Umri unapokuwa umeenda na hujaoa au kuolewa unakabiliana vipi na maneno ya jamii inayokuzunguka?

Umri unapokuwa umeenda na hujaoa au kuolewa unakabiliana vipi na maneno ya jamii inayokuzunguka?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Kumekuwepo na maswali Mengi katika jamii ambayo umri wako ukiwa umeenda huwa hayakwepi kama vile
siku hizi uko wapi?

Bado unaishi palepale kwenu au unajitegemea?

Kama umesoma utaulizwa umeshapata kazi?

Lakini kuna swali moja ambalo wengi wetu tukiuliza huwa hatupendi kuliongelea nalo ni unaowa lini au utaolewa lini ?

Kama upo katika mahusiano utaulizwa ndoa lini ?

Ili kukabiliana na hii situations unafanyaje ili uweze kuihandle ndani ya jamii iliyokuzunguka.
 
Kuanzia leo waambie una mchumba tayari ila kwa mila zao haruhusiwi kuja kujitambulisha mpaka kaka yake aoe kwanza.

Wakitaka picha njoo pm niwe nakutumia picha mbalimbali.
Wala sina mpango.
 
Ni kuwajibu tu kuwa unasubiria wakati wa Bwana ufike, kama Ndoa ipo ipo tu na kama Ndoa haipo haipo tu na maisha lazima yaendelee kwa Neema za Mungu.
 
Tunavumilia hivohivo..hasa wanawake
Nkiulizwa ntaolewa lini,najibu Mungu akipenda.wengine tuna changamoto za kimaisha kiafya zinazotufanya iwe ngumu kuolewa
Na zaidi sifanyi maamuzi kumfurahisha mtu.nafanya moyo wangu ukiwa umeridhia
Mimi hujibu ukioa au kuolewa wewe inatosha. Hili swali huwa common kwa wanaume sana
 
Back
Top Bottom