Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa

Ndugu wana jamvi nmeona Serikali imetoa taarifa kuwa Ile siku inayotangazwa Sana ya Sensa kuwa sio siku ya mapumziko. Kiukweli niseme serikali inakosea Sana na haitapata taarifa sahihi kabisa.

Kuna Baadhi ya nyumba hakuna anaebaki Nyumbani hivyo hata wakienda kesho yake hawatakuta mtu maana wote wanaenda kazini.

Pia wanasema ukiondoka uache taarifa zako Kwa anaebaki. Hilo ni ngumu Kwa vile sio Kila niliepanga nae ninamuamini kiasi cha kueza kumuachia taarifa zangu zote binafsi.

Pia Kwa wale walio na wadada wa kazi haiwezekani kuanza kumuambia mdada wa kazi taarifa zangu na familia Kwa ujumla maana ni kama kuwa wazi sasa kitu ambacho sio wote tupo tayari.

Pia hawajasema ni taarifa zipi ambazo zinatakiwa kuachwa ili wakija waweze jibiwa maana tangazo linasema Tu taarifa ziachwe Nyumbani.

Naishauri serikali hiyo siku waifanye iwe ya mapumziko ili kuondoa hizi dosari lasivyo watapata taarifa potofu kuwa tumefika 67m kumbe tupo pungufu
View attachment 2326622
cc Samia Suluhu Hassan.

Jesus is Lord
 
View attachment 2326622View attachment 2326626
Wanaongea upuuzi,tuwe tumeacha taarifa zetu kwani tunajua watauliza maswali Gani?

Huku ni kutojielewa, yaani siku ya usafi ya Magufuli day watu hawafungui biashara kwa ajili ya usafi Kwa masaa 5 harafu zoezi muhimu la sensa linachukuliwa poa?

Ngoja watapata wanachokitafuta ,may be Wana uzoefu wa sensa za awali.
 
Naiona kabisa hela ya mlipa Kodi ikipotea bure yaaan. Labda kama Wana idadi wanataka kuipika yaaan. Hajasema taarifa zinazohitajika wanataka niote Tu kumuachia jiran yangu au
 
Yaani kwangu labda waje kuanzia saa3 usiku hata wakisema ni mapumziko,maisha yenyewe ndio haya tukae home na wife tule nini na watoto?life wameliseti wenyewe limekua gumu kama nini!nitawaachia namba ya simu mlangoni wanipigie labda
 
Sioni logic, why upumzike siku moja wakati zoezi ni la siku saba, bora ungesema upumzike siku 7.
Imagine mkoa kama Dar es salaam, EA moja tu wanaweza wasimalize plus hata huko vijijini (mf longido kwa wafugaji) maeneo yako very scattered na namna akifikika.

Kuhusu questionnaires sidhani kama ni very secret kiasi hicho kwamba hata dada wa nyumbani asipewe kuepuka UHAINI ndani ya familia 😅
Maswali kama mna choo na mnakitumia, mmeala wangapi usiku wa 23 agost, uchumi wenu unategemea nini, mkuu wa kaya ni jinsia gani nk nk.

Hakuna maajabu sana kwamba questions ni classified kiasi hicho
 
Kama hicho ndio wameamua basi washachemsha...

Labda kama wana mpango wa kuhesabu nyumba na mitaa...
 
Sioni logic, why upumzike siku moja wakati zoezi ni la siku saba, bora ungesema upumzike siku 7.
Imagine mkoa kama Dar es salaam, EA moja tu wanaweza wasimalize plus hata huko vijijini (mf longido kwa wafugaji) maeneo yako very scattered na namna akifikika.

Kuhusu questionnaires sidhani kama ni very secret kiasi hicho kwamba hata dada wa nyumbani asipewe kuepuka UHAINI ndani ya familia [emoji28]
Maswali kama mna choo na mnakitumia, mmeala wangapi usiku wa 23 agost, uchumi wenu unategemea nini, mkuu wa kaya ni jinsia gani nk nk.

Hakuna maajabu sana kwamba questions ni classified kiasi hicho
Hivi unadhani swali la uchumi wenu unategemea kitu gani bila kuambiwa umuachie beki tatu majibu utajuaje hivi unafahamu kuwa kuna maswali kama 100 hivi kwenye Dodoso dogo
 
Kiukweli Serikali iwe serious hasa inapoamua kutumia pesa zake. Ili kufanikiwa taarifa sahihi, nashauri Serikali ifanye siku za sensa angalau mbili za mwanzo ziwe public holiday.

Hii itawezesha kufanya zoezi la kupata taarifa liwe bora. Kwa watu busy wanaoenda kazini kila siku ni ngumu taarifa hizo kumuachia dada wa kazi, labda kama Serikali inachukulia sensa kama formality tu.
 
Ndo nashangaa ata Mimi,kama serikali imeamua kutumia ela mlipa Kodi kufanya sensa basi wajitahidi zoezi liwe Bora wasifanye kulipua lipua
 
Naiona kabisa serikali ikiharibu hela ya Mlipa Kodi kwa kiwango cha kutisha. Serikali haitapata data na takwimu sahihi kuhusu wananchi wake.
 
Kwanza hili litakuwa kichaka Cha wezi kuingia majumbani kwa watu mchana wakijifanya maafisa wa sensaa na kuiba bila wasichana wa kazi kujua malengo yao
 
Mtaa ninaoishi 50% ya wana kaya wake wanaishi peke yao. Je, hizo taarifa watamwachia nani hapo nyumbani? Hili zoezi linaweza lisiwe na ufanisi uliokusudiwa.
 
Inasemekana Dodoso (Questionnaire) lina maswali zaidi ya 100 ambayo hatuyajui yatahusu nini. Hivi kweli naweza kubuni vitu zaidi ya 100 watakavyouliza zaidi nikamfahamisha beki 3 na asisahau hata kimoja kweli??

Kama kweli maswali ni mengi kiasi hicho watu watachoka na itaathiri usahihi wa taarifa
 
Back
Top Bottom