Swali la utaoa au kuolewa lini ni swali la unyanyapaa linaloingilia uhuru wa mtu.
Mtu asiyekuhusu akikuuliza hivyo, muulize, kwani tulikubaliana kuhusu hilo?
Pengine unaukizwa na watu wa karibu kwa maoenzi mazuri tu, pengine wanatafuta wajukuu.
Kuna siku mtu ambaye kifamilia ninamuheshimu kabisa aliwahi kuniuliza hilo.
Nilimjibu kitu kimoja tu.
"I don't want to talk about that".
Habari nzima ikafikia tamati hapohapo, na yeye akajua sipendi mjadala juu ya jambo hilo, kama kuna habari nitamueleza.
Sasa inategemea na familia yenu ikoje, inawezekana jibu hilo likakubalika, au likaonekana la dharau.
Kwetu lilikubalika nikaachiwa uhuru wangu.