ITR
JF-Expert Member
- Sep 22, 2022
- 6,096
- 16,390
Labda kwenye jamii yako ww.Sijui nani katudanganya wanaume kuwa kwenye swala la ndoa na mahusiano wanaume hatuchuji, hata sisi tunachuja, kuchuja kwa mwanaume kunaanza taratibu kuanzia miaka 30+, mwanaume wa miaka 35 ukitaka oa mdada wa miaka 21, hapo mara nyingi mdada atakuwa anakupendea pesa, maana atakuona ushaanza kua mzee. Mwanaume anakuwa na soko kwenye mahusiano pale anapoanza kubalehe (16-23)
Labda na wadada wa humu jf watuongezee ujuzi kidogo Kelsea Numbisa Ms R To yeye Madame B binti kiziwi Jadda ITR
Kwa hiyo mwanaume usipo pendewa kwa aset zako ulizo nazo utapendewa nini, au ndo nyinyi mnao shinda humu mnalilia mapenzi ya kuonewa huruma na wanawake ? Ya kwamba mwanamke akupende tu hata kama huna faida yeyote kwenye maisha yake?
Kanuni ya maisha ni moja japo mnajifanya kuikwepa hasa nyinyi vijana wa siku hizi na yenyewe ni hii.
Thamani ya mwanamke kwenye mahusiano huwa iko kwenye mvuto wa mwili wake, hivyo kadri miaka inavyo enda thamani yake huwa inapungua kwenye soko la mahusiano kwa sababu mwili utaenda unapoteza mvuto ,na ndio maana kigezo kikubwa cha mwanamke kuolewa huwa ni uzuri na tabia yake.
Wakati huo thamani ya mwanaume huwa ni mali zake alizo nazo, na ndio maana mwanaume akitaka kuoa kigezo cha kwanza kinacho angaliwa ni uwezo wako wa kumtunza huyo mwanamke na watoto utakao zaa naye.
Kingine mwanaume ana uwezo wa kuamua muda wa yeye kuoa , wakati hiyo nafasi mwanamke hana.
Alafu kingine hakuna lika la wanaume wenye soko kubwa kwenye ndoa kama rika la kuanzia miaka 30 kwenda juu,mabinti wengi huwa hawataki kuolewa na wanaume chini ya miaka 30.