Umoja wa wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Wajitetea kuhusu kupanda kwa Sukari. Hawajawahi kuficha Sukari, Si kazi yao kuagiza Sukari nje
Wanatakiwa wazalishe sukari ya kutosha ili watu tununue kwa bei ya chini. Porojo zingine hazina maana.

Inawezekana bashe alikiuka taratibu lakini hao aliowapa vibari vya kuingiza sukari waliingiza hiyo sukari nchini au walishindwa? Kama waliingiza na sisi tunahitaji sukari basi hakuna sababu kubwa ya kuendelea na mijadala ya hii kitu

Bashe atakuwa amejifunza kuhusu kufuata taratibu na wenye viwanda wamejifunza kwamba wasipozalisha sukari ya kutosha soko lao litachukuliwa na watu wa nje
 
Hali ya Bashe sasa itadhidi kuwa mbaya baada ya Kilombero Sugar kutema cheche

View attachment 3031040
Wazalishaji sukari wavunja ukimya, wadai kutotendewa haki sakata la sukari

Aurea Simtowe

Muktasari:

Baada ya kushutumiwa kwa muda mrefu na kutajwa kuwa wao ndiyo chanzo cha kupanda kwa bei ya sukari nchini, umoja wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) wavunja ukimya.

Dar es Salaam
. Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi.

Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari leo Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Kwa hivyo, waliomba utaratibu wa uagizaji sukari uwekwe.

Licha ya ufafanuzi huo, itakumbukwa siku chache zilizopita, kulikuwa na mijadala sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye Bunge lililoahirishwa Ijumaa Juni 28, 2024 iliyokuwa ikiwatuhumu wafanyabiashara hayo kuhusika katika kusababisha bei ya sukari kupanda bei.

Baadhi ya watu katika mijadala hiyo walidai wazalishaji wanatengeneza nakisi ya sukari kwa makusudi ili waweze kujinufaisha, jambo ambalo Mpungwe anasema si kweli.

“Kulikuwa na mawasiliano na si mara moja wala mbili, tulikuwa tunakumbushia na kweli ilipofika Desemba hali ikaanza kuwa vile tulivyosema,” amedai Mpungwe.

Amesema cha kushangaza, hadi Desemba vibali vya kuagiza sukari vilikuwa havijatoka na Kampuni ya Sukari Kilombero ikalazimika kuizuia meli yake iliyokuwa inapeleka tani 45,000 ya sukari nchi nyingine na kuagiza iingizwe nchini kwa lengo la kufidia upungufu mkubwa uliojitokeza.

Mpungwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kilombero Sugar, amesema si kweli kwamba kampuni hizo zilipewa vibali vya kuagiza sukari na kuviuza.

Amesema kazi ya uagizaji sukari kutoka nje si yao, wao ni wazalishaji tu na hulazimika kuingilia kati kwenye usambazaji kama kuna uhaba nchini kama walivyofanya kwa lengo la kukabiliana na uhaba na vurugu kama zilizokuwepo.

“Sisi kama Kilombero hatutaki kuingia katika biashara ya kuagiza sukari, tuko katika biashara ya kuzalishaji sukari, hili wazo la kuweka chombo cha Serikali kuagiza sukari nadhani lingekuja tangu mwanzo tungeunga mkono,” amesema Mpungwe.

Amesema wazalishaji hao waliamua kukaa kimya pale waliporushiwa maneno kwa sababu walikuwa wakiwasiliana na Spika wa Bunge ili wapate nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kilimo na Viwanda, lakini walipangiwa kukutana Agosti, mwaka huu.

“Tulipewa nafasi ya kukutana na kamati ya uchumi na bajeti wiki iliyopita, lakini ilikuwa ni kuzungumzia muswada wa fedha, tulijitahidi kuwa na mawasiliano lakini uamuzi umetoka bila sisi kuhusishwa tumekuwa watuhumiwa hadi tumehukumiwa bila sisi kusikilizwa,” amesema Mpungwe.

Amesema kutuhumiwa kwamba hawawafikirii Watanzania zaidi ya milioni 60 si sawa, kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa unaodumu kwa zaidi ya miaka 60.

“Tumeshutumiwa kuwa sisi ni cartel ni tuhuma nzito katika biashara, huwezi kuwa na mpango mkubwa wa kuwekeza ukajiingiza katika mambo haya na tuhuma hizi haziamriwi kisiasa,” amesema.

Amesema kama kuna hofu kuwa wawekezaji hawa wanacheza mchezo mchafu kwenye biashara, wapelekwe Tume ya Ushindani (FCC), wakajibu tuhuma zao huko.

Naye Mwakilishi wa Bagamoyo Sugar, Hussein Sufian amesema kauli ya kuvitaka viwanda vya sukari kutoficha sukari wakati hakuna kiwanda kilichowahi kuficha sukari, sio sahihi.

Amesema wamejengewa taswira mbaya isiyo na ukweli kwa washirika wa maendeleo ya sekta ya sukari na umma kwa jumla.

Kuhusu dhamira ya kuondokana na uzalishaji sukari nchini ili kuleta sukari ya nje na wakulima kuhamasishwa kulima mazao mbadala kama mpunga, amesema inadhoofisha jitihada zilizokwishafanyika za kuleta utulivu kwenye sekta ya sukari.

Wakati hayo yakisemwa, Sufian amesema pia sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama kubwa za uzalishaji.

“Gharama za mahitaji muhimu kwa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni pia uwepo wa sera zisizotabirika za soko la sukari ni tatizo,” amesema Sufian.

Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba kutaka kujua undani wa malalamiko hayo, akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa; “Ningekushauri kwa hoja kama hizi ni vyema ukaanza na wizara ya sekta husika.”

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alipoulizwa kuhusu barua zilizoandikwa na TSPA aliomba kutumiwa ujumbe mfupi ambao haukujibiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Naibu wake, Joseph Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweri simu zao ziliita bila kupokelewa.
Maelezo haya yote ni mazuri, lakini cha kujiuliza ni nini kiliwaziba midomo kupelekea hadi akina Mpina kujeruhiwa kwa hila?

Kwanini wasingelitoa ushuhuda wa tamko hili mapema haraka iwezekanavyo ili kuuweka ukweli wa tuhuma hizo potofu mapema?

Tz imegawika kwa kunyamazia maneno haya kwa kushindwa kuyatoa kwa wakati.

Wengi wapo upande wa Waziri kwa namna walivyoaminishwa na maneno yake ya shobo juu ya tuhuma nzito kuhusu wenye viwanda kuweka mazingira ya uhaba.

Ni wachache tu wenye akili kubwa ndiyo wapo na Mpina baada ya kutumia jicho la tatu kuusaka ukweli wa mambo.

Mnakujaje kutoa ushahidi wa mtu aliyetuhumiwa kwa kesi ya mauwaji ya uongo na tayari alikwisha hukumiwa na adhabu ya kunyongwa ilishatekelezwa?
 
Wanakuwaga wagumu hao kuelewa somo; kwa ule ushahidi wa Mpina hayuko peke yake nyuma yake kuna kundi.

Kwa kifupi Bashe ongea na ‘bi-tozo’ gurudumu la ufisadi kilimo ampe mtu mwingine akutoe hapo kwa usalama wako. Jamaa wamekuchoka na ujambazi unaofanya huko, uamini subiri.

Report ya CAG kila ikija imeja madudu ya upigaji sehemu zenyewe unakuta Bashe ndio alilazimisha hela zipelekwe huko.
Hujaona hayo mapapa yanavyohaha hapo? Bila Bashe ungeyajuwa hayo?

Wao wazalishe sukari, Bashe huko kishafunga mjadala, sasa hakuna cha kibali hakuna cha nini., NFRA wanahakikishsa wanaipata sukari popote ilipo mradi ghala lao la kuhifadhi lisipunguwe tani 200,000 za sukari.

Wananunuwa kwa nani kazi kwao.
 
Hali ya Bashe sasa itadhidi kuwa mbaya baada ya Kilombero Sugar kutema cheche

View attachment 3031040
Wazalishaji sukari wavunja ukimya, wadai kutotendewa haki sakata la sukari

Aurea Simtowe

Muktasari:

Baada ya kushutumiwa kwa muda mrefu na kutajwa kuwa wao ndiyo chanzo cha kupanda kwa bei ya sukari nchini, umoja wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) wavunja ukimya.

Dar es Salaam
. Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi.

Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari leo Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Kwa hivyo, waliomba utaratibu wa uagizaji sukari uwekwe.

Licha ya ufafanuzi huo, itakumbukwa siku chache zilizopita, kulikuwa na mijadala sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye Bunge lililoahirishwa Ijumaa Juni 28, 2024 iliyokuwa ikiwatuhumu wafanyabiashara hayo kuhusika katika kusababisha bei ya sukari kupanda bei.

Baadhi ya watu katika mijadala hiyo walidai wazalishaji wanatengeneza nakisi ya sukari kwa makusudi ili waweze kujinufaisha, jambo ambalo Mpungwe anasema si kweli.

“Kulikuwa na mawasiliano na si mara moja wala mbili, tulikuwa tunakumbushia na kweli ilipofika Desemba hali ikaanza kuwa vile tulivyosema,” amedai Mpungwe.

Amesema cha kushangaza, hadi Desemba vibali vya kuagiza sukari vilikuwa havijatoka na Kampuni ya Sukari Kilombero ikalazimika kuizuia meli yake iliyokuwa inapeleka tani 45,000 ya sukari nchi nyingine na kuagiza iingizwe nchini kwa lengo la kufidia upungufu mkubwa uliojitokeza.

Mpungwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kilombero Sugar, amesema si kweli kwamba kampuni hizo zilipewa vibali vya kuagiza sukari na kuviuza.

Amesema kazi ya uagizaji sukari kutoka nje si yao, wao ni wazalishaji tu na hulazimika kuingilia kati kwenye usambazaji kama kuna uhaba nchini kama walivyofanya kwa lengo la kukabiliana na uhaba na vurugu kama zilizokuwepo.

“Sisi kama Kilombero hatutaki kuingia katika biashara ya kuagiza sukari, tuko katika biashara ya kuzalishaji sukari, hili wazo la kuweka chombo cha Serikali kuagiza sukari nadhani lingekuja tangu mwanzo tungeunga mkono,” amesema Mpungwe.

Amesema wazalishaji hao waliamua kukaa kimya pale waliporushiwa maneno kwa sababu walikuwa wakiwasiliana na Spika wa Bunge ili wapate nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kilimo na Viwanda, lakini walipangiwa kukutana Agosti, mwaka huu.

“Tulipewa nafasi ya kukutana na kamati ya uchumi na bajeti wiki iliyopita, lakini ilikuwa ni kuzungumzia muswada wa fedha, tulijitahidi kuwa na mawasiliano lakini uamuzi umetoka bila sisi kuhusishwa tumekuwa watuhumiwa hadi tumehukumiwa bila sisi kusikilizwa,” amesema Mpungwe.

Amesema kutuhumiwa kwamba hawawafikirii Watanzania zaidi ya milioni 60 si sawa, kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa unaodumu kwa zaidi ya miaka 60.

“Tumeshutumiwa kuwa sisi ni cartel ni tuhuma nzito katika biashara, huwezi kuwa na mpango mkubwa wa kuwekeza ukajiingiza katika mambo haya na tuhuma hizi haziamriwi kisiasa,” amesema.

Amesema kama kuna hofu kuwa wawekezaji hawa wanacheza mchezo mchafu kwenye biashara, wapelekwe Tume ya Ushindani (FCC), wakajibu tuhuma zao huko.

Naye Mwakilishi wa Bagamoyo Sugar, Hussein Sufian amesema kauli ya kuvitaka viwanda vya sukari kutoficha sukari wakati hakuna kiwanda kilichowahi kuficha sukari, sio sahihi.

Amesema wamejengewa taswira mbaya isiyo na ukweli kwa washirika wa maendeleo ya sekta ya sukari na umma kwa jumla.

Kuhusu dhamira ya kuondokana na uzalishaji sukari nchini ili kuleta sukari ya nje na wakulima kuhamasishwa kulima mazao mbadala kama mpunga, amesema inadhoofisha jitihada zilizokwishafanyika za kuleta utulivu kwenye sekta ya sukari.

Wakati hayo yakisemwa, Sufian amesema pia sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama kubwa za uzalishaji.

“Gharama za mahitaji muhimu kwa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni pia uwepo wa sera zisizotabirika za soko la sukari ni tatizo,” amesema Sufian.

Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba kutaka kujua undani wa malalamiko hayo, akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa; “Ningekushauri kwa hoja kama hizi ni vyema ukaanza na wizara ya sekta husika.”

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alipoulizwa kuhusu barua zilizoandikwa na TSPA aliomba kutumiwa ujumbe mfupi ambao haukujibiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Naibu wake, Joseph Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweri simu zao ziliita bila kupokelewa.
Waziri Bashe anatakiwa kujiuzulu hafai kuongoza Wizara ya kilimo. Laiti ningelikuwa ndio mimi Rais wa Nchi ningesha litumbuwa hilo jipu lakini wapi Mama Abdul anamlinda Waziri Bashe Mama anawalinda Mafisadi wa nchi wanaosababisha hali ya maisha ya watu wa chini kuwa ni ngumu. Ewe Mungu tusaidie sisi Walala hoi na nchi yetu na utupe viongozi ambao wenye uchungu wa kuipenda nchi yao na wananchi walala hoi na masikini amin yarabi.
 
Waziri Bashe anatakiwa kujiuzulu hafai kuongoza Wizara ya kilimo. Laiti ningelikuw andio mimiRais wa Nchi ningesha litumbuw ahilo jipu lakini wapi Mama Abdul anamlinda Waziri Bashe Mama anawalinda Mafisadi wa nchi wanaosababisha hali ya maisha ya watu wachini kuwa ngumu. Ewe Mungu tusaidie sisi Walala hoi na nchi yetu na utupe viongozi ambao wenye uchungu wa kuipenda nchi yao na wananchi walala hoi na masikini amin yarabi.
Wapenda nchi upinzaji wananunuliwa na CCM kuupunguzia upinzani nguvu hapo wananchi watafanya nini. Watetezi wao wanavunjwavunjwa na watesi kuongezeka
 
Mjinga huyu, dalali anayetumiwa kufanya lobbying serikalini, alianzia Tanzanite. Hii kampuni ya Kilombelo ndio Mkapa aliichukua kwa mgongo wa wananchi.

Hawa wajinga ndio wamemuhonga Mpina na kulipia vyombo vya habari kila kimoja 10,000,000
hii nchi bana waandishi wa habari wananunuliwa,wapinzani wananunuliwa,viongozi wa dini wananunuliwa na chama Tawala, ccm ni balaa kubwa wananchi mtaponea wapi?Amkeni Bunge hili balaa
 
Tunaweza kuzunguka na kutengeneza fitina, lakini ukweli utabakia pale pale, BASHE NI FISADO PAPA. Bilioni 36 amezitembeza vizuri kwa wabunge wala rushwa. Na ukifuatilia, wabunge waliokula mlungura ni walewale wa DP W, wakiongozwa na Musukuma, ambaye DP W walimpa dola 50k, nyumba Dubaina V8.
 
Hujaona hayo mapapa yanavyohaha hapo? Bila Bashe ungeyajuwa hayo?

Wao wazalishe sukari, Bashe huko kishafunga mjadala, sasa hakuna cha kibali hakuna cha nini., NFRA wanahakikishsa wanaipata sukari popote ilipo mradi ghala lao la kuhifadhi lisipunguwe tani 200,000 za sukari.

Wananunuwa kwa nani kazi kwao.

..wauza vocha wataruhusiwa kuagiza sukari au wameshatosheka walivyopiga?
 
Mpaka sasa nimewasikiliza jwa dakika 30, naendelea kuwasikiliza lakini cha kusikifisha wanaongelea siasw na porojo nyingi. Kuwa "watazalisha" sukari ya kutosha kuanziq mwaka huu.

Pambaf kabisa, walikuwa wapi siku zote mpaka Bashe kaja kuwatia vidole vya masikio ndiyo wanasikia kuwa Watanzania wameathiriwa na bei za sukari?

Hawa wazalishaji hawatakiwi kutupigia porojo, wanatakiwa wazalishe sukari ishuke bei.

Ujinga mtupu.
Dini yetu inaongoea binti
Ukiwa sober tatakari upya
 
Hao wengine wote hawajapendewzewa mwendazake alivyompa shamba Bakhresa.

Bakhresa hayupo kabisa katika ujinga wao hao.

Unafahamu kuwa sukari anayozalisha Bakhresa mpaka sasa hata yeye mwenyewe kwa matumizi ya viwanda vyake haimtoshi?
Bwege wew Habari inasema umoja wa watengeneza sukari kiwanda Cha bagamoyo nclusive

Naona unajitahidi kutetea dini lakini unajichanganya
 
Back
Top Bottom