Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Kwa nini wasingefanya siku ya Jumapili kama ilivyokuwa kwenye uchafuzi?!! Sawa mimi nitaacha taarifa zangu kwenye ghetto langu sasa sijui watazipataje!!!!
 
Mambo ni kujipanga tu hakuna kinachoshindikana.

Kuna watakaokuwa safarini pia bila shaka mipango ipo maana watu wa takwimu ni Wasomi wazuri tu.
 
Yaani kwangu labda waje kuanzia saa3 usiku hata wakisema ni mapumziko,maisha yenyewe ndio haya tukae home na wife tule nini na watoto?life wameliseti wenyewe limekua gumu kama nini!nitawaachia namba ya simu mlangoni wanipigie labda
Hilo neno. Nitaacha namba ya sinu
 
Wapeni taarifa wapate data zakwenda kuombea mikopo nje, lakini pia usawa na ufanisi katika ugawaji wa keki ya Taifa.
 
Wewe nani wa kuishauri serikali....
Watanzania wamepiga kura kuwachagua viongozi ila hawajui lengo la kuwachagua hao viongozi ,kama umepigiwa kura lazima uchukue ushauri WA hao waliokuchagua maneno yako hapo juu inaonesha ni namna gani hujui kazi ya serikali period nendeni darasani
 
Na kuna hii nimeikuta mahali...

Ndugu zangu watendaji huko serikalini naombeni kuconfirm kama siku ya sensa ni siku ya kazi kama kawaida…. And if yes I am worried na quality ya data tutakazozipata …. Few thoughts/concerns

1. Ijumaa nilifanyia kazi nyumbani bahati nzuri kata ya kawe wakawa wanafanya pre-testing na ikaangukia nyumbami kwangu … sikuwa nimejiandaa lakini niliwapokea vizuri and it took two hours kumaliza

2. Kwa maswali yale ya pre- testing wakisema twenda makazini , I have a serious concern na data watakazocollect…. House helpers kamwe hawataweza jibu maswali yote yale …. They are many and detailed in actual fact hata mkuu wa kaya mwenye wakati mwingine atahangaika

3. Mama makinda hapo anasema tuache taarifa nyumbani …. Taarifa zipi na ni nani atajua taarifa gani za kuacha hakuna hata mwongozo… yale maswali yapo kwenye categories nyingi na ni mengi sasa mtu atajua ni taarifa gani za kuacha home? Mfano kama kaya yako inawakazi sita na wote wana NIDA utahitaji kutoa namba zao zote za nida as per the questionnaire, lakini pia kuna taarifa za elimu, vizazi na vifo katika kaya …. Ni house girl gani atakuwa na hizo data zote?

4. Uwezo wa wahojaji wenyewe siyo mkubwa ukilinganisha na maswali halafu ndo aje akutane na house helper …. Itakuwa garbage in garbage out huyu mtoto alokuja hapa kwangu for pre testing it was a disaster mpaka nikaihurumia nchi yangu…. Ilibidi mpaka nimwulize kiwango cha elimu akanambia anasoma VETA lakini ni kadogo na hana confidence kabisa ya kuuliza …. I had to help him maana natamani saana zoezi hili lifanikiwe….

I wish wa reconside hii decision kwakweli…. We need quality data for our next ten years plans.
 
Kwa hiyo maofisi yafungwe siku saba? Maana ndani ya siku Saba utakuwa umehesabiwa haijatajwa "kwenu" watafika lini. Acha watu wafanye kazi wewe kaa nyumbani subiri sensa ikishapita nenda kachukue kilicho chako kwenye desk lako ofisini uje usubiri matokeo ya sensa nyumbani.

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Moja ya swali ni kipato cha wastani cha kaya. Kwa hiyo umuachie housegirl au jirani hiyo taarifa kwamba bwana wastani wa kipato changu kwa mwezi ni laki 1.
 
Nikiangalia zoezi la postkodi za mitaa lilivyofanyika na lilikuwa zoezi rahisi sana na lilikuwa "straight forward" lakini matokeo yakawa na walakini kwa kiasi kikubwa, napata mashaka sana iwapo hili la sensa litafanikiwa kwa jinsi lilivyo gumu zaidi ya zoezi la postkodi. Vipi hili zoezi la sensa ambalo ni muhimu zaidi aachiwe beki tatu kwa kiasi kikubwa atoe taarifa za familia labda ya watu sita. Na ikumbukwe kuwa hao mabeki tatu wengine hata kusoma hawajui.

Vinginevyo labda ijulikane tu wazi hili zoezi la sensa ni zoezi la kutimiza tu ratiba kwa vile huu ni mwaka wa sensa basi tunafanya tu sensa mpaka mwaka mwingine wa sensa ufike. Muda bado upo kwa serikali kulitafakari hili suala kwani kufeli kujua idadi ya watu kwa usahihi basi ndio mwanzo wa kufeli kwa mipango mengine mingi ya maendeleo. Walau siku yenyewe ya sensa yaani tarehe 23/08/2022 ikiwa siku ya mapumziko serikali itapata kwa asilimia kubwa taarifa sahihi hata kama siku zinazofuata taarifa hazitakuwa sahihi sana.

Kwa heshima na taadhima naiomba serikali iangalie mara mbil mbili kipi bora hasara ya siku moja ya watu kutokwenda kazini au hasara ya muda mrefu ya kutokuwa na takwimu sahihih ambazo zitaisadia nchi kwenye mipango yake mbali mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…