Umri huu ni kete yako ya mwisho, ukikosea ni majuto hadi unaingia kaburini

" Huyu mwanaume anaboa, hamna matukio kabisa, haya mahusiano yanaboa"

Kama umeshawahi kukutana na mtu wa aina hii utagundua binadamu tunatamani jambo la utofauti kila wakati hivyo siku zote tunaona tulikosea kufanya maamuzi ndo maana usishangae kukutana na tajiri hana furaha.
 
Wakati mwingine wanadamu tunatengeneza scenerio kwenye maisha yetu yanayotupa tabu na mahangaiko yanayopelekea kukosa Raha za maisha na kuyajutia maisha........

Chini ya jua wanadamu tumekosa au hatuna udhibiti wa mambo mengi yanayoendelea au kutokea maishani mwetu kinyume na matakwa ya nafsi zetu......

Kila mwanadamu ni shahidi wa nafsi yake na ni kawaida ya nafsi kupendelea mambo mazuri.......lakini wakati mwingine mambo hutokea maishani ambayo huleta matokeo kinyume na matakwa ya nafsi au matarajio yetu............

Tusipende kuyapima mambo yetu kwa umri wetu au mitazamo ya watu wengine wanaoonekana kama kwamba wametuacha mbali.....

Katika mlango wa kiimani kuna nguvu kubwa juu ya mienendo yetu na sisi nguvu zetu ni ndogo kubadilisha matokeo ya nguvu hizo......

Ishi maisha yako kwa uwezo wako na kwa namna ulivyorudhukiwa na muumba.... nyakati na umri ni mambo ya kiulimwengu ambayo yako nje ya uwezo wako.......

Usipende kupima mafanikio na umri wako ndio chanzo kikuu na kuiondosha furaha maishani mwako......
 
umeandika vizuri ila suala la kujutia kwasababu ya kuzaa watoto wachache HAPANA kwakweli watoto wengi zama hizi ni mzigo tu uwe na hela usiwe hela watoto wengi ni mzigooo.. naenda zangu
 
Nyakati hizi vijana wa umri huo wakike na kiume, ni kweli, wachache wanajuta tena sana lakini wengi wao wala hawajali, hawana habari, hawana mipango na wala hawatishiki kabisa na hali hiyo ni Mwendo wa kula Bata tu......
 
At 26yrs nishaaza kujuta,najuta kwanini sikukaza shule asee mzee wangu kafariki akiwa na kinyongo na mimi kwasababu ya hili.
I hate myself
Relax bro. Kuhusu shule wengi tuna majuto. Tumepishana tu viwango. Kuna mtu alienda Advance na One ya 9 halafu six akapiga div. IV, Mwingine aliingia chuo na one kali ila akatoka na G.P.A ya kishenzi.
 

Kijana,

Umenena vyema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…