Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nini wasingefanya siku ya Jumapili kama ilivyokuwa kwenye uchafuzi?!! Sawa mimi nitaacha taarifa zangu kwenye ghetto langu sasa sijui watazipataje!!!!Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.
Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.
Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.
Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.
Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.
Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu
View attachment 2326622View attachment 2326626
Hilo neno. Nitaacha namba ya sinuYaani kwangu labda waje kuanzia saa3 usiku hata wakisema ni mapumziko,maisha yenyewe ndio haya tukae home na wife tule nini na watoto?life wameliseti wenyewe limekua gumu kama nini!nitawaachia namba ya simu mlangoni wanipigie labda
Watanzania wamepiga kura kuwachagua viongozi ila hawajui lengo la kuwachagua hao viongozi ,kama umepigiwa kura lazima uchukue ushauri WA hao waliokuchagua maneno yako hapo juu inaonesha ni namna gani hujui kazi ya serikali period nendeni darasaniWewe nani wa kuishauri serikali....
Serikali unadhani ni ya mama yako?Wewe nani wa kuishauri serikali....
Ndiyo maana nchi haiendeleiWaajiriwa mnapenda kuongezewa mishahara lakini ni wavivu.
Kwamba ungekuwa umejiajiri hata ingetangazwa ni mapumziko usingeenda kwenye shughuli zako?
Kwa hiyo maofisi yafungwe siku saba? Maana ndani ya siku Saba utakuwa umehesabiwa haijatajwa "kwenu" watafika lini. Acha watu wafanye kazi wewe kaa nyumbani subiri sensa ikishapita nenda kachukue kilicho chako kwenye desk lako ofisini uje usubiri matokeo ya sensa nyumbani.Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.
Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.
Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.
Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.
Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.
Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu
View attachment 2326622
View attachment 2326626
Moja ya swali ni kipato cha wastani cha kaya. Kwa hiyo umuachie housegirl au jirani hiyo taarifa kwamba bwana wastani wa kipato changu kwa mwezi ni laki 1.Sioni logic, why upumzike siku moja wakati zoezi ni la siku saba, bora ungesema upumzike siku 7.
Imagine mkoa kama Dar es salaam, EA moja tu wanaweza wasimalize plus hata huko vijijini (mf longido kwa wafugaji) maeneo yako very scattered na namna akifikika.
Kuhusu questionnaires sidhani kama ni very secret kiasi hicho kwamba hata dada wa nyumbani asipewe kuepuka UHAINI ndani ya familia [emoji28]
Maswali kama mna choo na mnakitumia, mmeala wangapi usiku wa 23 agost, uchumi wenu unategemea nini, mkuu wa kaya ni jinsia gani nk nk.
Hakuna maajabu sana kwamba questions ni classified kiasi hicho
Kwani sensor ni siku ngapi?Kama kweli maswali ni mengi kiasi hicho watu watachoka na itaathiri usahihi wa taarifa