wao hapa na wanajua wale Wasiyojulikana bado wapowanangoja tu maagizo waende kazini maana kazi inaendelea. Fedha hizo ni za walipa Kodi wao na wanajua namna fedha za Kodi zetu zinavyowanufaisha wakubwa Wananchi wakiachwa solemba na kuwaongezea matozo lukuki mpaka tunabanwa hadi kushindwa kupumua wakidai hiyo ni COVID 19 tu tuendelee kuchanjwa.
 
"...Ukitaka kula ni lazima uliwe...." JK

Wanatoa mshiko huo wakijua watapa nini cha faida zaidi bila kujali wanachotoa kitawanufaisha wananchi wa kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…