Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 4,486
- 8,098
cc Samia Suluhu Hassan.Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.
Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.
Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.
Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.
Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.
Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu
View attachment 2326622
Jesus is Lord