Kuna mambo mengi haujaelezea kama vile historia ya tatizo, je ulikuwa hivyo tangu zamani au imetokea wakati huu?
Una mahusiano na watu wangapi je na huko inakuwa hivyo? Uzito wako kilo ngapi, unaona uko katika uzito sahihi?
Kazi zako na michakato yako inakupa muda wa kutosha kupumzika? Kama umeoa mke unampenda au ilibidi tu?
Lishe yako vipi, unaweza kusema unakula vyakula vya aina gani zaidi, je ni mlo sawia/kamili(balanced diet).
Una historia ya magonjwa au ugonjwa unaoshambulia njia ya hewa? Unatumia bidhaa kama pombe,sigara au dawa?
Mi nakushauri yafuatayo kabla ya dawa;
Kunywa maji ya kutosha, sio mengi sana wala kidogo sana kulingana na uwezo wako, achana na sayansi za lita tano kwa siku. HAIFAI.
Loweka karanga mbichi kiganja kimoja katika maji kwa muda wa nusu saa mpaka lisaa kisha tafuna mpa umalize, hili fanya kabla ya kifungua kinywa au kabla ya chakula cha mchana, HAPA TUNAREKEBISHA PROTINI NA NISHATI UTAKUWA UNAJISKIA HAUCHOKI KIRAHISI HATA KATIKA SHUGHULI ZA KAWAIDA.
PUNGUZA VYAKULA VYA MAFUTA, SUKARI NA BIDHAA ZA SUKARI, chai ya sukari nyingi,soda, bia.
Ukiamka asubuhi kojoa kwa mafungu matatu mpaka manne, yani kojoaa halfu kata mkojo bila kubana tumbo wala sehemu ya haja kubwa(hapa ni pagumu kidogo, jitahidi yani usibane sana sehemu ya haja kubwa) hapa ni kama unakuwa gym ya uume
Wakati huu ukijirekebisha fanya tendo mara moja kwa siku tano.
Siku moja kabla ya game loweka mdalasini katika maji ya kunywa glasi moja.
Siku au wakati wa game usishibe sana, tumia ndizi mbivu mbili piga game, kisha kula nyingine mbili wakati wa breki. Tumia muda mwingi kucheza cheza na mwenzako.
Ziada penda kula ndizi mbivu, tikiti maji, mara kadhaa jioni kunywa kahawa kikombe kimoja